top of page

Mwandishi:

Dkt. Mangwella S, M.D

Mhariri:

Dkt. Charles W, M.D

kirusi mumps-ulyclinic

Zinc ni dawa inayoimarisha mfumo wa kinga ya mwili ili upambane na maradhi ya bakteria na virusi, huponya vidonda kwenye utumbo, huimarisha hisia za kunusa na ladha ya chakula na pia huhusika katika utengenezaji wa protini na DNA mwilini. Zinc hupatikana katika fomu tofauti, na ikiwa imechanyanywa na vitamin kama Pedizinc C ambayo huwa a vitamin C.


Majina ya kibiashara ya zinc

Zinc hufahamika kwa majina ya kibiashara kama;

  • Galzin

  • Pedzinc

  • ZnCl2

  • Anodan-HC

  • Anusol

  • Egozinc

  • Multitrace-4

  • Multitrace-5

  • Proctodan-HC

  • Rectogel

  • Riva-sol HC


Majina mengine ambayo si ya kibishara

Jina jingine la zinc hupatikana kama Pedzinki. Pedzinc hutumika sana kwa watoto.

Dawa zilizo kundi moja na zinc

  • Chromium

  • Chromium 3

  • Chromium picolinate

  • Copper

  • Galzin

  • Glucose tolerance factor

  • Iodine

  • Manganese

  • Mncl2

  • Molybdenum

  • Molypen

  • Selenious acid

  • Selenium

  • Selepen

  • Trace elements

  • Tralement

  • Trivalent chromium


Fomu na uzito wa zinc

Hupatikana katika fomu ya

  • Tembe (zinc gluconate) yenye uzito wa 50 mg

  • Tembe (zinc acetate) yenye uzito wa 25 mg, 50 mg

Kidonge (zinc gluconate) chenye uzito wa;
  • 10mg

  • 15 mg

  • 30 mg

  • 50 mg

  • 100 mg


Kimiminika (zinc sulfate) cha kuchoma kwenye mishipa chenye uzito wa;
  • 1 mg/ml

  • 5 mg/ml


Kimiminika (zinc chloride) cha kuchoma kwenye mishipa chenye uzito wa;
  • 1 mg/ml


Zinc hutibu nini?

Zinc hutumika katika matibabu ya;

  • Homa ya baridi ( kutokana na maambukizi ya mafua)

  • Ugonjwa wa Wilson's

  • Kuzuia upungufu wa zinc kwa watoto na watu wazima wanaoharisha

  • Kutibu upungufu wa zinc kwa watoto na watu wazima wanaoharisha

  • Hutumika kutibu upungufu wa zinc kwa wagonjwa wanaolishwa kwa njia ya mishipa


Namna zinc inavyoweza kufanya kazi

Zinc huzuia milango ya utumbo ileum isiruhusu maji kutolewa ndani ya mwili kuingia kwenye utumbo, hufanya kazi hii kwa kufunga njia za potassium. Zinc pia huimarisha ufyozwaji wa maji na madini, huimarisha uumbaji upya wa chembe za ukuta wa utumbo zilizoharibiwa, huongeza vimeng’enya kwenye mipaka ya kuta za utumbo, huimarisha mwitikio wa mfumo wa kinga kwenye maradhi na kufanya vimelea walio tumboni wadhibitiwe vema.


Ufozwaji wa dawa

Wastani wa asilimia 20 hadi 30 ya zinc kwenye chakula hufyonzwa na kuingia kwenye damu haswa kwenye duodenum na ileum. Kiasi cha ufyonzwaji wa zinc hutegemea kiasi cha zinc kilichomo kwenye chakula. Zinc hupatikana sana kwenye nyama nyekundu na samaki jamii ya oyster. Phytates huathiri ufyonzwaji wa zinc. Baada ya kufyonzwa, zinc hujishikiza kwenye metallothionein iliyo kwenye utumbo mpana.


Mwingiliano wa zinc na chakula

Usitumie maziwa au vyakula vinavyotokana na maziwa angalau masaa mawili kabla ya kunywa dawa. Mara baada ya kutumia dawa, usile ndani ya masaa 2 baada ya kutumia dawa. Usile pamoja na vyakula vyenye nyuzinyuzi kwa wingi. Ili kuongeza ufyonzwaji wake kunywa kabla au baada ya masaa mawili toka umekula chakula chenye nyuzinyuzi kwa wingi.

Tumia dawa hii bila chakula. Tumia angalau saa 1 kabla ya kula au masaa 2 baada ya kula ili ifyonzwe vema. Unaweza kutumia zinc na chakula kama unataka kupunguza maudhi ya tumbo.


Utoaji taka za zinc mwilini

Asilimia 90 ya dawa hutolewa awali kwa njiaya kinyesi na kiasi kidogo kwa njia ya mkojo na pumzi.


