top of page

Matibabu ya kisukari aina ya 2

 

Imeandikwa na Dkt. Mangwella Sospeter(MD)

Kiwango rejea kina choshauriwa kwa watu wengi wenye kisukari*

  • A1C** % 7.0 au chini

  • FBG/Kiwango cha sukari kabla hujala kitu asubuhi(mmol/L) 4.0-7.0

  • Kiwano cha sukari masaa mawili baada ya kula(mmol/L) 5.0 hadi 10(5.0-8.0) kama A1C** rejea hakishafikiwa

Maelezo ya ziada

*kiwango hiki kimeshauriwa na shirika la Canadian Diabetic association 2013 huu ni mwongozo

***A1C ni kipimo cha kiwango cha wastani wa kudhibiti sukari katika miezi 2 hadi 3iliyopita na asilimia 30 ya matokeo ya majibu hutokana na kiwango cha siku 30 zilizopita.

Kila baada ya miezi 3 unatakiwa kupima kipimo cha A1C, unapima endapo hufiki kiwango rejea cha sukari au kama unabadili matibabu ya kisukariKipimo hiki hufanyika kabla na baaad ya kula pia.

 

 

4.Kudhibiti kiwango cha sukari ukiwa unaumwa

Ukiwa unaumwa, kiwango chako cha sukari kinaweza kubadilika au kutotabilika. Wakati huu, ni jambo la msingi kupima kiwango chako cha sukari mara nyingi kuliko kawaida (mfano kila baada ya masaa mawili au manne) ni vema pia kuendelea kutumia dawa zako za kisukari kama una mafua ya kuchuruzika na unataka kutumia dawa za mafua mwombe mfamasia wako akuchagulie chaguzi nzuri ya dawa au ongea na daktari wako. Madawa mengi ya kutibu mafua na kikohozi huwa na sukari hivyo jaribu kuchagua dawa zisizo na sukari.

Ikiwa unaumwa ni muhimu kufanya yafuatayo;

  • Kunywa maji mengi na vinywaji visivyo na sukari, epuka kahawa, chai ,cola kwani huwa na caffeine inayoweza kusababisha kupoteza maji mengi.

  • Kula vitu vya majimaji vyenye glukosi badala ya vitu vigumu ambavyo huwezi kula kulingana na utaratibu wako.

  • Jaribu kutumia gramu 15 za wanga kila saa

  • Fuata utaratibu wako wa kila siku wa chakula

  • Mtafute daktari wako kwa simu uede kwenye huduma ya dharura endapo unatapika au unaharisha mara mbili au zaidi ndani ya masaa manne na

  • Kama unatumia sindano ya insulin, hakikisha unaendelea kutumia dozi yako wakati unaumwa. Ongea na daktari wako kuhusu marekebisho ya dozi wakati unaumwa.

 

 

Wasiliana na daktari wako siku zote kwa ushauri na tiba kabla ya kuchukua hatu yoyote

Pata ushauri na tiba kutoka kwa daktari wa ULY clinic kwa kubonyeza hapa au piga namba za simu chini ya tovuti hii.

Imeboreshwa 12.03.2020

Rejea

Kiwango cha sukari kinachohitajika
Kudhibiti kiwango cha sukari
Kudhibiti sukari ukiwa unaumwa
bottom of page