top of page

Mwandishi:

Dkt. Mercy M, CO

Mhariri:

Dkt. Sospeter B, MD

kirusi mumps-ulyclinic

Clobazam ni dawa jamii ya benzodiazepam inayotumika kama adijuvanti katika matibabu ya degedege la sindromu ya Lennox-Gastaut


Majina ya kibiashara


Majina mengine ya kibiashara ya Clobazam ni;

  • Onfi

  • Sympazan


Clobazam ipo kundi gani la dawa?


Clobazam ni dawa iliyo katika kundi la


  • Dawa za degedede

  • Dawa jamii ya benzodiazepine.


Dawa zilizo kundi moja na Clobazam


Dawa zilizo kundi moja na Clobazam ni;


  • Alparazolam

  • Chlordiazepoxide

  • Diazepam

  • Clobazam

  • Clonazepam

  • Clorazepate

  • Estazolam

  • Flurazepam

  • Lorazepam

  • Midazolam

  • Oxazepam

  • Temazepam

  • Triazolam


Fomu ya dawa


Dawa hii ipo katika fomu ya;


  • Kidonge

  • Kimiminika cha kunywa

  • Kimiminika kisicho


Uzito wa dawa


Clobazam ina uzito ufuatao;


Kidonge

  • 10mg

  • 20mg


Suspesheni kwa ajiri ya kunywa

2.5mg/ml


Kimiminika kilichochanganyika na maji

  • 5mg

  • 10mg

  • 20mg



Clobazam hutibu nini?


Hutibu degedege.


Namna Clobazam inavyoweza kufanya kazi


Clobazam hujishikiza kwenye sehemu maalumu inapojishikiza chloride ionopore kwenye risepta GABA. Risepta GABA hupatikana sehemu mbalimbali za mfumo wa kati wa fahamu. Kujishikiza katika risepta hii husababisha kuendelea kuwa wazi kwa mlango chloride ionopore na matokeo yake ni kupungua kwa mwitikio wa chembe hai.


Ufyozwaji wa dawa


Mara baada ya kunywa, kiasi cha clobazam, kinachoingia kwenye damu hufikia hadi asilimia 87 ya dozi iliyotumika. Kama kimiminika kikitumika ufyonzwaji wake hufiki hadi asilimia 100 ndani ya saa 1 hadi 3


Mwingiliano wa Clobazam na chakula.


Dawa hii inaweza kutumika pamoja au bila chakula. Hakuna mwingiliano wa dawa hii na chakula ulioripotiwa.


Mwingiliano na pombe


Clobazam haipaswi kutumia na pombe. Pombe huongeza ufyonzwaji wa dawa hii kwa asilimia 50 zaidi na hivyo kama itatumika pamoja kuna ongezeko la dalili za kineva kama vile kizunguzungu, usingizi mkali, kushindwa kutafakari na kupungua uwezo wa kufanya maamuzi.


Wagonjwa wasiopaswa kutumia Clobazam


  • Wagonjwa wenye mzio wa Clobazam

  • Wagonjwa wenye mzio wa dawa jamii ya Benzodiazepine



Utoaji taka wa Clobazam mwilini


Asilimia themanini na mbili (82%) ya dawa hutolewa kwa njia ya mkojo kama mazao ya umetaboli na asilimia kumi na moja (11%) hutolewa kupitia kinyesi. Chini ya asilimia 2 ya dawa hutolewa kwa njia ya mkojo bila kufanyiwa umetaboli.


Matumizi ya Clobazam kwa mama mjamzito


Hakuna tafiti zinazoonesha madhara ya dawa hii kwa mama mjamzito na kwa mtoto aliyeko tumboni hivyo tahadhari inatakiwa wakati mama anatumia dawa hii.



Matumizi ya Clobazam kwa mama anayenyonyesha


Tafiti zinaonesha kuwa dawa hii inatolewa kwenye maziwa ya mama lakini haijaonesha madhara kwa mtoto hivyo kimoja wapo kinatakiwa kizingatiwe kati ya mama kutumia dawa au mtoto kunyonya.


