top of page

Madhara sugu

Imeandikwa nadr mangwella sospeter MD

Imepitiwa na Dr.Kisa kapaga MD

Kuna baadhi ya mambo ya kijeni na uwezo wa kudhibiti sukari yanayoweza kutabiri mtu  gani atapata madhara ya kisukari hapo mbeleni. Mtu aliyedhibiti sukari yake kwa kiwango kinachoshauriwa huishi vema kama mtu asiye na kisukari.

 

Kutokea kwa madhara hutokana na kubadilishwa kwa glukosi kwenda sorbitol kwenye damu, kemikali hii ni sumu kwenye tishu mbalimbali mwilini.

Kuna ushahidi wa kisayansi kwamba kudhibiti vizuri sukari huweza kuzuia madhara mengi yanayoweza kutokea kutokana na kisukari.

 

Wasiwasi uliopitiliza

Ni kawaidakupata wasiwasi au hofu wakati Fulani katika maisha na kila mtu huwa na hali hii, wasiwasi wa kiasi huweza kuwa ni vema kwa sababu hukusaidia kupambana na hatari mbaya na huweza kukupa hamasa ya kufanya vizuri shuleni au kazini.

Lakini kama una wasiwasi mara nyingi bila sababu na wasiwasi huo unaathiri maisha yako, basi una tatizo la wasiwasi. Tatizo la wsiwasi linaweza kusababisha hofu iliyopitiliza na zisizo za kweli dhidi ya hali mbalimbali za kimaisha bila kuwa na kisababishi kinachojulikana.

Mahusino kati ya tatizo la wasiwasi na kisukari haufahamiki vema, lakini tafiti zinaonyesha kuwa kiwango cha wasiwasi kwa watu wenye kisukari huwa kikubwa. Wasiwasi kwa watu wenye kisukari huweza kusababisha tatizo katika kudhibiti kiwango cha sukari katika damu.

Dalili za mtu mwenye tatizo la wasiwasi huwa kama hizi

  • Kutotulia

  • Kujihisi mwenye fadhaa au umefikia ukomo

  • Kuhisi uvimbe kwenye koo lako

  • Kushindwa kutulia kwenye jambo moja kimawazo

  • Kuchoka

  • Kutokuwa mvumilivu

  • Kupotezwa kimawzo haraka na jambo fulani

  • Misuli kukaza

  • Kutopata usingizi au kushindwa kuendelea kulala

  • Kutokwa na jasho jingi

  • Kuishiwa pumzi

  • Maumivu ya tumbo

  • Kuharisha

  • Kichwa kuuma

Matibabu ya wasiwasi huhusisha matibabu ya dawa na maongezi maalumu, huweza kutumika kwa pamoja au unaweza kupewa aina moja ya matibabu.

Ongea na daktari wako endapo unahisi kwamba unatatizo la wasiwasi kwa ushauri na matibabu.

Ugonjwa wa celiac

Tatizo hili huonekana sana kwa watu wenye kisukari aina ya 1 kuliko kwa watu wengine, hutokea kwa asilimia 4 hadi 9 ya watoto wenye kisukari aia ya 1 na kati yao asilimia zaidi ya 50 huwa hawana dalili. Watoto wenye kisukari aina ya 1 wanahatarishi ya kupata ugonjwa huu.

Nini maana ya Ugonjwa wa celiac?

Ni tatizo linalotokana na kinga za mwili kupambana dhidi ya protini ya gluten inayopatikana kwenye ngano. Ngano hutumiwa katika utengenezaji wa bidhaa mbalimbali kama mkate, sambusa, maandazi n.k. kama una ugonjwa wa celiac basi ukitumia vitu viilivyoengenezwa kwa ngano kinga yako ya mwili utapambana nayo na kuababisha uharibifu kwenye kuta za tumbo lako na hivyo ufyonzwaji protini, mafuta, wanga,vitamin, na madini hupungua.

Tatizo hili la celiac hurithiwa kutoka. Ndugu wa damu wa karibu (dada, kaka, watoto wa dada) wa mtu mwenye tatizo la celiac huwa na hatari ya kupata tatizo hili pia bila hata kutambulika. Huweza kuonekana kwenye kipindi chpchote kile cha maisha ya mtu, na hurithiwa. Sababu za kimazingira kama msongo wa mawazo, ujauzito, upasuaji, maambukizi(nimonia, kuhara) huweza kuamsha tatizo hili la celiac.

Dalili

Mara nyingi watu wenye tatizo la celiac huwa hawana dalili kabisa, ndio maana tatizo huwa halitambuliwi. Kama watu wakipata dalili huhusiana na mambo ya mmengenyo kama kuharisha sana pia hupata dalili za kimsongo wa mawazo na mabadiliko ya tabia.

