top of page

Mwandishi: ULY-CLINIC

​

Mhariri: Leticia M, BPHARM, Dkt. Benjamin L, MD

​

18.10.2018

​

 

Dawa salama kipindi kabla ya ujauzito, ujauzito na kujifungua

​

Dawa zinazotumika sana kipindi cha ujauzito ni zile zilizo katika makundi yafuatayo;

  • Dawa za kuzuia kutapiaka(antemetics)

  • Dawa za kuzuia uzalishaji tindikali(antacid)

  • Dawa za aleji (anthistamine)

  • Dawa za kupooza maumivu(analegesics)

  • Dawa za kupambana na vijidudu vya bakteria (antimicrobial)

  • Dawa za kutuliza mwili (tranquilizers) hypnotic

  • Dawa za kupunguza maji mwilini (diuretics) na

  • Dawa ya kulevya

​

Shirika la chakula na dawa duniani FDA liligawa  dawa katika makundi ma 5 kulingana na usalama wake kipindi cha ujauzito. Makundi haya ni A, B, C, D na X. Mgawanyiko huu ulifanyika mwaka 1979 na umefanyiwa marekebisho na kuja na utaratibu mpya ambao umeanza kutumika mwaka 2015.

 

Tafiti chache za dawa zimefanyika kuonyesha usalama wa dawa kipindi cha ujauzito. Taarifa nyingi kuhusu usalama wa dawa kwa mama mjamzito zimefanyika kwa wanyama wengine, mara baada ya dawa hizo kuonekana zipo salama basi huweza kutumiwa na wamama wajawazito na madhara yanapoonekana, taarifa hizo hutumika kama sehemu ya tafiti ya madhara ya dawa.

 

Wakati wa ujauzito dawa hutumika katika matibabu ya baadhi ya magonjwa au shida Fulani, ingawa kuna wasiwasi wa usalama wa matumizi ya dawa kipindi cha ujauzito, dawa nyingi zimeripotiwa kusababisha madhaifu kwa mtoto kwa asilimia 2 hadi 3 ya madhaifu ya kiuumbaji yanayotokea kwa watoto bila kuhuisha pombe.

​

Si kwamba dawa zote zinaweza kupita kwenye kitovu cha mtoto na kuingia kwa mtoto wakati yupo ndani ya mama.

 

Dawa zenye uwezo wa kupita na kuingia kwa mtoto huweza kusabaisha matatizo ya kiuumbaji wa mtoto. Dawa ambazo hazipiti pia huweza kumdhuru mtoto kwa kusinyaza kitovu na hivyo kuzuia uingiaji wa damu na chakula kwa mtoto akiwa tumboni kwa mama, pia huweza kusababisha kusinyaa kwa mfuko wa kizazi na kusababisha mtoto kukandamizwa na kukosa hewa, au kusababisha matatizo kwa mama kama shinikizo la chini la damu.

 

Madhara ya dawa kwa kichanga hutegemea umri wa kichanga tumboni, dozi ya dawa, ukali wa dawa. Dawa zinazotumiwa kabla ya wiki 20 za ujauzito baada ya uchavushwaji huwa na madhara mengi au haina madhara kipindi cha ujauzito.

 

Madhara ya kiuumbaji yanaweza yasitokee kipindi hiki.Kipindi cha uumbaji wa viungo vya binadamu(Siku ya 14 hadi 56) dawa zilizo sumu zikitumika huweza kusababisha matatizo ya kiuumbaji kwa kichanga. Dawa zinazoingia kwa kichanga kipindi cha ujauzito zinaweza kusababisha;

​

  • Mimba kutoka

  • Kuzaliwa na maumbile yasiyo ya kawaida

  • Madhara ya kimetaboli katika seli(huweza kutokea kabla, wakati au miaka mingi baada ya kuzaliwa)

 

Dawa zinazotumika mara baada ya uumbaji wa viungo vya binadamu yaani miezi mitatu ya pili na mitatu ya mwisho kipindi cha ujauzito huweza zisisababishe madhara au zinaweza kusababisha utendaji kazi mbaya wa organi zilizotengenezwa.

 

Karika viboksi vimeelezea mifano ya dawa zilizo kwenye kundi husika, kundi C, D na X yametolewa mifano kwa sababu ni kundi lililofahamika kuwa salama kwa kichanga.Hata hivyo ni vema kufahamu mabadiliko mapya ya makund haya ya dawa ili kuyatumia kama yalivyoelezewa hapa chini.

 

Sheria mpya ya makundi ya dawa salama kipindi cha ujauzito

​

Mabadiliko ya makundi ya dawa kipindi cha ujauzito

​

Makundi ya dawa kipindi cha ujauzito kama yalivyoelezewa hapo juu yalianza kutumika toka mwaka 1979, makundi hayo yalikuwa muhimu sana, hata hivyo mwaka 2015 shirika la dawa na chakula duniani liliona kubadilisha utaratibu kutokana na changamoto za matumizi ya makundi hayo ya alfabeti A, B, C, D na E kwa wajawazito, wanaotarajia kuwa wajawazito na watalamu wa afya(daktari). Changamoto hizo moja ilikuwa ni kutoeleweka vema kwa makundi hayo hivyo kufanya dawa fulani isitumiwe au itumike bila kuwa na ushahidi uliofanyika kwa wanyama au binadamu kama ulivyosoma/utakavyosoma  kwenye makundi haya ya alfabeti. Kufikia mwaka 2020 dawa zote zinatakiwa kuwa na mabadiliko mapya katika kipengele cha usalama wa dawa kipindi cha ujauzito.

