top of page

Mwandishi;

Mhariri:

Jaza jina na cheo cha mwandishi

Jumanne, 23 Machi 2021

Kiharusi cha mpito-Huduma ya kwanza
Kiharusi cha mpito-Huduma ya kwanza
Kiharusi cha mpito-Huduma ya kwanza
Kiharusi cha mpito-Huduma ya kwanza

Kiharusi cha mpito-Huduma ya kwanza

Kiharusi cha mpito kwa lugha tiba huitwa transient ischemic attack, ni kiharusi kinachotokea kwa muda mfupi kisha kupotea. Dalili za kiharusi cha mpito hufanana na dalili za kiharusi cha kawaida, ingawa dalili zake hupotea ndani ya masaa 24. Mtu mwenye kiharusi cha mpito huwa na hatari kubwa ya kupata kiharusi cha kudumu kwa wakati mwingine hivyo anabidi kutibiwa ipasavyo na kufuata ushauri wa kitiba wa namna ya kujuzuia kwenye hatari ya kiharusi hapo baadae.


Huduma ya kwanza kwa mgonjwa mwenye kiharusi cha mpito ni sawa na huduma ya kwanza kwa mgonjwa mwenye kiharusi cha kawaida. Huduma hiyo huhusisha


Dalili za kiharusi cha mpito


Kiharusi cha mpito huonyesha dalili zinazofanana na kiharusi cha kudumu isipokuwa dalili zake hudumu chini ya masaa 24 tu. Dalili hizo zinaweza kuwa;


 • Kuanguka kwa uso upande mmoja

 • Kupooza upande mmoja wa mwili

 • Kuongea kama mlevi

 • Kupoteza uono ghafla

 • Kizunguzungu

 • Kupungua kiwango cha kuweza kujitambua

 • Kupata kifafa

 • Kuona vitu vinazunguka(mgonjwa)

 • Kushindwa kutembea


Unamtambuzi wa mhanga wa kiharusi cha mpito?


Unaweza kumtambua mhanga wa kiharusi kwa kufanya mambo yafuatayo pia;


 • Je uso wa mgonjwa umeanguka au kuonyesha haupo sawa upande wa kushoto na kulia? Fanya hivyo kwa kumwambia atabasamu

 • Je anaweza inua mikono yote miwili bila mmoja kuanguka?

 • Je ana mabadiliko kwenye kutamka maneno au anaongea kama mlevi?


Huduma ya kwanza kwa mtu mwenye kiharusi cha mpito

Kama unahisi mgonjwa wako ana kiharusi, fanya mambo yafuatayo haraka


 • Piga simu za huduma ya dharura haraka iwezekanavyo

 • Muweke mhanga kwenye pozi la uhuru

 • Endapo amepoteza fahamu na mapigo ya moyo hayasikiki, mfanyie CPR(jifunze namna ya kufanya CPR kwenye Makala zingine za ULY CLINIC)

 • Andika muda wa dalili za kiharusi kuonekana na dalili zilizotokea ili kumfahamisha kiongozi wa huduma za dharura atakapofika

 • Mpe tumaini mgonjwa na pima viashiria uhai mpaka timu ya dharura itakapofika

 • Usimpe mhanga chochote cha kula au kunywa kwani utaongeza hatari ya kupaliwa na hivyo kumsababishia matatizo zaidi

 • Usimpatie mgonjwa aspirini au dawa zingine za kuyeyuesha damu kwani hii itapalekea damu kuvia zaidi kwenye ubongo endapo kiharusi ni kutokana na kuvia kwa damu

 • Legeza mavazi au vitu vinavyobana mhanga

 • Kama anahisi baridi mfunike na blanketi

 • Angalia kama nnjia ya hewa haina kitu, kama vile chakula au matapishi yanayoweza kuzuia upumuaji wake. Kama vipo unaweza kutoa kwa kufuata utaratibu ilioandikwa sehemu nyingine katika tovuti hii ya ULY CLINIC


Kwanini kukumbuka muda dalili zilipotokea?


Matibabu ya kiharusi hutegemea muda tangu ilipotokea, endapo muda ni chini ya masaa 4 na nusu, mgonjwa anaweza faidika kupata matibabu kwa dawa endapo kiharusi chake kinasababishwa na kuziba kwa mishipa ya damu. Hata yule mwenye kiharusi kutokana na kupasuka kwa mshipa wa damu anaweza kupata huduma ya dharura ya upasuaji. Kupata huduma za dharura za dawa au upasuaji huzuia sehemu kubwa ya ubongo kuathirika na hivyo kuondoa au kupunguza athari inayoweza kutokea kutokana na kiharusi


ULY CLINIC inakukumbusha siku zote uwasiliane na daktari wako kwa elimu na ushauri zaidi kabla ya kuchukua thatua yoyote baada ya kusoma makala hii

Wasiliana na daktari wa ULY CLINIC kwa suhauri zaidi kupitia namba za simu au kwa kubonyeza 'Pata tiba'  chini ya tovuti hii

Imeboreshwa,

1 Oktoba 2021 08:12:13

Rejea za mada:

Penn medicine. If Someone is Having a Stroke: 3 Things To Do and 3 Things Not To Do. https://www.pennmedicine.org/updates/blogs/neuroscience-blog/2019/april/if-someone-is-having-a-stroke-3-things-to-do-and-3-things-not-to-do. Imechukuliwa 23.03.2021 2. Elite medica centre. FIRST AID FOR STROKE. https://elitelv.com/doctors-corner/first-aid-for-stroke/. Imechukuliwa 23.03.2021 3. “Stroke Facts.” Centers for Disease Control and Prevention, Centers for Disease Control and Prevention. www.cdc.gov/stroke/facts.htm. Imechukuliwa 23.03.2021 4. Stroke: First Aid.” Mayo Clinic, Mayo Foundation for Medical Education and Research. www.mayoclinic.org/first-aid/first-aid-stroke/basics/art-20056602. Imechukuliwa 23.03.2021 5. “About Stroke.” www.stroke.org, www.stroke.org/en/about-stroke. Imechukuliwa 23.03.2021 6. René Handschu , et al. First aid in acute stroke. Introducing a concept of first action to laypersons. https://www.ncbi.nlm.nih.gov/pmc/articles/PMC1705488/. Imechukuliwa 23.03.2021 7. Jen Heng Pek, et al. Guidelines for Bystander First Aid 2016. https://www.ncbi.nlm.nih.gov/pmc/articles/PMC5523093/. Imechukuliwa 23.03.2021 8. Pathophysiology and Treatment of Stroke. https://www.mdpi.com/1422-0067/21/20/7609/pdf. Imechukuliwa 23.03.2021

bottom of page