top of page

Mwandishi:

Imeboreshwa:

ULY CLINIC

3 Aprili 2026, 03:03:54

7/7  humaanisha nini katika cheti cha dawa?

7/7 humaanisha nini katika cheti cha dawa?

7/7 katika tiba humaanisha siku 7 katika wiki

Kama umeandikiwa dozi ya dawa na ikawekwa 7/7 inamaanisha dawa hiyo itumike kwa muda wa siku 7.


Vifupisho vingine vinavyoashiria kwa muda wa siku saba za wiki

Idadi ya kutumia dawa katika wiki inaweza kuandikwa kwa namba ya siku dawa inapotakiwa kutumika chini ya 7. Mfano

  • 1/7 humaanisha dawa inatumika siku 1 au dozi ya siku 1

  • 2/7 humaanisha dawa itumike kwa muda wa siku 2 au dozi ya siku 2

  • 3/7 humaanisha dawa itumike kwa siku 3 au dozi ya siku 3

  • 4/7 humaanisha dawa itumike kwa siku 4 au dozi ya siku nne

  • 6/7 humaanisha dawa itumike kwa siku 6 au dozi ya siku 6

Imeandikwa:

3 Aprili 2026, 03:03:30

bottom of page