Dawa zenye muingiliano na Clobazam



Dawa zenye mwingiliano mkali na hivyo kutofaa kutumika pamoja na Clobazam;

  • Apalutamide

  • Avapritinib

  • Axitinib

  • Cabozantinib

  • Deflazacort

  • Elbasvir/grazoprevir

  • Entrectinib

  • Fedratinib

  • Finerenone

  • Infigratinib

  • Irinotecan

  • Irinotecan liposomal

  • Ivabradine

  • Lefamulin

  • Lemborexant

  • Lonafarnib

  • Lorlatinib

  • Lurbinectedin

  • Metoclopramide intranasal

  • Mobocertinib

  • Neratinib

  • Pemigatinib

  • Pretomanid

  • Rimegepant

  • Selinexor

  • Selumetinib

  • Siponimod

  • Sofosbuvir/velpatasvir

  • Sonidegib

  • Tazemetostat

  • Venetoclax

  • Voclosporin

  • Voxelotor

  • Zanubrutinib


Dawa zinazoweza kutumika na Clobazam chini ya uangalizi;

  • Alfentanil

  • Alprazolam

  • Amitriptyline

  • Amobarbital

  • Amoxapine

  • Carbamazepine

  • Carbinoxamine

  • Carisoprodol

  • Carvedilol

  • Cenobamate

  • Cetirizine

  • Chloral hydrate

  • Chlordiazepoxide

  • Chloroquine

  • Chlorpheniramine

  • Chlorpromazine

  • Chlorzoxazone

  • Clemastine

  • Clomipramine

  • Diazepam

  • Esomeprazole

  • Ethanol

  • Fluconazole

  • Gabapentin

  • Isoniazid

  • Ketoconazole

  • Lansoprazole

  • Miconazole oral

  • Morphine

  • Omeprazole

  • Pentobarbital

  • Pregabalin

  • Promethazine

  • Rabeprazole

  • Tinidazole

  • Tizanidine

  • Trimipramine

  • Zaleplol


Dawa zenye mwingiliano mdogo Clobazam;

  • Pantoprazole

  • Perampanel


Maudhi madogo ya Clobazam


  • Huzuniko na ukaputi

  • Huzuni

  • Kupanda kwa joto la mwili

  • Maambukizi mfumo wa juu wa upumuaji

  • Uchovu

  • Kutokwa na udenda

  • Kuwa na hasira

  • Kulialia kwa mtoto

  • Kutapika

  • Kukosa usingizi

  • Kukosa uwiano wa mwili wakati wa kujongea

  • Haja ngumu

  • Uchovu wa mwili

  • Kikohozi

  • Kuongezeka kwamijongeo ya kisaikomota

  • Nimonia

  • Maambukizi ya njia ya mkojo

  • Kushindwa tamka maneno

  • Kukosa hamu ya kula

  • Kuongezeka kwa hamu ya kula

  • Bronkaitiz

  • Maumivu wakati wa kumeza chakula


Maudhi mengine baada ya dawa kuingia sokono

  • Kushuka kwa joto la mwili

  • Upungufu wa damu

  • Eosinofilia

  • Leukopenia

  • Thrombosaitopenia

  • Diplopia

  • Uono hafifu

  • Kujaa kwa tumbo

  • Kubakisha mkojo kwenye kibofu

  • Ongezeko la vimen’enya vya ini

  • Misuli kubana


Ufanye nini kama umesahau kutumia dozi yako?


Kama umesahau kutumia dozi yako tumia mara pale utakapokumbuka, kama muda wa dozi inayofata umekaribia usimeze dozi uliyosahau endelea na dozi inayofuata kwa muda uliopangiwa na daktari. Usimeze dozi mbili kufidia uliyosahau.

17 Januari 2026, 15:31:06

Dawa Clobazam

Imeboreshwa,

6 Oktoba 2021, 05:02:33

Dawa yoyote ni sumu, usitumie dawa pasipo ushauri wa daktari kuepuka madhara kwenye ogani mbalimbali kama figo na ini. Matumizi ya dawa pasipo ushauri wa daktari unaweza kusababisha madhara na usugu wa vimelea vya maradhi kwenye dawa.

ULY CLINIC inakushauri siku zote uwasiliane na daktari wako kwa ushauri na tiba kabla ya kuchukua hatua yoyote ile baad aya kusoma makala hii.

Kupata ushauri zaidi na tiba kutoka kwa daktari wa ULY CLINIC bofya Mawasiliano yetu au Pata tiba.

Rejea za mada hii:

  1. Brunton LL, Hilal-Dandan R, Knollmann BC. Goodman & Gilman's: The Pharmacological Basis of Therapeutics. 14th ed. New York: McGraw-Hill; 2023. Antihypertensive agents.

  2. Sweetman SC, editor. Martindale: The Complete Drug Reference. 40th ed. London: Pharmaceutical Press; 2020. Methyldopa.

  3. McEvoy GK, editor. AHFS Drug Information 2024. Bethesda (MD): ASHP; 2024. Methyldopa.

  4. World Health Organization. WHO recommendations for prevention and treatment of pre-eclampsia and eclampsia. Geneva: WHO; 2023.

  5. Drugs.com. Methyldopa [Internet]. 2024 [cited 2025 Jun 5].

  6. Micromedex (IBM Watson). Methyldopa Drug Monograph. 2024.

bottom of page