Mafunzo kwa wataalamu na wagonjwa
Jifunze kupitia programu zinazotoa mafunzo ya afya kwa njia rahisi na ya kisasa na kiswahili, huku akili unde ikitoa usaidizi unaodhibitiwa na misingi ya programu ili kuongeza uelewa wa matibabu, mawasiliano ya afya, na elimu kwa wagonjwa. Baada ya kukamilisha mafunzo, washiriki hupata cheti cha ushiriki.
Jifunze namna sahihi ya kumlea mtoto katika hatua muhimu za ukuaji, ikiwemo usafi, chanjo, unyonyeshaji, ufuatiliaji wa afya, na namna ya kutambua dalili za hatari mapema ili kuhakikisha mtoto anakua salama na mwenye afya njema. Bofya hapa kuanza programu.
.jpg)
Programu hii inatoa elimu kuhusu umuhimu wa kula matunda na mboga za majani kwa afya bora, namna ya kuchagua vyakula vyenye virutubisho muhimu, na jinsi ya kujenga mtindo bora wa lishe kwa ajili ya kinga ya mwili na ustawi wa afya. Bofya hapa kuanza mafunzo.

Jifunze namna ya kuandaa lishe bora na yenye virutubisho kwa mtoto kulingana na umri wake, ikiwemo uchaguzi wa vyakula sahihi, ratiba ya mlo, na mbinu za kuhakikisha mtoto anapata ukuaji na maendeleo mazuri kiafya. Bofya hapa kujifunza.
.jpg)
Programu hii huwasaidia wataalamu wa afya kuboresha ujuzi wa kuchukua historia ya mgonjwa kwa usahihi, kuuliza maswali muhimu ya kitabibu, na kujenga mawasiliano bora na mgonjwa ili kusaidia kufanya tathmini na maamuzi sahihi ya matibabu. Bofya kuanza mafunzo.
.jpg)
Programu hii inalenga kuongeza uwezo wa wataalamu wa afya katika kutambua magonjwa, kufanya uchambuzi wa dalili, na kuchagua hatua sahihi za matibabu kupitia mafunzo ya vitendo na mifano halisi ya kitabibu. Bofya kuanza mafunzo.
.jpg)
Tumia msaidizi Uly Clinic AU kupata majibu ya maswali ya kiafya na ushauri kwa wagonjwa kwa urahisi zaidi. Bofya kiboksi chenye ishara ya meseji kilichopo chini ya tovuti hii kuanza mazungumzo na kupata msaada wa taarifa za afya wakati wowote. Kama unatumia Kompyuta bofya kitufe cha meseji kushoto mwa tovuti hii kutumia huduma.

