Mwandishi:
Dkt. Benjamin L, MD
Mhariri:
Dkt. Adolf S, MD
Dawa za kuyeyusha na kuzuia damu kuganda
21 Machi 2021 11:15:21
Kuna aina nyingi ya dawa za kuyeyusha damu, dawa hizi kiukweli huwa hazifanyi kazi ya kuyeyusha damu iliyoganda bali hufanya kazi ya kuzuia kuendelea kuganda kwa damu au kuendelea kukua kwa bonge la damu iliyoganda.
Makundi ya dawa za kuyeyusha damu
Dawa za kuyeyusha damu zipo kwenye makundi mawili ambayo ni;
Anticoagulants
Antiplatelet
Dawa za Anticoagulant
Anticoagulant huzuia damu kuganda au kuwa nzito na hivyo kuzuia uwezekano wa chembe sahani za damu kukusanyika, tukio ambalo linaweza kusababisha damu kuganda.
Mfano wa dawa za Anticoagulant na majina yake ya kibishara yaliyo kwenye mabano ni;
Apixaban (Eliquis)
Dabigatran (Pradaxa)
Edoxaban (Savaysa)
Fondaparinux (Arixtra)
Heparin (Fragmin, Innohep, and Lovenox)
Rivaroxaban (Xarelto)
Warfarin (Coumadin, Jantoven)
Dawa za Antiplatelet
Antiplatelet kazi yake ni kuzuia chembe sahani za damu(platelet) kukusanyika katika eneo lenye jeraha. Chembe sahani za damu kwa kawaida hukusanyika kwenye eneo la jeraha na kuanzisha mwitikio wa mwili kugandisha damu. Jambo hili ni jema kwani huzuia damu kutoka nyingi kwa mfano wa watu waliojikata au kupasuka mishipa ya damu ndani ya mwili.
Dawa za antiplatelet mfano wake na majina ya kibishara yaliyo kwenye mabano ni;
Aspirin
Clopidogrel (Plavix)
Dipyridamole (Persantine)
Prasugrel (Effient)
Ticagrelor (Brilinta)
Vorapaxar (Zontivity)
Kina nani hufaidika kutumia dawa za antiplatelet na antcoagulant?
Daktari wako anaweza kukuandikia utumie dawa jamii hii endapo una magonjwa yanayoongeza hatari au yale yanayosababishwa na damu kuganda kama vile;
Magonjwa ya mishipa ya damu ya moyo
Mshituko wa moyo
Magonjwa ya mfumo wa umeme wa moyo mfano mapigo ya moyo kwenda bila mpangilio
Ugonjwa wa deep vein thrombosis
Ugonjwa wa obeziti(uzito mkubwa kupita kiasi huongeza hatari ya damu kuganda)
Kufanyiwa upasuaji
Kuwa na kiwango kikubwa cha kolestrol kwenye damu wakati wa uzeeni
Kuwa na milango bandia ya moyo
Ugonjwa wa rheumatic ya moyo
Wagonjwa waliofanyiwa upasuaji mkubwa au upasuaji wa moyo
Kiharusi kutokana na sehemu ya ubongo kukosa damu
Madhara ya kutumia dawa za kuyeyusha damu
Moja ya madhara ya kutumia dawa za kuyeyusha damu ni kuvia kwa damu pamoja na kutoka kwa damu kirahisi au kwa muda mrefu mara unapojikata au kupata majeraha. Madhara makubwa yanayowez akujitokeza ni pamoja na;
Kuvia wa damu ndani ya ubongo kunakoweza pelekea kiharusi cha kuia damu
Upungufu wa chembe sahani za damu au chembe nyeupe za damu
Kuongezeka kwa shinikizo la damu
Ugonjwa wa kuvia damu kama hemophilia
Vidonda vya tumbo
Kutokwa na damu puani