top of page

Dalili na viashiria bonyeza herufi ya kwanza kusoma zaidi

[A] [B] [C] [D] [E] [F] [G] [H] [I] [J] [K] [L] [M] [N] [O] [P] [Q] [R] [S] [T] [U] [V] [W] [X] [Y] [Z] [#]

Mwandishi:

Dkt. Sospeter B, MD

Mhariri:

Dkt. Salome A, MD

18 Machi 2021 16:20:06

Presha ya kushuka matibababu ya nyumbani

Presha ya kushuka matibababu ya nyumbani

Presha ya kushuka huitwa kitiba kama hypotension, endapo una presha ya kushuka ni vema kufahamu ni nini kisababishi cha presha yako. Aina kadhaa za presha ya kushuka zinafahamika, ambazo zimezungumziwa kwenye makala hii na matibabu yake ya nyumbani ni;


  • Kuwa makini unapokuwa unaamka,

  • Presha ya kushuka unapoamka asubuhi na mapema,

  • Presha ya kushuka baada ya kula,

  • Presha kushuka unapolala chali

  • Presha ya kushuka kutokana na upungufu wa damu


Dalili za presha ya kushuka/Presha kushuka


Baadhi ya dalili zinazoweza kuonekana kwa mtu mwenye presha iliyoshuka ni pamoja na


Kichwa kuwa chepesi

Kizunguzungu au kuhisi vitu vinazunguka

Uchovu wa mwili

Kutoweza kuwaza vema

Maumivu ya kichwa

Kuzimia

Kuhisi kuzimia

Mapigo ya moyo kwenda mbio

Kichefuchefu

Hisia za baridi miihsio ya mwili(vidoleni)

Maumivu ya kifua


Presha ya kushuka unapoamka asubuhi na mapema

Unaweza fanya mambo yafuatayo kutibu presha ya kushuka wakati wa asubuhi unapokuwa unaamba kutoka kitandani.


Usiamke haraka

Tumia dakika 3 hadi 5 kuamka. Fanya hivi unapohisi unataka kuamka, fumbua macho kwanza, kisha fikiria kwa dakika mbili kuhusu kuamka kwenye kitanda chako, kisha kaa wakati miguu bado ipo kitandani kwa muda wa dakika 1, kisha weka miguu chini ya kitanda kwa muda wa dakika 2 kabla ya kusimama


Nyanyua kitanda chako sehemu kichwa kinapolala na punguza kukojoa usiku

Kunyanyua kitanda itasaidia mwili uzoee pozi hilo na kusababisha shinikizo lako la damu lishishuke sana wakati unataka kusimama.


Kunywa glasi moja ya maji ya baridi dakika 30 kabla ya kuamka

Hii itaongeza kiasi cha maji kwenye mishipa ya damu, maji haya hupelekea moyo kuweza kusukuma damu kwenye maeneo muhimu ya ubongo na hivyo kupunguza dalili za kuzimia na kushuka kwa shinikizo la damu.


Presha ya kushuka baada ya kula

Kula chakula kidogo na mara nyingi zaidi, epuka kula mlo mkubwa kwa wakati mmoja na punguza kiasi cha pombe unachokunywa kwenda kiasi kinachoshauriwa

Usitumie vinywaji au vyakula vya moto, vyenye wanga kwa wingi kwa kuwa huongeza hatari ya kushuka kwa presha baada ya kula.


Presha kushuka unapolala chali

  • Usitumie dawa za kupandisha presha inapofika sa 12 jioni

  • Inua kitanda chako au weka mito miwili wakati unalala

  • Kula kitafunwa na kikombe kimoja cha chai ya uvuguvugu

  • Jaribu kinywa glasi moja ya wine wakati wa kulala

  • Ondoa vigandamiza tumbo kabla ya kulala


Presha ya kushuka kutokana na upungufu wa damu

  • Tumia dawa kama ulivyoelekezwa na daktari wako

  • Kama unaweza choma homon erythropoietin choma ili kuongeza uzalishaji wa chembe nyekundu za damu na hivyo kuondoa tatizo hili.

