top of page

Imeandikwa na daktari wa ULY Clinic

Jumatano, 25 Machi 2020

Insulin

Insulin

Utangulizi

Insulin ni homoni inayotengenezwa na kongosho inayofanya kazi ya kuruhusu sukari aina ya glukosi iingie kwenye seli na kuipa nguvu ifanye kazi au kuhifadhi sukari hiyokwa matumizi ya baadae.

Mbali na kazi hiyo muhimu, insulin pia hufanya kazi ya kurekebisha kiwango cha sukari kwenye damu.

Kwa kawaida glukosi huwa haina uwezo wa kuingia moja kwa moja ndani ya seli bila kufunguliwa mlango na insulin.

Mara baada ya kula chakula kiwango cha sukari huongezeka sana kwenye damu, hivyo tezi ya kongosho huanza kuzalisha homoni ya insulin. Insulin inayozalishwa huingia kwenye damu na kisha hujishikiza kwenye kuta za seli na kufungua mlango wa glukosi ili iingie kwenye seli.

Endapo kiwango cha glukosi katika damu ni kikubwa kuliko matumizi, insulin husaidia kuhifdhi sukari hiyo kwenye seli za Ini. Sukari hii iliyohifadhiwa hutolewa endapo kuna mahitaji au kiwango kidogo cha sukari katika damu kama wakati wa mazoezi au wakati umefunga kula chakula. Kwa maana hiyo insulin husaidia kusawazisha kiwango cha sukari mwilini.

Kama mwili wako hauzalishi kiwango cha kutosha cha insulin au seli kuleta upinzani dhidi yake, kiwango cha glukosi kwenye damu hupanda na kusababisha tatizo la haipaglaisemia. Hali ya haipaglaisemia ikidumu kwa muda mrefu huweza kusababisha madhara mwilini na huhusiana na kisukari aina ya pili(soma kwenye kuhusu kisukari aina ya pili kwenye tovuti hii)

Endapo mwili hauzalishi insulin ya kutosha au kuna upinzani dhidi ya insulin kwa muda mrefu mtu hupata tatizo la kisukari

Insulin na kisukari

Kisukari- Kinaelezewa na umoja wa kisukari Amerika kuwa ni ugonjwa unatotokana na kutozalishwa au kutotumiwa vema kwa insulin mwilini.

Visababishi vya kisukari vinaweza kuwa sababu za kimazingira na maisha au kurithi. Kwa baadhi ya visababishi vya kisukari kama vile Maisha ya kutoushuhgulisha mwili kwa kazi za kutoa jasho na uzito kupita kiasi unaweza kupelekea kupata kisukari aina ya pili(soma zaidi kwenye mada ya kisukari).

Nini huweza kusababisha kiwango cha chini cha insulin?

Kuna baadhi ya hali, dawa na magonjwa yanayoweza kusababisha kiwango cha homoni insulin kuzaliswa kwa kiasi kidogo kama vile; kuondolewa kongosho (kwa njia ya upasuaji) matumizi ya dawa za corticosteroid, dawa za beta blocker na dawa ya phenytoin

Nini husababisha kuzalishwa kwa wingi kwa homoni insulin?

Kiwango cha juu cha homoni ya insulin kwenye damu husababishwa awali na upinzani wa seli kwenye homoni hii ya insulin. Upinzani huu husababisha kongosho kuzalisha kiwango kikubwa cha insulin. Sababu zingine ni pamoja na; saratani ya kongosho inayoitwa insulinoma, na kuwepo kwa kiwango kikubwa cha seli za nesidioblastosis zinazozalisha insulin kwa wingi kwenye kongosho.

Dalili za kiwango kikubwa cha insulin kwenye damu ni;

• Kutokwa na jasho jingi
• Kutetemeka
• Mapigo ya moyo kubadilika(kwenda nivyo sivyo)
• Kuchanganyikiwa/konfyusheni
• Kupata njaa kali
• Kuona ukungu
• Kifo

Dalili za kiwango kikubwa cha insulin kwenye damu ni;

• Kuongezeka uzito sana(obeziti)
• Njaa ya sukari(kula sukari sana)
• Kuhisi njaa inauma mara kwa mara
• Kula mara kwa mara
• Kupungua kwa umakini
• Tatizola shauku na kupaniki
• Uchovu wa mwili wa kupitiliza

ULY CLINIC inakushauri uwasiliana na daktari wako kabla ya kuchukua hatua yoyote baada ya kusoma makala hii

Kwa ushauri zaidi na tiba unaweza kuwasialiana na daktari wa ULY CLINIC kupitia linki ya 'mawasialiano yetu' chini ya tovuti hii

Imeboreshwa,

9 Aprili 2020 04:39:03

Rejea za mada hii;

bottom of page