Mwandishi:
Dkt. Benjamin L, MD
Mhariri:
Dkt. Adolf S, MD
Dawa za kutibu na kukinga maambukizi ya TB
28 Machi 2021 11:37:55
TB ni ugonjwa wa mapafu unaosumbua sana watu wengi duniani, historia zinaonyesha ugonjwa huu ulikuwa unaua kila mtu aliyeupata na dawa haikuwepo. Katika miaka ya 1882, Dr. Robert Koch aligundua bakteria anayesababisha TB na mwanga wa wanasayansi kuweza kugundua dawa. Toka mwaka huo TB imekuwa ikitibiwa bila mafanikio makubwa mpaka miaka ya 1940 ambapo dawa za TB zilianza kugunduliwa. Makala hii imezungumzia kuhusu dawa za kutibu na kujikinga na TB. Kumbuka dawa hizi hutumika kwa muunganiko, dawa moja huwa haina uwezo peke yake kutibu ugonjwa wa TB.
Madaraja ya dawa zinazotumika katika matibabu ya kifua kikuu (TB)
Dawa za TB daraja la kwanza
Isoniazid (INH)
Rifampin (RIF)
Ethambutol (EMB)
Pyrazinamide (PZA)
Rifapentine
Dawa za TB daraja la pili
Dawa za matibabu ya Tb daraja la pili zipo katika makundi matatu kutokana na mgawanyo wa WHO mwaka 2019 ambazo ni;
Kundi A
Kundi B
Kundi C
Malezo zaidi yapo hapa chini
Daraja la pili Kundi A
Levofloxacin
Moxifloxacin
Bedaquiline
Delamanid
Linezolid
Daraja la pili Kundi B
Clofazimine (Cfz)
Cycloserine (Cs) au terizidone (Trd)
Daraja la pili Kundi C na dawa zinazotumika kukinga maambukizi ya TB
Pyrazinamide (Z)
Imipenem-cilastatin (Ipm-Cln) au meropenem (Mpm)
Amikacin (Am) (au stretomycin) (S)
Ethionamide (Eto) au Prothionamide (Pto)
P-aminosalicylic (PAS)
Dawa zinazotumika kuzuia maambukizi ya TB kwa watu walio kwenye hatari
Isoniazid
Rifampicin
Rifapentine
Isoniazid plus rifampicin
Isoniazid plus rifapentine
Isoniazid + cotrimoxazole + pyridoxine
Maudhi ya dawa za kifua kikuu kundi la kwanza
Maudhi madogo
Kichefuchefu
Kutapika
Kuvurugika kwa tumbo
Maumivu ya tumbo
Kiungulia
Kuharisha
Maumivu ya misuli na maungio
Maumivu ya kichwa
Harara na muwasho wa ngozi
Kusinzia
Kizunguzungu
Kuhisi vitu vinazunguka
Kelele masikioni
Ganzi au hisia za kuchomachoma miguuni
Maudhi makubwa
Maumivu au kuvimba kwa maungio ya mikono au miguu
Kubadilika kwa kiasi cha mkojo
Kuongezeka kwa kiu au kukojoa sana
Kukojoa mkojo wenye damu
Kubadilika kwa uono
Mapigo ya moyo kwenda kasi
Kutokwa na damu kirahisi
Dalili za maambukizi mapya kama koo kuwa chungu na homa
Kubadilika kwa hali kama vile kukanganyikiwa
Degedege
Endapo unatumia dawa za kifua kikuu na unapata dalili zifuatazo ni vema ukawasiliana na daktari wako haraka.
Kufa ganzi/kuchomachoma au hisia za kuungua kwenye mikono au miguu
Matatizo ya kuona ikiwa pamoja na maumivu nyuma ya macho
Kifua kutoa miruzi au kupumua kwa shida
Maumivu makali ya tumbo
Kuharisha maji au damu