Mwandishi:
Mhariri:
Dkt. Sospeter B, M.D
Dkt. Salome A, M.D
19 Julai 2023, 12:17:54
Dalili za awali za uchungu
Kwa kawaida uchungu huanza wenyewe kwa mjamzito na dhumuni ni kutoa kiumbe nje ya mji wa mimba.
Kila mjamzito wakati huu huwa na dalili na ishara za kipekee ambapo inakuwa ngumu kutabili kwa kutumia uzoefu wa watu wengine.
Makala hii imeorodhesha dalili na viashiria kadhaa vya kuanza kwa uchungu wa kujifungua zinazotokea kwa wajawazito wengi licha ya zingine kutoweza kutambulika na wajawazito.
Kubana au kujongea kwa misuri
Huitwa uchungu wa uongo kwa sabababu huwa hauongezeki kwa jinsi muda unavyoenda na hautokei kwa mpangilio wa kueleweka. Mijongeo hii hupelekea mabadiliko kiasi ya urefu na upana wa shingo ya kizazi.
Kuzibuka kwa kifuniko cha shingo ya kizazi
Kutokwa na makamasi mengi ukeni yanayoweza kuwa ya rangi ya maji, pinki, au kuwa na michirizi yad amu. Dalili hii ni kiashiria cha kutoka kwa kifuniko cha shingo ya kizazi ambacho huzuia vimelea kutoka ukeni kuingia kwenye kizazi.Â
Makamasi yanaweza kutoka kwa dakika chache, masaa au siku kadhaa kabla ya uchungu kuanza. Dalili hii huwa haigunduliwi na wanawake wengi.
Maumivu ya mgongo
Maumivu mara nyingi huwa ya mgongo wa chini yaani katika maeneo ya kiuno, ambayo huwa endelevu na huwa makali ya kutovumilika kwenye hatua za mwisho za uchungu. Maumivu haya yanahusishwa kusababishwa na mgandamizo kwenye via na mishipa ya fahamu ya mfuko wa matumbo(peritoniamu) kutokana na unaoletwa na kukua kwa kizazi.
Hisia za za kujisaidia
Ni ishara ya mgandamizo kwenye matumbo na kibofu cha mkojo hivyo kupelekea hisia za kutaka kujisaidia. Hi pia humaanisha mtoto anajongea uelekeo wa kutoka nje ya kizazi kwa jina jingine mtoto kushuka. Mara nyingi hizia hizi huletwa na mgandamizo wa kichwa cha mtoto kwenye maeneo tajwa.
Kupasuka kwa chupa ya uzazi
Kati ya wanawake 10, mjamzito mmoja hupata dalili hii ambayo hutokea sana nyumbani wakati umelala. Baadhi ya nyakati chupa ya uzazi hupasuka kwenye uchungu na wakati mwingine hupasuliwa kwneye hatua ya pili ya uchungu.
Baadhi ya nyakahu huwa ni vigumu kutofautisha kati ya mkojo na maji ya chupa ya uzazi. Hata hivyo kupasuka kwa chupa ya uzazi huambatana na maji mengi yanayochuruzika kwenye mapaja kama mtu amesimama na huwa meupe, hayana harufu na hutoka mengi kwa ghafla au kuendelea kumwagika taratibu.
Kama ukipata dalili hii hakikisha kuwa si mkojo kwa kunusa, na kama ikionekana si mkojo unapaswa kuzingatia utoshiriki ngono au kutumia pedi ya kuchomeka ukeni au kufanya chochote kinachoweza kuingiza bakteria ukeni. Wakati huu onana na mtoa huduma ya afya.Â
Maji yakiwa na rangi tofauti na maji au harufu huweza kuashiria, maambukizi, au kuchanganyika na choo cha mtoto.
