Madhara ya kisukari
Madhara ya mda mfupi (madhara ya ghafla)
1. Kushuka kwa sukari
Kukabiliana na tatizo la kushuka na sukari kwenye damu
2.Diabetic ketoacidosis
3.HHS
Madhara ya kisukari
​
Imeandikwa na Daktari wa ULY clinic
​
Madhara yanayotokea kwa mda mfupi na madhara yanayotokea kwa mda mrefu
​
Madhara ya mda mfupi (madhara ya ghafla)
​
1.Kushuka kwa sukari
​
Sukari kushuka chini ya kiwango cha kawaida (chini ya 3.5mmol/L), tatizo hili linatokana na matumizi ya dawa hasa aina ya sulphonyurea au sindano za insulin kuliko kusababishwa na ugonjwa wenyewe. Pia pombe, mazoezi makali, kutokula chakula, kula chakula kidogo au kutofuata ratiba ya kula.
Kushuka kwa sukari hutokea sana pale, kabla ya kula, unapokuwa unafanya mazoezi, mda mfupi baada ya kujichoma sindano ya homoni insulin, kiwango cha pombe kikiongezeka wakati kiwango cha chakula kimebaki kilekile. Pia wakati wa usiku ambapo mchana wake ulikuwa na mazoezi mengi au umejidunga insulin nyingi kabla ya kulala au ulkula kidogo au hukula kabisa.
​
Dalili zake huwa kati ya hizi;
​
-
Kutokwa na jasho mwilini
-
Njaa kali
-
Mwili Kutetemeka
-
Kuwa na hwasiwasi sana
-
Moyo kudunda kwa nguvu
-
Kuchanganyikiwa
-
Kushindwa kuongea
-
Kulegea sana kwa mwili
-
Kushindwa kumanikia jambo
​
Pia dalili zingine zisizo rasimi ni kama kichefuchefu, kuchoka mwili na kichwa kuuma
Kumbuka:
-
Si kila mtu anapata dalili zote hizo, ni baadhi tu, na pia ni vema kuangalia wewe unapata dalili gani. Kumbuka kupima kiwango cha sukari katika damu kwa utaratibu maalumu (inashauriwa mtu mwenye kisukari aina ya 1 kupima mara 4 hadi 5 kwa siku, kabla ya kula mlo wowote, na wakati wa usiku mida ya sa nane au tisa- mara moja kwa wiki)
-
Kwa jinsi unayopima sukari yako katika dam undo jinsi unavyojua kiwango chako na kuwa na uwezo wa kudhibiti kama imeshuka au kupanda. Usisahau kuweka rekodi katika kitabu chako pale unapopima sukari.
-
Hakikisha umeongea na ndugu na jamaa wanaoishi nawe ili waweze jua dalili za sukari kushuka chini ya kiwango ili waweze kukusaidia endapo wewe utakuwa hujitambui au kushindwa kuongea wakati huo. Kama ukishindwa kutambua kushuka kwa sukari ubongo ukikosa sukari unaweza kupata matatizo makubwa na utapoteza fahamu. Pia kumbuka kubeba kiutambulisho kwamba wewe unakisukari.
​
Kukabiliana na tatizo la kushuka na sukari kwenye damu
​
Unaweza kufanya haya mara sukari yako inappokuwa imeshuka chini ya 3mmol/L
-
Chukua maji safi na kuweka glukosi vijiko viwili kisha kunywa au kuweka sukari vijiko viwili na kunywa kama huduma ya kwanza
-
Kunywa soda kama ipo karibu
-
Kunywa gramu 3 au tano za kidonge cha sukari
-
Kula zabibu wingi wa kiganja kimoja cha mkono
-
Kunywa vijiko viwili vya asali
-
Maziwa yasiyo na mafuta glasi moja na pia waweza kula biskuti
-
Kula pipi sita
​
-
Diabetic ketoacidosis-DKA
Hili ni tatizo linaloambatana na kiwango kikubwa cha kemikali za ketone na sukari katika damu kwa sababu ya kukosekana kwa homoni ya insulin kwenye damu, hutokea sana kwa wagonjwa wenye kisukari aina ya 1.
​
Tatizo la DKA mara nyingi huwa na visababishi, mara nyingi huwa ni hivi vilivyoambatanishwa chini;
-
Kusahau kujichoma dozi yako ya insulin
-
Kusahau dozi mojawapo ya insulin
-
Kutoongeza dozi ya insulin wakati unaugua
-
Maambukizi kwenye mwili (kama maambukizi ya malaria, bakteria kwenye damu, maambukizi ya njia ya mkojo)
​
DKA huambatana na dalili hizi;
-
Dalili za kisukari( kiu ya mara kwa mara, kukojoa mara kwa maraji
-
Dalili za kuishiwa maji mwilini kama vile kukauka midomo, na ngozi kuwa kavu
-
Maumivu makali ya tumbo maeneo ya kuzunguka kitovu- kukosa hamu ya kula, kichefuchefu na kutapika
-
Kupooza kwa matumbo
-
Mapigo ya moyo kwenda kasi
-
Kushuka kwa shinikizo la damu unapokuwa umesimama
-
Uwezo wa kiakili kupungua- uwezo wa kujitambua
-
Kupumua kwa kina zaidi na kwa haraka sana
-
Kutoa harufu nzuri kinywani
-
Kupoteza fahamu
-
Sukari kupanda zaidi ya 33 endapo utapima kwenye kipimo(au huweza kuonyesha HIGH pasipo kuonyesha namba)
-
Mwili kuwa dhaifu sana
-
Kuonekana kwa ketone kwenye mkojo ukipimwa
​
​
Mgonjwa huyu atahitaji matibabu ya haraka sana hospitali kwenye chumba chenye uangalizi wa makini (ICU)
Matibabu ya awali unayoweza kufanya wakati unampeleka hospitali ni
​
-
HHS
​
Ni aina ya tatizo linalotokea kwenye wagonjwa wenye kisukari aina ya 2 huwa na dalili chache za awali na huambatana na dalili hizi
-
Kukojoa sana
-
Dalili za kuishiwa maji mwili(kukauka kwa midomo, ngozi kuwa kavu)
Hatua za mwisho ni kama kupigwa na degedege, kuzimia, au kifo cha ghafla.
Vihatarishi/visababishi vyaweza kuwa;
-
Kuugua
-
Kushindwa kudhibiti kiwango cha sukari mwilini kwa mda mrefu
-
Msongo wa mawazo
-
Dawa na chakula- kama vile vunywaji vyenye kahawa, pombe na dawa aina ya diuretics zinazotumika kutibu shinikizo la juu la damu, dawa aina ya steroid, cimetidine, na dawa ya aina ya phenytoin
-
Wagonjwa wa figo wanaofanyiwa dialysis
​
HHS yaweza kuzuiliwa kwa kupima sukari yako mara kwa mara kulingana na ulivyoshauriwa na daktari wako, haswa pale ukiwa unaumwa waweza kupima zaidi ya mara mbili kwa siku.
Kumbuka
Endapo umetambua mgonjwa mwenye tatizo hili basi ni vema kumuwahisha hospitali haraka akapate matibabu
​
Wasiliana na daktari wako siku zote kwa ushauri na tiba kabla ya kuchukua hatu yoyote
​
​
Imeboreshwa 12.03.2020
​
Rejea​