Mwandishi:
Dkt. Mwercy M, CO
Mhariri:
Dkt. Benjamin L, MD

Ambrisentan ni dawa kundi la dawa pinzani kwenye risepta endothelin inayotumika kutibu shinikizo la juu la damu kwenye arteri za mapafu
Majina ya kibiashara ya Ambrisentan
Letairis
Ambrisentan ipo kundi gani la dawa?
Ambrisentan ni dawa iliyo katika kundi la Endothelin Antagonists.
Dawa zilizo kundi moja na Ambrisentan
Dawa zilizo kundi moja na Ambrisentan ni ;
Bosentan
Macitentan
Fomu na uzito Ambrisentan
Dawa hii ipo katika fomu ya kidonge chenye uzito wa 5mg na 10mg
Ambrisentan hutibu nini?
Hutumika kutibu shinikizo la juu la damu kwenye mapafu ( mishipa ya arteri ya mapafu)
Namna Ambrisentan inavyofanya kazi
Endothelin-1 (ET-1) ni peptide asili kwenye endothelin aina A (ETA) na aina B (ETB) kwenye risepta za misuli laini ya damu na ukuta uliyofunika ndani ya mishipa ya damu (endothelium). ETA- hufanya kazi ya kutanua mishipa ya damu na utoaji nakala wa chembe, wakati ETB hufanya kazi kuu ya kutanua mishipa ya damu na utoaji wa ET-1. KWa mgonjwa mwenye shinikizo la damu kwenye mishipa ya ateri kweney mapafu, kiwango cha risepta ET-1 huongezeka kiasi cha kuendana na kiwango cha shinikizo la damu kwenye arteri za mapau. Dawa ambrisentan ni moja ya dawa zilizogunduliwa hivi karibuni zenye uwezo wa kutanua kipenyo cha mishipa ya damu ya mapafu kwa kufanya kazi kwenye ripepta ETA. Hufanya kazi kwa kuzuia ufanyaji kazi wa risepta hii kwa kuifanya ishindwe kusinyaza mishipa ya damu ya mapafu. Dawa hii huwa haizuii utendaji kazi wa risepta ETB, nitric oxide na uzalishaji wa prostacyclin, utanuaji wa mishipa kunakoamshwa na cyclic GMP- na cyclic AMP na utoaji wa endothelin-1 (ET-1) mwilini.
Ufozwaji wa dawa
Kiwango cha dawa kinachopatikana kwenye damu huonekana ndani ya masaa mawili baada ya kumeza dawa.
Mwingiliano wa Ambrisentan na chakula
Dawa hii inaweza kutumika mtu akiwa amepata chakula au akiwa hajapata chakula.
Utoaji taka wa Ambrisentan mwilini
Predominantly non-renal.
Wagonjwa wasiopaswa kutumia Ambrisentan
Wagonjwa wenye mzio wa Ambrisentan.
Wagonjwa wenye mzio wa dawa jamii ya Endothelin antagonists.