  • Tumia vyakula vya kuongeza damu


Hali zinazoshusha shinikizo la damu


Hali ambazo zinaweza kuamsha au kufanya shinikizo la damu lishuke sana ni;


  • Kuishiwa maji mwilini

  • Wakati wa asubuhi endapo umetumia dawa za kupunguza maji mwilini

  • Kuamka ghafla kutoka kwenye pozi la kulala

  • Kusimama muda mefu bila kutembea

  • Kufanya mazoezi makalai au mazoezi ya aina moja

  • Kunywa pombe

  • Kula mlo mkubwa wenye wanga

  • Kukaa kwenye joto kali au kuwa na homa

  • Kukenya wakati wa kukojoa au wakati wa haja kubwa


Matibabu ya presha ya kushuka kwa undani zaidi


Endapo una presha ya kushuka wakati unasimama, fanya mambo yafuatayo;


  • Tumia vikandamiza, au vibana tumbo unapotoka kwenye kitanda chako

  • Kunywa maji asubuhi na mapema. Kunywa maji ya baridi robo lita (glasi moja) wakati wa asubuhi kabla ya kusimama kwa muda mrefu

  • Lala kwenye kitanda kilichoinuka maeneo ya kichwa

  • Inua kitanda kwenye eneo unaloweka kichwa kwa kutumia mto au kutumia kitanda chenye uwezo huo wa kuinuka. Inua ifike nnchi 4 tu.

  • Fanya mazoezi ya kuongeza shinikizo la damu. Kwa kufanya mazoezi haya kwa muda wa nusu dakika au dakika moja kwa kila zoezi, utaweza kufanya mwili uongeze shinikizo la damu wakati umesimama kwa muda mrefu. mazoezi hayo ni;

  • Kunyanyua kidole gumba

  • Kukunja nne kisha kubana na kuachia misuli ya vidole vya miguu na miguu

  • Kuchezesha misuli ya paja

  • Kujikunja kwenye nyonga kama unainama na kuinuka au kuinamia upande mmoja wa mwili kisha mwingine

  • Kuweka miguu juu ya usawa wa mwili

  • Kutembea kwa marching


Matumizi ya dawa


Dawa zinazoamsha shinikizo la damu ni kama vile


  • Midodrine

  • Fludrocortisone

  • Pyridostigmine


Fanya mazoezi

Epuka kukaa bila kufanya mazoezi, fanya mazoezi ya wastani na si makali maamna utashusha shinikizo lako la damu kwa mazoezi makali.


Tumia chumvi kwenye maji unayokunywa

Hii itabisi uwasiliane na daktari wkao endapo inafaa kutumia chumvi kwenye maji ya kunywa kwa sababu ni hatari kwa baadhi ya watuw enye magonjwa ya moyo, figo n,k

Endapo unafaa kutumia chumvu na umeshauriwa unaweza tumia, tumia kiasi cha gramu 10 hadi ishirini kwa siku tu. Weka chumvi kwenye maji ya kunywa kwa siku. Kumbuka unatakiw akunywa glasi nane kwa siku sawa na lita mbili.


Endapo huwezi weka chumvi, unaweza tumia Oral (ORS) ambayo huwa na chumvi na madini mengine pamoja na sukari. Hii inabidi pia ushauriwe na daktari wako endapo ni salama kulingana na afya yako, mfano inaweza kuwa si nzuri kwa wagonjwa wenye kisukari kwa sababu huweza pandisha kiwango cha sukari kwenye damu. Namna ya kutuia ni kuweka paketi moja ya oral(ORS) kwenye lita moja ya maji kisha kunywa kwa jinsi unavyoweza ili mradi unywe lita mbili kwa siku kwa watu wazima.


Inashauriwa pia kutumia vyakula vyenye madini ya potassium kwa sababu kutumia chumvu huongeza kupotea kwa madini haya hivyo huweza pelekea kuharibu mfumo wa umeme wa mwili na moyo.


Elimu ya ziada


Unatakiwa kutambua dalili zinazoashirika kushuka kwa shinikizo la damu wakati unainuka ili uweze kukaa haraka kabla ya kuinuka ili kuepuka kuanguka.

Fahamu kuhusu hali na mambo yanayoweza kushusha shinikizo la damu kama vile kula mlo mkubwa wa wanga, kubadili pozi la mwili kutoka pozi la kulala kwenda la kusimama, joto, homa na mazoezi au kuoga maji ya moto.

Jifunze na kufahamu mamabo unayoweza kufanya ili kuongeza shinikizo la damu.


Kumbuka

Matibabu ya presha ya kushuka hulenga kutibu visababishi, njia zilizotajwa hapa juu ni njia za matibabu ambazo zinalenga kupandisha shinikizo la damu. Ni vema ukawasiliana na daktari wako kwa kila kitu unachotaka kukifanya ili kupata matibabu yanayoendana na afya yako.

ULY CLINIC inakushauri siku zote uwasilianane na daktari wako kwa ushauri zaidi na tiba kabla ya kuchukua hatua yoyote baada ya kusoma makala hii

Wasiliana na daktari wa ULY clinic kwa kupiga namba za simu  au kubonyeza sehemu imeandikwa "Pata tiba" chini ya tovuti hii.