 

Dalili zingine ni kama

  1. Dalili za kujirudia za mvurugiko wa tumbo kama

  • Gesi

  • Maumivu ya tumbo, kusokota kwa tumbo na tumbo kuja

  • Chakula kukaa mda mrefu tumboni na kichefuchefu

  • Kuhara sana

  • Kinyesi kunuka kama kitu kilichooza

  • Kutoongezeka uzito kwa shida

  1. Upungufu wa damu kutokana na kutofyonzwa kwa madini chuma, folate na vitamin B12

  2. Kuchoka sana na mwili kuwa dhaifu

  3. Kiwango cha chini sana cha sukari kisichokuwa na sababu kwa watu wenye kisukari aina ya 1

  4. Kutokwa na vipele au harara zinazowasha sana

  5. Kutopata choo

  6. Kuhara au kutopata choo

  7. Kuchanika midomo

Dalili za ziada kwa watoto wadogo ni

  • Kuchelewa kukua

  • Kubadilika tabia na kuwa msumbufu

  • Kutapika

  • Kuchelewa kubalehe

  • Matatizoya meno na fizi

Utambuzi

Kipimo cha kuchukua kinyama kidogo kutoka kwenye kuta za utumbo huwa kipimo kitambuzi cha kepee

Matibabu

Bila matibabu, ugonjwa huu hupelekea upungufu wa lishe (utapiamlo), upungufu wa damu, mifupa isiyo imara, ugumba, na kwa watu wenye kisukari aina ya 1 hupata tatizo la kiwango cha chini cha damu.

Matibabu pekee ni kujiepusha na vyakula vyenye protini ya gluteni ambayo hupatikana kwenye ngano. Hivyo mtu anatakiwa kuepuka vitu vilivyotengenezwa kwa ngano kama mkate, maandazi n.k

Mtaalamu wa lishe atakusaidia kujua vyakula vvisivyo na protini ya gluten, au unaweza kuangalia katika mtandao wetu wa ULY-CLINIC.

Huzuniko

Dalili ya huzuniko huonekana kwa asimilia 30 kwa wagonjwa wenye kisukari, asilimia 10 kati ya hizi 30 hupata dalili kuu za huzuniko. Hali ya Huzuniko husababisha mtu kuwa dhaifu kiakili na kimwili na husababisha ugumu zaidi kwenye matibabu ya kisukari na kupelekea

  • Kushindwa kudhibiti sukari

  • Kutokea kwa matatizo mengine yanayodhuru afya ya mwili yanayoambatana na kisukari

  • Kupungua kwa ubora wa maisha ya mtu

  • Kuongezeka kwa matatizo ya kifamilia na kuongezeka kwa gharama za matibabu

 

Uhusiano kati ya huzuniko na kisukari haujaweza kufahamika vema. Huzuniko huweza kutokea kwa sababu ya msongo wa mawazo na hofu inayotokea mtu akiwa katika matibabu ya kisukari. Kwa mara nyingi ni vigumu kutambua mtu mwenye huzuniko na hivo ni vigumu kutibu pia. Ni kazi ya wataalamu wa afya kuweza kuwa na utaratibu maalumu wa kuwachunguza wagonjwa wa kisukari dhidi ya matatizo ya kisaikolojia ili kuweza kutambua endapo wana huzuniko na kuwapatia matibabu yanayotakiwa.

Matibabu

Kutibu huzuniko kunahusisha matibabu ya maongezi ya kisaikolojia, madawa au vyote viwili, matibabu haya huweza kuimarisha afya ya mtu na kuweza kudhibiti kisukari. Kwa watu wenye huzuniko na kisukari kwa pamoja,tafiti za wanasayansi zimeonyesha matibabu ya maongezi ya kisaikolojia na dawa dhidi ya huzuniko husaidia kuimarisha afya ya mtu na kudhibiti kupanda kwa kisukari. Dawa dhidi ya huzuniko hufanya kazi vema, na aina Fulani ya matibabu ya kisaikolojia husaidia kutibu huzuniko ingawa matibabu ya huzuniko huwa ya mtu mrefu. Madawa dhidi ya huzuniko huweza kutumia wiki kadhaa kupambana na huzuniko na huweza kuhitaji kuchanganya matibabu ya dawa na maongezi ya kisaikolojia. Pia miili hutofautiana katika kusikia dawa, hivyo mtu anaweza kuongezewa dozi, kupunguziwa au kubadilishiwa dawa na daktari ili kukabiliana na huzuniko.

Kwa matumizi ya dawa za asili kwa ajili ya kutibu huzuniko, lazima uombe ushauri wa daktari ili kujua kama yana mwingiliano na dawa zingine za kisukari. Matumizi ya dawa za asili yanaweza kufanya dawa za kisukari zisifanye kazi vema na huweza kuleta madhara ikiwemo kifo.

Wasiliana na daktari wako siku zote kwa ushauri na tiba kabla ya kuchukua hatu yoyote

Pata ushauri na tiba kutoka kwa daktari wa ULY clinic kwa kubonyeza hapa au piga namba za simu chini ya tovuti hii.

Imeboreshwa 12.03.2020

Rejea

Wasiwasi
Anchor 1
Celiac
Huzuniko
bottom of page