​

Makundi mapya ni yapi?

​

Makundi yanayotumika kwa sasa yanafanana na makundi ya zamani lakini yapo kwenye maelezo zaidi kama yalivyoelezewa hapa chini.

 

Ujauzito( hujumuisha pia kipindi cha uchungu na baada ya kujifungua- siku 42)

​

Kundi hili huwa na maelezo yafutayo

​

  • Mfumo wa ukusanyaji na utunzaji wa taarifa za matumizi ya dawa zilizo ruhusiwa na FDA

  • Muhtasari wa madhara ya dawa

  • Taarifa kuhusu madhara yanayoonekana/yaliyoonekana moja kwa moja kwa mtumiaji

  • Taarifa za kina kuhusu muhtasari wa madhara

​

Kipindi cha kunyonyesha 

​

Kipengele hiki hutoa maelezo kuhusu matumizi ya dawa, kiwango cha dawa na Maelezo ya ziada kuhusu matumizi ya dawa kipindi cha kunyonyesha. VIpengele vyake ni

​

  • Muhtasari wa madhara ya dawa

  • Taarifa kuhusu madhara yanayoonekana/yaliyoonekana moja kwa moja kwa mtumiaji

  • Taarifa za kina kuhusu muhtasari wa madhara

​

Matumizi kwa wanawake na wanaume wenye uzazi

​

Kipengele hiki ni kipya na hakikuwepo kwenye kundi la awali la kutumia alfabeti. Kipengele hiki kinazungumzia taarifa zinazohusu umuhimu/uhaja wa kufahamu kuhusu;

  • Kupima ujauzito kabla ya kutumia dawa

  • Matumizi ya dawa pamoja na uzazi wa mpango

  • Matumizi ya dawa na uzazi 

​

Kutokana na mabadiliko mapya, ULY CLINIC itaendelea kuelezea dawa zake kulingana na makundi haya mapya ili kukurahisishia kuchagua kutumia dawa kulinganana maelezo.

​

Bofya hapa kwenda kwenye orodha ya dawa na ushauri wa matumizi wakati wa ujauzito na kunyonyesha

Dawa zimeonyesha hazina madhara kwa kichanga tumboni kutokana na tafiti zilizofanyika kwa binadamu

Kwa tafiti za wanyama dawa zimeonyesha hazina madhara kwa kichanga, hakuna tafiti zilizofanyika kwa binadamu au tafiti kwa wanyama zimeonyesha madhara ila kwa binadamu hazijaonyesha madhara kwa kichanga

Hakuna tafiti za kutosha zilizofanyika kwa binadamu au wanyama, au tafiti zimefanyika kwa wanyama na kuonyesha madhara lakini kwa binadamu hakuna tafiti zilizofanyika

Ushahidi wa madhara kwa kichanga kwa binadamu upo lakini faida ya kutumia dawa inaweza kuwa kubwa kuliko madhara kwa mtoto endapo mfano(ugonjwa wa kufisha mama,ugonjwa mbaya amabapo dawa salama haziwezi kutibu ila ile isiyo salama inaweza)

Imethibitishwa Madhara ni makubwa kwa mtoto kuliko faida zinazoweza kupatikana kwa matumizi ya dawa kipindi cha ujauzito.

Baadhi ya dawa ambazo ni sumu kwa kijusi na mama mjamzito

 

Dawa zifuatazo ni sumu kwa mama na kichanga na hazipaswi kutumika wakati wa ujauzito;

​

Dawa jamii ya ACE, Pombe, Aminopterin, Androgens, Carbamazepine, Coumarins, Danazol, Dethylstilbestrol, Etretine, Isotretinoin, lithium, Methimazole, Methotrexate, Phenytoin, radioactive Iodine, Tetracycline, Trimethadione, Valproate

​

​

Unashauriwa kwa sasa usitumie makundi ya alfabeti A, B, C, D na E kwa kuwa yamepitwa na wakati. Endapo una shida ya kufahamu usalama wa dawa kipindi cha ujauzito basi wasiliana na daktari wako akupe taarifa sahihi na zinazoendana na wakati ili kumlinda mwanao na uzazi wako.

​

Wasiliana na daktari wa ULY CLINIC kwa ushauri na maelezo zaidi kuhusu makundi haya ya dawa kupitia nambaza simu au bonyeza pata tiba chini ya tovuti hii

​

Imeboreshwa,   13.08.2021

​

Rejea za mada

​

  1. CHEMM. FDA pregnancy category. https://chemm.nlm.nih.gov/pregnancycategories.htm.Imechukuliwa 28.10.2020

  2. FDA.Pregnancy and lactation labeling fInal rule. https://www.fda.gov/drugs/labeling-information-drug-products/pregnancy-and-lactation-labeling-drugs-final-rule. Imechukuliwa 28.10.2020

  3. Drugs.com.  New FDA prefnancy category. https://www.drugs.com/pregnancy-categories.html. Imechukuliwa 28.10.2020

  4. FDA.pdf. The prenancy and lactation labeling rule. https://www.fda.gov/media/100406/download. Imechukuliwa 28.10.2020

  5. Drugs.FDA http://www.accessdata.fda.gov/scripts/cder/drugsatfda/in dex.cfm.  Imechukuliwa 28.10.2020

  6. Daily Med (National Library of Medicine) http://dailymed.nlm.nih.gov/dailymed/about.cfm.  Imechukuliwa 28.10.2020

bottom of page