Imeboreshwa,

21 Julai 2023 16:18:21

Rejea za mada hii;

1. Sjöstrand, Torgny. "The regulation of the blood distribution in man." Acta physiologica Scandinavica 26.4 (1952): 312-327. Inapatikana hapa https://www.ncbi.nlm.nih.gov/pubmed/13007487

2. Ziegler, M. G., Lake, C. R., & Kopin, I. J. (1977). The sympathetic-nervous-system defect in primary orthostatic hypotension. New England Journal of Medicine, 296(6), 293-297. Inapatikana hapa https://www.ncbi.nlm.nih.gov/pubmed/831126

3. Lipsitz LA, Pluchino FC, Wei JY, Rowe JW. Syncope in institutionalized elderly: the impact of multiple pathological conditions and situational stress. J Chronic Dis. 1986;39:619–630. Inapatikana https://www.ncbi.nlm.nih.gov/pubmed/3090090. Inapatikana https://www.ncbi.nlm.nih.gov/pubmed/10081712

4. Mtinangi BL, Hainsworth R. Effects of moderate exercise training on plasma volume, baroreceptor sensitivity and orthostatic tolerance in healthy subjects. Exp Physiol. 1999;84:121–130.

5. Bonnin P, Ben Driss A, Benessiano J, Maillet A, Pavy le Traon A, Levy BI. Enhanced flow-dependent
vasodilatation after bed rest, a possible mechanism for orthostatic intolerance in humans. Eur J Appl Physiol. 2001;85:420–426. Inapatikana https://pubmed.ncbi.nlm.nih.gov/11606010/

6. Gibbons CH, Freeman R. Delayed orthostatic hypotension: a frequent cause of orthostatic intolerance. Neurology. 2006;67:28–32. Inapatikana https://www.ncbi.nlm.nih.gov/pubmed/16832073

7. Poon IO, Braun U. High prevalence of orthostatic hypotension and its correlation with potentially causative medications among elderly veterans. J Clin Pharm Ther. 2005;30:173–178. Inapatikana https://www.ncbi.nlm.nih.gov/pubmed/15811171

8. Weiss A, Grossman E, Beloosesky Y, Grinblat J. Orthostatic hypotension in acute geriatric ward: is it a consistent finding? Arch Intern Med. 2002;162:2369–2374. Inapatikana https://www.ncbi.nlm.nih.gov/pubmed/12418952

9. Mader SL, Josephson KR, Rubenstein LZ. Low prevalence of postural hypotension among community-dwelling elderly. JAMA. 1987;258:1511–1514. Inapatikana https://www.ncbi.nlm.nih.gov/pubmed/3625952

10. Sandroni P, Ahlskog JE, Fealey RD, Low PA. Autonomic involvement in extrapyramidal and cerebellar disorders. Clin Auton Res. 1991;1:147–155. Inapatikana https://www.ncbi.nlm.nih.gov/pubmed/1822762

11. Saito Y, Matsuoka Y, Takahashi A, Ohno Y. Survival of patients with multiple system atrophy. Intern Med. 1994;33:321–325. Inapatikana https://www.ncbi.nlm.nih.gov/pubmed/7919616

12. Davis BR, Langford HG, Blaufox MD, Curb JD, Polk BF, Shulman NB. The association of postural changes in systolic blood pressure and mortality in persons with hypertension: the Hypertension Detection and Follow-up Program experience. Circulation. 1987;75:340–346. Inapatikana https://www.ncbi.nlm.nih.gov/pubmed/3802437

13. Luukinen H, Koski K, Laippala P, Kivelä SL. Prognosis of diastolic and systolic orthostatic hypotension in older persons. Arch Intern Med. 1999;159:273–280. Inapatikana https://www.ncbi.nlm.nih.gov/pubmed/9989539.

14. Hoeldtke RD, Streeten DH. Treatment of orthostatic hypotension with erythropoietin. N Engl J Med. 1993;329:611–615. Inapatikana hapa https://www.ncbi.nlm.nih.gov/pubmed/8341335

15. Denq JC, Opfer-Gehrking TL, Giuliani M, Felten J, Convertino VA, Low PA. Efficacy of compression of different capacitance beds in the amelioration of orthostatic hypotension. Clin Auton Res. 1997;7:321–326. Inapatikana hapa https://www.ncbi.nlm.nih.gov/pubmed/9430805

16. Sjostrand T. Volume and distribution of blood and their significance in regulating the circulation. Physiol Rev. 1953;33:202–228. Inapatikana hapa https://www.ncbi.nlm.nih.gov/pubmed/13055444

17. Rowell LB, Detry JM, Blackmon JR, Wyss C. Importance of the splanchnic vascular bed in human blood pressure regulation. J Appl Physiol. 1972;32:213–220. Inapatikana hapa https://www.ncbi.nlm.nih.gov/pubmed/4550275

bottom of page