Dawa zenye muingiliano na Ambrisentan
Dawa zenye mwingiliano mkali na hivyo kutofaa kutumika pamoja na Ambrisentan;
Apalutamide
Cyclosporine
Idelalisib
Lasmiditan
Lonafarnib
Sotorasib
Tepotinib
Dawa zinazoweza kutumika na Ambrisentan chini ya uangalizi;
Berotralstat
Cannabidiol
Cenobamate
Conjugated estrogens
Conjugated estrogens, a kuweka ukeni
Crofelemer
Eslicarbazepine acetate
Etonogestrel
Fedratinib
Fexinidazole
Fostamatinib
Fostemsavir
Iloperidone
Istradefylline
Ivacaftor
Letermovir
Lumacaftor/ivacaftor
Mitotane
Ponatinib
Rifampin
Rucaparib
Sarecycline
Sofosbuvir/velpatasvir
Stiripentol
Tecovirimat
Triclabendazole
Tucatinib
Dawa zenye mwingiliano mdogo na Ambrisentan;
Amiodarone
Atazanavir
Bosentan
Carbamazepine
Clarithromycin
Dexamethasone
Dronedarone
Efavirenz
Erythromycin base
Erythromycin ethylsuccinate
Erythromycin lactobionate
Erythromycin stearate
Esomeprazole
Fluconazole
Fosphenytoin
Indinavir
Isoniazid
Itraconazole
Ketoconazole
Modafinil
Nefazodone
Nelfinavir
Nevirapine
Nicardipine
Omeprazole
Pentobarbital
Phenobarbital
Phenytoin
Posaconazole
Primidone
Quinidine
Ranolazine
Ribociclib
Rifabutin
Rifapentine
Shepherd's purse
Simvastatin
St john's wort
Tolvaptan
Verapamil
Voclosporin
Matumizi ya Ambrisentan kwa mama mjamzito
Tafiti zinaonesha kuwa dawa hii ina madhara kwa mama mjamzito na kwa mtoto aliyepo tumboni hivyo hairuhusiwi kutumika wakati wa ujauzito.
Matumizi ya Ambrisentan mama anayenyonyesha
Hakuna tafiti zinazoonesha madhara ya dawa hii kwa mama anayenyonyesha, kwa mtoto na katika uzalishwaji wa maziwa hivyo kimoja wapo kati ya mtoto kunyonya na mama kutumia dawa inatakiwa viangaliwe kulingana na uhitaji .
Maudhi ya Ambrisentan
Maumivu ya tumbo
Kichefuchefu
Maumivu ya kichwa
Mwili kuvimba
Kuziba kwa pua
Kushindwa kupumua vizuri
Kichefuchefu
Kutokwa na jasho
Sinusaitiz
Homa
Kutapika
Kupungukiwa damu
Moyo kushindwa kufanya kazi vizuri
Kizunguzungu
Ini kushindwa kufanya kazi vizuri
Mzio
Mwili kuchoka
Ufanye nini kama kutumia dozi yako?
Ukisahau kutumia dozi yako tumia mara pale utakapokumbuka, kama muda wa dozi inayofata umekaribia usimeze dozi uliyosahau endelea na dozi inayofuata kwa muda uliopangiwa na daktari. Usimeze dozi mbili kufidia uliyosahau.
17 Januari 2026, 15:31:06
Dawa Ambrisentan
Imeboreshwa,
6 Oktoba 2021, 05:00:37
Dawa yoyote ni sumu, usitumie dawa pasipo ushauri wa daktari kuepuka madhara kwenye ogani mbalimbali kama figo na ini. Matumizi ya dawa pasipo ushauri wa daktari unaweza kusababisha madhara na usugu wa vimelea vya maradhi kwenye dawa.
ULY CLINIC inakushauri siku zote uwasiliane na daktari wako kwa ushauri na tiba kabla ya kuchukua hatua yoyote ile baad aya kusoma makala hii.
Kupata ushauri zaidi na tiba kutoka kwa daktari wa ULY CLINIC bofya Mawasiliano yetu au Pata tiba.
Rejea za mada hii:
Brunton LL, Hilal-Dandan R, Knollmann BC. Goodman & Gilman's: The Pharmacological Basis of Therapeutics. 14th ed. New York: McGraw-Hill; 2023. Antihypertensive agents.
Sweetman SC, editor. Martindale: The Complete Drug Reference. 40th ed. London: Pharmaceutical Press; 2020. Methyldopa.
McEvoy GK, editor. AHFS Drug Information 2024. Bethesda (MD): ASHP; 2024. Methyldopa.
World Health Organization. WHO recommendations for prevention and treatment of pre-eclampsia and eclampsia. Geneva: WHO; 2023.
Drugs.com. Methyldopa [Internet]. 2024 [cited 2025 Jun 5].
Micromedex (IBM Watson). Methyldopa Drug Monograph. 2024.
