Dawa
ULY CLINIC inakutahadharisha kuwa matumizi ya dawa pasipo ushauri wa daktari yanaweza kuleta madhara makubwa mwilini mwako.
Siku zote wasiliana na daktari wako kwa elimu na ushauri wa dawa gani na namna ya kutumia dawa inayoendana na hali yako halisi kama mbadala ya kujichukulia hatua mwenyewe.
Bonyeza 'Soma zaidi ' kwenye dawa unayohitaji kuanza kusoma kuhusu dawa hiyo..

Dawa Benzylpenicillin
Benzylpenicillin (Penicillin G) ni antibiotiki ya kundi la penicillin inayotumika kwa kuchomwa kutibu maambukizi makali ya bakteria kama nimonia, kaswende, meningitis na maambukizi ya damu. Hufanya kazi kwa kuzuia utengenezaji wa ukuta wa seli za bakteria na kwa ujumla huchukuliwa kuwa salama kwa wajawazito na mama wanaonyonyesha chini ya uangalizi wa daktari.

Dawa Cotrimoxazole
Cotrimoxazole ni antibayootiki ya mchanganyiko wa sulfamethoxazole na trimethoprim inayotumika sana Tanzania kutibu maambukizi ya mkojo, upumuaji, tumbo, ngozi na magonjwa nyemelezi kwa wagonjwa wenye kinga dhaifu. Hufanya kazi kwa kuzuia utengenezaji wa folate kwa bakteria, lakini inahitaji tahadhari maalum kwa wajawazito, wagonjwa wa figo, na watu wenye mzio wa sulfonamides.

Dawa ya Dextromethorphan
Dextromethorphan ni dawa ya kuzuia kikohozi kikavu inayofanya kazi kwenye mfumo wa kati wa fahamu(Ubongo) kwa kupunguza msisimko wa kituo cha kikohozi bila kutibu chanzo cha ugonjwa. Hutumika kwa kikohozi cha muda mfupi, inapaswa kutumiwa kwa tahadhari kwa watoto, wajawazito, na kuepukwa pamoja na pombe au dawa zinazoongeza hatari ya madhara ya mfumo wa fahamu.

Dawa Chlorpheniramine
Chlorpheniramine ni dawa ya antihistamine inayotumika kupunguza dalili za mzio kama mafua ya mzio, chafya, kuwashwa na kikohozi kinachosababishwa na mzio. Hufanya kazi kwa kuzuia histamine mwilini lakini inaweza kusababisha kusinzia, hivyo inapaswa kutumiwa kwa tahadhari, hasa kwa wazee, wajawazito na wanaonyonyesha.

Dawa Theophylline
Theophylline ni bronchodilator inayotumika kudhibiti pumu, COPD, na kuziba kwa njia za bronkai, lakini inaweza kusababisha mapigo ya moyo kwenda kasi, degedege, na kizunguzungu. Dozi lazima ichaguliwe na daktari kwa kuzingatia umri, uzito, magonjwa mengine, na dawa zinazoshirikiana.

Dawa Aminophylline
Aminophylline ni bronchodilator inayotumika kudhibiti pumu ya kifua na ugonjwa sugu wa kuziba kwa njia za hewa (COPD) kwa kupanua njia za hewa, lakini inaweza kusababisha mapigo ya moyo kwenda haraka, arithimia, na kizunguzungu. Dozi lazima ichaguliwe na daktari, ikizingatia umri, uzito na hali ya afya ya mgonjwa.

Dawa Promethazine
Promethazine ni antihistamine na antitussive inayotumika kupunguza allergy, kichefuchefu, na kikohozi kikavu, lakini inaweza kusababisha usingizi mkali na madhara makubwa kwa watoto, wajawazito, na wanaonyonyesha. Inapaswa kutumika tu chini ya uangalizi wa daktari na kwa dozi sahihi.
Hujapata dawa unayotafuta?
Endapo hujapata dawa unayotafuta andika katika kiboksi kilichoandikwa "Tafuta chochote hapa...." juu ya kurasa hii na endapo hujapata katika kiboksi hiko basi wasiliana na wafamasia wa ULY CLINIC maelezo zaidi kuhusu dawa.
Wasiliana na daktari wa ULY CLINIC kwa ushauri na tiba kwa kubofya linki ya 'Mawasiliano yetu' au 'Pata tiba' chini ya tovuti hii



