top of page

Dalili na viashiria vya magonjwa mbalimbali

ULY Clinic inakushauri kufuata ushauri wa daktari wako kabla ya kuchukua hatua yoyote ile baada ya kusoma makala. Bofya picha au neno soma zaidi ili kuingia kwenye makala kwa undani.

Kutokwa majimaji meupe bila maumivu uumeni

Kutokwa majimaji meupe bila maumivu uumeni

Kutokwa na majimaji meupe kutoka kwenye uume bila maumivu kunaweza kuwa dalili ya maambukizi ya zinaa kama chlamydia au urethritis isiyo ya kisonono. Uchunguzi wa kitaalamu na matibabu ya haraka ni muhimu ili kuepuka madhara zaidi.

Dalili za gono kwa mwanamke

Dalili za gono kwa mwanamke

Ni wanawake wachache (≈ 20–50 %) wanaopata gono huonyesha dalili, ambazo hujumuisha ute/usahu ukeni wenye harufu au rangi isiyo kawaida na maumivu wakati wa tendo la ndoa.  Gono hutibiwa kwa antibiotiki mseto; daima pata uchunguzi na ushauri wa daktari kabla ya kuanza tiba yoyote.

Maumivu katikati ya kifua

Maumivu katikati ya kifua

Maumivu katikati ya kifua yanaweza kuwa dalili ya tatizo dogo au la hatari kubwa. Ni muhimu kutosahau kuwa si kila maumivu ni kutokana na moyo kukosa oksijeni, lakini kutopuuza dalili ni hatua ya busara. Kupata uchunguzi sahihi mapema kunaweza kuokoa maisha.

Maumivu ya pumbu

Maumivu ya pumbu

Yanaweza kusababishwa na maambukizi, majeraha, au matatizo ya kiafya kama vile uvimbe wa mshipa wa pumbu. Uchunguzi wa haraka na matibabu sahihi ni muhimu ili kuepuka madhara ya muda mrefu.

Maumivu ya chembe ya moyo

Maumivu ya chembe ya moyo

Maumivu ya chembe ya moyo yanaweza kusababishwa na matatizo mbalimbali ya tumbo au via vingine ndani ya kifua, kama vidonda vya tumbo, au kucheua tindikali. Matibabu yanategemea chanzo cha maumivu na yanaweza kujumuisha dawa, mabadiliko ya mtindo wa maisha, na, wakati mwingine, upasuaji.

bottom of page