Dawa ya kutibu gono kwa mwanaume ni ipi?
Orodha ya dawa za gono kwa mwanaume.
Dawa ya kutibu usaha uumeni.
Dawa ya kuondoa usaha kwenye uume.
Maelezo muhimu ya kufahamu kabla ya kufahamu dawa
Gono ni moja ya ugonjwa wa zinaa unaosababishwa na maambukizi ya bakteria mwenye jina la Nisseria gonorrhoear, ambaye huenezwa kwa njia ya kujamiana na mtu mwenye maambukizi. Dalili kuu ya ugonjwa zimeelezewa katika makala nyingine ya dalili za gono kwa wanaume.
Dawa za kutibu gono zipo za aina nyingi kutegemea eneo na eneo pia nchi na nchi. Utofauti huu huletwa na mambo mbalimbali ikiwa pamoja na hali ya mwitikio wa kimelea kwenye dawa husika. Baadhi ya vimelea vimebadili tabia na hivyo havisikii dawa ambazo hapo awaki zimekuwa zikitibu ugonjwa huo.
Kwa kawaida watu wengi huchanganya ugonjwa wa gono na magonjwa mengine ya zinaa, kwa kuzania kuwa kutoka usaha kwenye uume hunasababishwa na gono tu. Hii si kweli, kuna magonjwa mengine yanaweza kupelekea uume kutoa usaha ambayo mara nyingi huwa magonjwa mengine ya zinaa pia. Hii ndio maana endapo una dalili hii ya gono ni muhimu kutibiwa magonjwa mengine ya zinaa yanayosababisha dalili hii iki kuhakikisha unapona haswa pale ambapo vipimo huwa havifanyiki au kutohitajika kufanyika.
Dawa za gono kwa wanaume
Inashauriwa ili kupata matibabu sahihi, wasiliana na daktari wako kwa ushauri na tiba. Baadhi ya dawa za kutibu gono kwa wanaume ni;
Kuona orodha kamili ya dawa za kutibu gono bofya soma makala ya dawa za gono.
Kumbuka
Endapo mgonjwa atatumia dawa sahihi na dozi sahihi atapona kwa wakati. Inashauriwa kutotumia dawa pasipo kushauriwa na daktari ili kuepuka madhara ya dawa na usugu wa vimelea kwenye dawa.
Majina mengine.
Gono hufahamika kwa majina mengine kama kisonono.
Namna ya kuwasiliana na daktari hapa ni ipi?
Kuna gono nyingine huwa haiponi mpaka ubadilishe dawa pia