Ongezeko la nguvu
Wajawazito wengi huwa hupitia hali ya kupata usingizi zaidi, uchungu unapokaribia mwili huongezeka nguvu kiasi cha kuweza kujipangia kazi na kuzifanya bila kuhisi uchovu.
Mabadiliko ya urefu na upana wa shingo ya kizazi
Shingo ya kizazi huwa fupi na nyembamba. Hii ni ishara kwamba sehemu ya chini ya kizazi inajiandaa kwa ajili ya kutoa mtoto kwa kuwa shingo kuwa nyembamba hufanya iweze kutanuka kirahisi Zaidi. Dalili hii hupimwa na mtaalamu wa afya kwa kutia vidole viwili ukeni ili kuifikia shingo ya kizazi.
Ongezeko kipenyo cha shingo ya kizazi
Kuongezeka kwa kipenyo cha shingo ya kizazi ni dalili inayoashiria kufunguka kwa njia ya uzazi ili kichwa cha mtoto. Kizio cha kipimo hiki ni sentimita na kipenyo cha mwisho cha kutanuka ni sentimita 10. Dalili hii huwezi kuifahamu mwenyewe, mtaalamu wa afya hupima shingo ya kizazi kupitia uke kutumia vidole viwili kila baada ya masaa 2 hadi 4 ikitegemea hatua ya uchungu uliyonayo. Hatua za awali za uchungu huweza kuchukua muda kabla ya kwenda kuwa uchungu wa kujifungua
Majina mengine
Makala hii pia imetoa maelezo na inafahamika pia kama:
Dalili za awali za uchungu
Dalili za kuanza kwa uchungu
Dalili za awali za leba
Dalili za kujifungua
Ishala za awali za uchungu
Ishara za awali za leba
Ishara za kuanza kwa uchungu
Ishala ya kujifungua
Dalili za uchungu wiki ya 37
Dalili za uchungu wiki ya 38
Dalili za uchungu wiki ya 39 na 40
ULY CLINIC inakushauri siku zote uwasiliane na daktari wako kwa ushauri na tiba zaidi kabla ya kuchukua hatua yoyote ile ya kiafya baada ya kusoma makala hii.
Wasiliana na daktari wa ulyclinic kwa ushauri zaidi na tiba kwa kutumia namba za simu au kubonyeza link ya Pata Tiba chini ya tovuti hii
Imeboreshwa,
19 Julai 2023, 12:17:54
Soma dalili zingine Zaidi kwa kubonyeza herufi ya mwanzo hapa chini
​
[A] [B] [C] [D] [E] [F] [G] [H] [I] [J] [K] [L] [M] [N] [O] [P] [Q] [R] [S] [T] [U] [V] [W] [X] [Y] [Z] [Z] [#]
Rejea za mada
1. Hutchison J, et al. Stages of Labor. 2023 Jan 30. In: StatPearls [Internet]. Treasure Island (FL): StatPearls Publishing; 2023 Jan–. PMID: 31335010.
2. Melzack R, et al. Low-back pain during labor. Am J Obstet Gynecol. 1987 Apr;156(4):901-5. doi: 10.1016/0002-9378(87)90349-8. PMID: 2953242.
3. Signs and Symptoms of Labor. https://americanpregnancy.org/healthy-pregnancy/labor-and-birth/signs-of-labor/. Imechukuliwa 18.07.2023
4. William’s Obstetrics Twenty-Second Ed. Cunningham, F. Gary, et al, Ch. 17.
5. NHS. Pregnancy signs. https://www.nhs.uk/pregnancy/labour-and-birth/signs-of-labour/signs-that-labour-has-begun/. Imechukuliwa 18.07.2023
6. Cleveland clinic. 8 Signs That Labor Is 24 to 48 Hours Away. https://www.google.com/search?q=labor+symptoms&client. Imechukuliwa 18.07.2023
7. NCBI. Stages of labor. https://www.ncbi.nlm.nih.gov/books/NBK544290/#:. Imechukuliwa 18.07.2023