Dalili na viashiria vya magonjwa mbalimbali
Unashauriwa kufuata ushauri wa daktari wako kabla ya kuchukua hatua yoyote ile baada ya kusoma makala. Bofya picha au neno soma zaidi ili kuingia kwenye makala kwa undani.

Maumivu ya muda Mrefu ya Bega la Kulia na Mgongo wa Juu
Maumivu ya muda mrefu ya bega la kulia na mgongo wa juu yanaweza kutokana na matatizo ya misuli, kano, viungo, mishipa ya fahamu au hata viungo vya ndani kama nyongo, ini na mapafu. Ingawa sababu nyingi si za hatari, maumivu yanayodumu kwa muda mrefu, yanayozidi kuongezeka au yanayoambatana na dalili kama ganzi, udhaifu wa mkono, homa, kupumua kwa shida au kupungua uzito yanahitaji uchunguzi wa kitabibu mapema ili kubaini chanzo na kuanza matibabu sahihi.

Maumivu ya mbavu unapoamka asubuhi
Yanaweza kutokana na sababu za kawaida kama kukaza kwa misuli au kulala vibaya, lakini pia yanaweza kuwa ishara ya magonjwa yanayohusisha moyo, mapafu, ini, nyongo, figo au viungo vingine muhimu. Maumivu yanayojirudia, kuongezeka au kuambatana na dalili za hatari kama kupumua kwa shida, homa au kubanwa kifua yanapaswa kuchunguzwa mapema ili kupata matibabu sahihi na kuzuia madhara makubwa.

Maumivu ya tumbo baada ya kutoa mimba kwa upasuaji wa kusafisha kizazi
Mara nyingi ni sehemu ya kawaida ya mchakato wa kupona na hupungua hatua kwa hatua ndani ya siku hadi wiki chache. Hata hivyo, maumivu yanayozidi kuongezeka, yanayoambatana na homa, kutokwa na damu nyingi au uchafu wenye harufu mbaya yanahitaji uchunguzi wa haraka hospitalini ili kubaini na kutibu chanzo chake mapema.

