top of page

Mwandishi:

Mhariri:

ULY CLINIC

Dkt. Adolf S, M.D

26 Machi 2020 12:39:14

Dalili za ugonjwa wa ini
shahawa-zenye-damu-ulyclinic-compressor.

Dalili za ugonjwa wa ini

Ini ni ogani muhimu ndani ya mwili wa binadamu, hupatikana sehemu ya juu kulia ya tumbo. Ini pia huwa chini ya ukuta wa dayaframu, juu ya tumbo, figo ya kulia na utumbo. Kuna kazi nyingi zinazofanywa na Ini, baadhi ya kazi hizo zimeorodheshwa hapa chini.


Kazi ya Ini


 • Kulinda mwili dhidi ya magonjwa kwa kuondoa bakteria mwilini

 • Kuhifadhi Vitamini A, D,E,K & B12 na madini chuma

 • Kushughulika na chakula kilichosagwa kutoka kwenye utombo mdogo

 • Ini hutengeneza chembechembe zinazozuia damu kuganda mfano fibrinogen, prothrombin

 • Huharibu na kuondoa sumu na madawa ambayo yanaingia mwilini

 • Hutengeneza nyongo (bile ) ambayo husaidia kumeng'enya chakula

 • Kutengeneza vimeng’enya na protini ambazo zinahitajika mwilini kwenye shughuli nyingi ikiwa pamoja na kuponya tishu zilizoharibika au kuzeeka.

 • Kuvunjavunja chakula na kutengeneza nguvu inayohitajika mwilini( kuipa mwili nguvu)

 • Huhifadhi na kutoa sukari inayotoka kwenye chakula ili kutumiaka baadaye

 • Huvunjavunja kemikali ya hemoglobin

 • Hurekebisha hali ya damu

 • Huondoa bilirubini mwilini- kemikali ambayo inaleta manjano.


Aina za magonjwa ya Ini


Magonjwa ya ini yanaweza kuwa yafuatayo;


 • Magonjwa yanayosababishwa na virusi kama vile homa ya ini inayosababishwa na kirusi cha Hepataitis A,B na C

 • Magonjwa yanayosababishwa na sumu, dawa au pombe kama vile Ini mafuta na silosisi

 • Saratani ya ini

 • Magonjwa ya kurithi kama vile ugonjwa wa hemokromatosisi and ugonjwa wa Wilson


Visababishi vya Magonjwa Ya Ini


 • Vimelea- kama Virusi vya hepataitiz A, B na C . Kirusi cha hepataitiz B kinaongoza kwa kusababisha ugonjwa wa Ini

 • Magonjwa ya Autoimyuni

 • Unywaji wa pombe uliopindukia kwa muda mrefu

 • Ugonjwa wa ini mafuta

 • Magonjwa ya Kurithi mfano ugonjwa wa Wilson's

 • Madawa na sumu zinazoharibu na kudhuru Ini, mfano wa dawa ya parasetamo/panado


Dalili na Ishara za Ugonjwa Wa Ini


 • Maumivu ya tumbo

 • Kuvimba kwa tumbo- hii ni kutokana na asaitizi.

 • Anjano kwenye macho na ngozi, na mkojo

 • Kutoka damu kwenye fizi au puani bila sababu

 • Kupata kichefuchefu na Kutapika

 • Miguu kuvimba

 • Kupoteza hamu ya chakula na kupungua uzito

 • Kupumua kwa shida

 • Kuwashwa mwili kutokana na chumvi ya bile kujikusanya kwenye ngozi

 • Kupata kaputi medusa (kuonekana kwa mishipa ya damu kwenye tumbo yenye umbo la buibui inayoanzia kwenye kitovu)

 • Kuhisi kiu sana

 • Kuhisi Mapigo ya moyo yanaenda kwa kasi

 • Mwili kuchoka mara kwa mara

 • Kupata Kinyesi kilichopauka

 • Kupata mkojo mweusi

ULY CLINIC inakushauri siku zote uwasiliane na daktari wako kwa ushauri na tiba zaidi kabla ya kuchukua hatua yoyote ile ya kiafya baada ya kusoma makala hii.

Wasiliana na daktari wa ulyclinic kwa ushauri zaidi na tiba kwa kutumia namba za simu au kubonyeza link ya Pata Tiba chini ya tovuti hii

Imeboreshwa, 

19 Julai 2023 20:03:53

Soma dalili zingine Zaidi kwa kubonyeza herufi ya mwanzo hapa chini

[A] [B] [C] [D] [E] [F] [G] [H] [I] [J] [K] [L] [M] [N] [O] [P] [Q] [R] [S] [T] [U] [V] [W] [X] [Y] [Z] [Z] [#]

Rejea za mada

bottom of page