top of page

Imeandikwa na daktari wa ULYclinic

Jumanne, 31 Machi 2020

Adrenalini

Adrenalini

Homoni ya adrenalini ikijulikana pia kama epinefrini ni homoni inayotolewa awali na tezi za adreno pamoja na sehemu ya ubongo inayoitwa medula oblangata, kazi yake kuu pamoja na noradrenalini(noraepinephrine) ni kuandaa mwili 'Kupambana au kukimbia' wakati wa tukio la ghafla. Adrenalini ni homoni na pia ni dawa.

Homoni hii inachukua jukumu muhimu katika mwitikio wa kupambana au kukimbia kwa kuongeza mzunguko wa damu kwenye misuli, usukumaji wa damu kwenye moyo na kiwango cha sukari kwenye damu. Homoni hii inapatikana katika wanyama wengi na viumbe vingine wenye sifa za seli moja.

Ndani ya dakika chache wakati wa hali ya kufadhaisha au kusitusha, homoni hii hutolewa kwa haraka na kuingia kwenye mishipa ya damu, ili kujiaanda na hali fulani ya mfadhaiko au kushitusha.

Je! Adrenalini inadhibitiwa vipi?

Adrenalini inatolewa kwa kupewa taarifa kutoka kwenye ubongo, taarifa hizo kwa kupitia mishipa iliyounganishwa kwenye tezi za adreno, husababisha kutolewa kwa adrenalini. Utaratibu huu hufanyika haraka sana ndani ya dakika 2 hadi 3 za tukio lililotokea .

Hali ya hofu au msongo wa mawazo inapoisha, mishipa ya fahamu ya tezi za adreno husinyaa na hivyo kusababisha tezi za adreno kuacha kutoa homoni ya adrenaline.

Je! Kazi ya adrenaline ni nini?

Adrenalini inasababisha mwitikio wa kupambana au kukimbia baada ya tukio la ghafla. Hali hii husababisha kupumua kwa kina ili hewa kuzama mapafuni na kutoa hewa ya oksijeni inayohitajika kuipa uwezo seli kuzalisha nguvu.

Adrenalini pia husababisha mishipa ya damu kuelekeza damu moja kwa moja kwenye misuli, pamoja na moyo na mapafu. Uwezo wa mwili kuhisi maumivu pia hupungua kwa sababu ya adrenalini, ndiyo sababu unaweza kuendelea kukimbia au kupigana na hatari hata kama umejeruhiwa.

Adrenalini husababisha kuongezeka kwa umahiri wa nguvu na utendaji pia kwa tatizo ulilolipata katika nyakati za hatari. Baada ya hatari kupungua, athari za adrenalini zinaweza kudumu kwa saa moja.

Shida zinazohusiana na adrenalini

Adrenalini homoni ni muhimu kuwezesha mwili wako kuishi. Wakati mwingine mwili hutoa homoni hii hata wakati ambapo hamna tukio la ghafla au hatari na hivyo homoni haikabiliani na hatari ya kweli. Hii inaweza kusababisha hisia za kizunguzungu, maumivu ya kichwa na mabadiliko ya kuona.

Adrenalini husababisha kutolewa kwa sukari kwenye damu wakati hakuna mahitaji ya sukari hiyo.

Hali hii inaweza kumfanya mtu ahisi kutulia au kukasirika. Kiwango cha juu cha homoni kinachotolewa bila tukio halisi kinaweza kusababisha uharibifu wa moyo, kukosa usingizi na hisia za neva.

Kuongezeka kwa uzalishaji wa homoni ya inaweza kusababishwa na saratani ya adreno na kupata dalili za wasiwasi, kupungua uzito, mapigo ya moyo kwenda kasi na shinikizo la damu la juu.

Kutolewa kwa Adrenalini kidogo sana hutokea mara chache, lakini ikitokea hivyo uwezo wa mwili kuitikia vizuri katika hali ya hatari hupungua.

Athari za uzalishaji wa Adrenalini kwa wingi;

• Unyofu wa mwili,
• Kuwa na wasiwasi,
• Kutoka na jasho,
• Mapigo ya moyo kwenda haraka ya haraka
• Shinikizo la damu la juu

ULY CLINIC inakushauri uwasiliana na daktari wako kabla ya kuchukua hatua yoyote baada ya kusoma makala hii

Kwa ushauri zaidi na tiba unaweza kuwasialiana na daktari wa ULY CLINIC kupitia linki ya 'mawasialiano yetu' chini ya tovuti hii

Imeboreshwa,

31 Machi 2020 18:11:34

Rejea za mada hii;

bottom of page