Mwandishi:
Dkt. Benjamin L, MD
Mhariri:
Dkt. Adolf S, MD
Dawa ya kutibu maambukizi ya chlamydia
7 Juni 2021 15:11:42
Dawa za kutibu maambukizi ya chlamydia hutumika kama mchanganyiko wa dawa zaidi ya moja. Ili kufahamu mchanganyiko unaokufaa ni vema ukawasiliana na daktari wako. Kumbuka pia kwa sababu pangusa ni ugonjwa wa zinaa, zinapaswa kutumia na mtu na mpenzi wake anayeshiriki naye ngono.
Endapo una wapenzi wengi, wote wanabidi kutumia dawa hizo au kuacha kushiriki nao ngono kwa sababu ya kuepuka maambukizi mapya.
Orodha ya dawa za kutibu Maambukizi ya Chlamydia
Dawa za (chlamydia) zinajumuisha;
Azithromycin
Doxycycline
Levofloxacin
Ofloxacin
Amoxicillin
Doxycycline
Majina mengine ya dawa za kutibu maambukizi ya chlamydia ni yapi?
Baadhi ya watu hutumia majina yafuatayo ambayo humaanisha maambukizi ya chlamydia au magonjwa mengine ya zinaa;
Dawa za uchafu wa njano ukeni
Dawa ya kukata uchafu wa njano na unaonuka ukeni
Dawa za kutokwa na majimaji ya njano ukeni
Dawa ya kutokwa na usaha wa njano ukeni
Kuelewa zaidi kuhusu maambukizi ya chlamydia, soma katika makala ya maambukizi ya chlamydia. Wasiliana na daktari wako siku zote kupata uhakika wa nini unaumbwa.