top of page

Dalili na viashiria vya magonjwa mbalimbali

Unashauriwa kufuata ushauri wa daktari wako kabla ya kuchukua hatua yoyote ile baada ya kusoma makala. Bofya picha au neno soma zaidi ili kuingia kwenye makala kwa undani.

Vipele vya muda mrefu Makalioni

Vipele vya muda mrefu Makalioni

Vipele vya muda mrefu makalioni vinaweza kutokana na maambukizi ya ngozi, msuguano, kuziba kwa vinyweleo au magonjwa sugu kama hidradenaitisi supurativa, hivyo si kila kipele ni jipu au fangasi. Vipele vinavyorudia kwa miaka, kutengeneza usaha, kuacha makovu au kutokea kwa mtu mwingine wa familia vinahitaji uchunguzi wa kitaalamu ili chanzo halisi kitambuliwe na kutibiwa ipasavyo.

Kuwashwa mrija wa Mkojo -Mwanaume: Sababu, Dalili, Uchunguzi na Matibabu

Kuwashwa mrija wa Mkojo -Mwanaume: Sababu, Dalili, Uchunguzi na Matibabu

Muwasho unaweza kutokana na sababu nyingi kuanzia maambukizi ya njia ya mkojo na magonjwa ya zinaa hadi muwasho wa mzio kwenye kemikali au matatizo mengine ya mfumo wa mkojo. Kutafuta chanzo kupitia uchunguzi sahihi husaidia kupata matibabu yanayofaa na kuzuia madhara ya muda mrefu.

Kikohozi Kisichokata

Kikohozi Kisichokata

Ni kikohozi kinachoendelea kwa muda mrefu kuliko kawaida na kinaweza kusababishwa na hali mbalimbali kama mafua, maambukizi ya virusi, pumu, mzio, kucheua tindikali, dawa fulani au maambukizi ya muda mrefu kama kifua kikuu. Kutambua chanzo chake ndiyo hatua muhimu ya kupata matibabu sahihi. Kikohozi kinachodumu, hasa kinachoambatana na dalili kama kupumua kwa shida, kukohoa damu, homa ya muda mrefu, kupungua uzito, maumivu ya kifua au kwa mjamzito na mtoto, kinahitaji tathmini ya mtaalamu wa afya.

Kupasuka kwa ngozi ya kichwa cha uume

Kupasuka kwa ngozi ya kichwa cha uume

Kupasuka kwa ngozi ya kichwa cha uume kunaweza kusababishwa na ukavu wa ngozi, msuguano, fangasi, mzio, kisukari, magonjwa ya ngozi au maambukizi ya zinaa, hivyo matibabu hutegemea chanzo halisi. Uchunguzi na matibabu ya mapema husaidia jeraha kupona vizuri, kuzuia kurudia kwa tatizo na kupunguza hatari ya madhara yanayoweza kutokea.

Kupasuka kwa viganja vya mikono

Kupasuka kwa viganja vya mikono

Husababishwa zaidi na ukavu wa ngozi, matumizi ya sabuni na kemikali kali, izima, fangasi, mzio na wakati mwingine magonjwa kama kisukari au matatizo ya tezi. Matibabu hutegemea chanzo na yanaweza kujumuisha kutumia vilainishi vya ngozi, kuepuka vitu vinavyokera, kutumia dawa maalumu za ngozi au kutibu ugonjwa wa msingi. Matibabu sahihi husaidia kuponya mipasuko na kuzuia kurudia kwa tatizo.

bottom of page