top of page

Ugonjwa na dawa

Kurasa hii utajifunza kuhusu dawa na ugonjwa unaotibiwa na dawa hiyo. Wasiliana na daktari wako kabla ya kutumia dawa yoyotee ile ili kuepuka madhara na usugu wa dawa mwilini mwako. Kumbuka siku zote kuwa dawa ni sumu kwenye mwili wako endapo haitatumika bila ushauri wa daktari

Dawa za kutibu dutu ya sehemu za siri (Genital warts)

Dawa za kutibu dutu ya sehemu za siri (Genital warts)

Chunjua au dutu inafahamika pia kwenye tovuti hii kama 'maoteo sehemu za siri' ni aina mojawapo ya ugonjwa wa zinaa . Nusu ya wanaojihusisha na ngono mara kwa mara haswa isiyo salama hupata maambukizi haya kwenye muda fulani katika maisha yao na wanawake wanaathiriwa sana na haya kuliko wanaume.

Dawa za kutibu saratani ya shingo ya kizazi

Dawa za kutibu saratani ya shingo ya kizazi

Shingo ya kizazi ni mlango wa kuingilia kwenye kizazi, sehemu hii ni sehemu ya chini kwenye mlango wa kuingilia ndani ya mfuko wa uzazi. Kama ilivyo kibuyu, sehemu nyembamba ambayo inaenda kukutana na mdomo wa kibuyu, hufananishwa kuwa mfano mzuri wa shingo ya kizazi. Angalia kwenye picha kwa maelezo sehemu ilipo shingo ya kizazi.

Dawa za kutibu Saratani ya koo

Dawa za kutibu Saratani ya koo

Saratani ya koo ni saratani inayoanzia kwenye chembe zinazofunika kuta za koo. Kwa kawaida koo limetengenezwa na kuta ambazo chini yake kuna misuli. Hata hivyo saratani ya koo humaanisha saratani iliyo kwenye maeneo ya koo na kiboksi cha kutengenezea sauti

Dawa za maambukizi ya Human papillomavirus (HPV)

Dawa za maambukizi ya Human papillomavirus (HPV)

Maambukizi ya kirusi cha HPV huwa hayatibiki, madhara yanayoletwa na kirusi huyu huwa yanatibika pamoja. Hata hivyo kuna chanjo ya kinga pia ya kuzuia kupata maambukizi ya kirusi cha HPV inayotolewa kwa wanawake ambao bado hawajaanza kushiriki ngono au wasio na maambukizi ya kirusi huyu.

Dawa za kutibu Vaginosis ya bakteria

Dawa za kutibu Vaginosis ya bakteria

Bacterial vaginosis au vaginosis ya bakteria ni moja yaugonjwa wa zinaa unaoambukizwa kwa kujamiana. Endapo umepimwa na kukutwa na ugonjwa huu ni vema ukatumia dawa wewe na mpenzi wako kila mtu dozi yake, isipofanyika hivyo, utapata maambukizi upya kutoka kwa mpenzi wako ambaye hajatibiwa. Endapo una wapenzi wengi, wote wanabidi kutibiwa ili kuepuka kupata maambukizi utakaposhiriki nao tena.

bottom of page