Mwandishi:
Dkt. Benjamin L, MD
Mhariri:
Dkt. Adolf S, MD
Chanjo ya kuzuia maambukizi ya HPV
7 Juni 2021 19:18:25
Virusi vya HPV wapo aina nyingi sana duniani na wengi wanaweza kusababisha magonjwa kwa binadamu saratani ya shingo ya kizazi, saratani ya koo na dutu sehemu mbalimbali za mwili.
Kupata chango ya virusi vya HPV haswa kwa wanawake ni njia mojawapo ya kupunguza kupata saratani ya shingo ya kizazi.
Chanjo ya kuzuia maambukizi ya HPV
Chanjo ya Cervarix (HPV Bivalent)
Gardasil (HPV Quadrivalent)
Gardasil 9 (HPV Nonavalent)
Recombinant (HPV) Bivalent Vaccine
Recombinant (HPV) Nonavalent Vaccine
Recombinant (HPV) Quadrivalent Vaccine
Kina nani wanapata chanjo ya HPV
Chanjo ya HPV kwa vile haitibu maambukizi yaliyopo, inashauriwa kutolewa kwenye makundi ya waru ambao bado hawajaanza kushiriki ngono.
Kama moja ya mpango wa kutoa chanjo kwa kila mtu, chanjo hii inashauriwa sana kuanza kutumia katika umri wa miaka 11 au 12 mpaka kufikia umri wa miaka 26, haa hivyo inaweza kutolewa umri kuanzia miaka 9.
Kutoa chanjo katika umri wa miaka zaidi ya 26 hadi 45 haina faida haswa kwatu ambao tayari walishawahi kujamiana na wana maambukizi tayari ya kirusi cha HPV
Chanjo inakinga aina gani ya virusi vya HPV?
Kila chanjo inakinga aina fulani ya kirusi kama ilivyoelezewa hapa;
Gardasil – inakinga dhidi ya kirusi cha HPV 6, 11, 16 na 18
Cervarix – inakinga dhidi ya kirusi cha HPV 16 na 18
Gardasil 9 – inakinga dhidi ya kirusi cha HPV 6, 11, 16, 18, 31, 33, 45, 52 na 58
Virusi wanaoathiri binadamu na kusababisha saratani ni wapi?
Kirusi cha HPV 16 na 18 husababisha saratani ya shingo ya kizazi
Kirusi cha HPV 6, na 11 husabaisha dutu sehemu za siri
Kirusi cha HPV 16, 18, 31, 32, 38 husababisha ugonjwa wa bowen
Kirusi cha HPV 5, 8, 9, 12, 14, 15, 17, 19-25, 36-38, 46, 47, 49 na 50 husababisha ugonjwa wa epidermodysplasia verruciformis
Kirusi cha HPV 16, 18, 31, 33, 35, 39, 45, 51, 52, 56, 58, 59, 66, 68, 73, 82 husababisha saratani kwenye ngozi laini kama koo, uke n.k
Kirusi HPV 5,8,9,15,20,24,36, na 38.Husababisha saratani ya ngozi isiyo ya melanoma
Wapi utapata taarifa zaidi kuhusu chanjoa ya HPV?
Kupata taarifa zaidi ingia kwenye kurasa za CDC na WHO kupitia linki hapa chin zilizo kwenye rejea za makala hii hapo chini.