Wagonjwa wasiopaswa kutumia zinc

Wagonjwa wenye mzio wa zinc au viungo villivyo ndani yake (sulphate n.k)


Dawa zenye muingiliano na zinc


Dawa zinazoongeza kiwango cha zinc kwenye damu
  • Amiloride (Midamor)

  • Cisplatin (Platinol-AQ)

  • Deferoxamine (Desferal)

  • Penicillamine


Dawa zinazopunguza kiwango cha zinc kwenye damu
  • Captopril (Capoten)

  • Benazepril (Lotensin)

  • Enalapril (Vasotec)

  • Lisinopril (Zestril)

  • Fosinopril (Monopril)

  • Ramipril (Altace)

  • Perindopril (Aceon)

  • Quinapril (Accupril)

  • Moexipril (Univasc)

  • Trandolapril (Mavik)


Dawa zinazopunguzwa ufyonzwaji wake zikitumika na zinc
  • Ciprofloxacin (Cipro)

  • Levofloxacin (Levaquin)

  • Ofloxacin (Floxin)

  • Moxifloxacin (Avelox)

  • Norfloxacin (Noroxin)

  • Gatifloxacin (Tequin)

  • Tetracycline

  • Minocycline (Minocin)

  • Demeclocycline (Declomycin)

  • Ibuprofen (Advil, Motrin)

  • Naprosyn (Aleve)

  • Piroxicam (Feldene)

  • Indomethacin (Indocin


Dawa zinazopingana ufanyaji kazi na zinc
  • Prednisone

  • Cyclosporine


Matumizi ya zinc kwa mama mjamzito

Tafiti zinaonyesha kuwa dawa hii haina madhara kwa wajawazito na inaweza kutumika kwa wanawake.


Matumizi ya zinc kwa mama mjamzito

Dawa hii huingia kwenye maziwa ya mama hivyo inapaswa kutumika kwa unagalifu.


Maudhi ya zinc

  • Kichefuchefu

  • Kutapika

  • Uchokozi wa tumbo

  • Ongezeko la vimeng’enya kama alkaline phosphatase, amylase, na lipase vitakavyorejea kwenye hali ya kawaida ndani ya mwaka 1 hadi 2 ya matibabu

  • Madhaifu ya mfumo wa fahamu

Kama ukipata dalili zifuatazo wasiliana na daktari haraka

  • Homa

  • Kutetemeka

  • Koo kuwa chungu

  • Vidonda mdomoni

  • Uchovu mkali

  • Kupooza kwa mwili


Ufanye nini ufanye kama umesahau kutumia dozi yako?

Ni muhimu sana kutumia dozi uliyoandikiwa kwa wakati sahihi. Kama umesahau kutumia kwa wakati sahihi tumia mara pale utakapokumbuka. Kama muda wa dozi inayofuata umekaribia sana, subiria muda huo ufike kisha endelea na dozi kama ulivyopangiwa. Usitumie dozi mbili kwa wakati mmoja.

13 Juni 2023 19:18:46

Dawa zinc

Imeboreshwa,

10 Julai 2023 09:13:06

Dawa yoyote ni sumu, usitumie dawa pasipo ushauri wa daktari kuepuka madhara kwenye ogani mbalimbali kama figo na ini. Matumizi ya dawa pasipo ushauri wa daktari unaweza kusababisha madhara na usugu wa vimelea vya maradhi kwenye dawa.

​

ULY CLINIC inakushauri siku zote uwasiliane na daktari wako kwa ushauri na tiba kabla ya kuchukua hatua yoyote ile baad aya kusoma makala hii.

Kupata ushauri zaidi na tiba kutoka kwa daktari wa ULY CLINIC bofya Mawasiliano yetu au Pata tiba.

Rejea za mada hii:

  1. Bäck SE, et al. Age dependence of renal function: clearance of iohexol and p-amino hippurate in healthy males. Scand J Clin Lab Invest. 1989 Nov;49(7):641–646.

  2. Bax RP, et al. The pharmacokinetics of meropenem in volunteers. J Antimicrob Chemother. 1989 Sep;24 (Suppl A):311–320.

  3. Burman LA, et al. Pharmacokinetics of meropenem and its metabolite ICI 213,689 in healthy subjects with known renal metabolism of imipenem. J Antimicrob Chemother. 1991 Feb;27(2):219–224.

  4. Christensson BA, et al. Pharmacokinetics of meropenem in subjects with various degrees of renal impairment. Antimicrob Agents Chemother. 1992 Jul;36(7):1532–1537. 

  5. DAVIES DF, SHOCK NW. Age changes in glomerular filtration rate, effective renal plasma flow, and tubular excretory capacity in adult males. J Clin Invest. 1950 May;29(5):496–507.

  6. Douglas JG, et al. The pharmacokinetics of cefuroxime in the elderly. J Antimicrob Chemother. 1980 Jul;6(4):543–549.

  7. Granerus G, et al. Reference values for 51Cr-EDTA clearance as a measure of glomerular filtration rate. Scand J Clin Lab Invest. 1981 Oct;41(6):611–616.

  8. Harrison MP, et al. The disposition and metabolism of meropenem in laboratory animals and man. J Antimicrob Chemother. 1989 Sep;24 (Suppl A):265–277. 

  9. Jones RN, et al. In-vitro studies of meropenem. J Antimicrob Chemother. 1989 Sep;24 (Suppl A):9–29. 

  10. Krutzén E, et al. Plasma clearance of a new contrast agent, iohexol: a method for the assessment of glomerular filtration rate. J Lab Clin Med. 1984 Dec;104(6):955–961.

  11. Ljungberg B, et al. Pharmacokinetics of antimicrobial agents in the elderly. Rev Infect Dis. 1987 Mar-Apr;9(2):250–264.

bottom of page