top of page
Vikokotoo vya Afya Vikokotoo vya Afya vya ULY Clinic vimeundwa kukusaidia kufanya maamuzi sahihi ya kiafya kwa kutumia taarifa sahihi, rahisi na za kitaalamu. Zana hizi hazichukui nafasi ya ushauri wa daktari, bali hukusaidia kuelewa hali yako kabla au baada ya kupata ushauri wa kitaalamu. Ili kutumia kikokotoo, bofya kichwa cha habari cha kikokotoo unachohitaji kisha kitafunguka na kukuelekeza namna ya kukitumia. ​ A. Vikokotoo vya Uzazi & Ujauzito Vikokotoo hivi vinahusiana na mzunguko wa hedhi, rutuba, ujauzito na maendeleo ya mtoto tumboni. ​ Mzunguko wa Hedhi Husaidia kufuatilia siku za hedhi, siku za rutuba na ovulesheni. ​ Siku ya Ovulesheni (Siku za hatari) Hukokotoa siku ya ovulesheni na siku hatarishi za kushika mimba. ​​ Kikokotoo cha siku ya Ovulesheni kwa kutumia mizunguko mbalimbali ya hedhi Kikokotoo hiki ni kizuri kwa wanawake ambao hawafahamu siku zao za mzunguko wa hedhi ni ngapi lakini wanakumbuka tarehe za kuingia hedhi zilizopita na ya sasa. ​​ Umri wa Mimba Hukokotoa wiki za ujauzito, kipindi cha sasa cha ujauzito na makadirio ya muda uliobakia. ​ Tarehe ya Kujifungua Hukadiria tarehe ya kujifungua (EDD) kulingana na tarehe ya mwisho ya hedhi. ​ Ukuaji wa Mtoto Tumboni Hutoa makadirio ya uzito, urefu na hatua ya maendeleo ya mtoto kwa wiki za ujauzito. ​ Siku salama na Hatari kwa ujauzito Huhesabu siku za hatari (Dirisha la rutuba), siku za kati, na siku salama za mzunguko wa hedhi ili kusaidia kupanga mimba au kuepuka ujauzito. ​ Idadi ya siku za mzunguko wa hedhi Kukokotoa urefu wa mzunguko wa hedhi ​​​​​ Shinikizo la damu kwa mjamzito Kikokotoo cha Shinikizo la Damu kwa Mama hukokotoa thamani ya shinikizo la damu kulingana na viwango vya juu (sistoliki) na vya chini (dayastoliki) vinavyoingizwa na mtumiaji. ​ Lini ushike mimba kujifungua siku yako Kikokotoo cha Tarehe ya Kushika Mimba hukusaidia kujua ni lini unapaswa kushika mimba ili kujifungua tarehe unayotaka, kulingana na mzunguko wako wa hedhi. ​ Utabiri wa jinsia ya mtoto Hiki ni kikokotoo cha makadirio kinachotumia dalili za mama pamoja na kalenda ya jinsia ya Kichina kubashiri uwezekano wa jinsia ya mtoto. ​ Siku ya kushiriki tendo kupata mtoto wa jinsia unayotamani Kikokotoo hiki kimeundwa kwa madhumuni ya elimu ya afya ya uzazi, kikilenga kusaidia wanandoa au watu wanaopanga kupata mtoto kuelewa siku za rutuba kulingana na mzunguko wa hedhi.​ ​Kikokotoo cha Kupona na MzungukoKikokotoo cha Kupona na Mzunguko ​ Kikokotoo cha siku za hatari na uwezekano wa kushika mimba baada ya kutoa mimba ​​Kikokotoo cha Kupona na Mzunguko Baada ya Kutoa Mimba hukusaidia kukadiria tarehe ya hedhi ya kwanza, kipindi ambacho unaweza kushika mimba tena na kufuatilia mchakato wa kupona baada ya kutoa mimba. Pia hutoa ushauri wa afya na lishe ili kukusaidia kujitunza na kutambua dalili zinazohitaji huduma za matibabu. ​ B. Uwezekano wa kushika mimba ​​ Uwezekano wa kushika mimba baada ya mimba kutoka/Kutolewa Kikokotoo hiki kinakadiria uwezekano wa kushika mimba baada ya kutoa mimba. ​ Uwezekano wa kushika mimba baada ya tendo la ndoa Kikokotoo hiki kinaweza kusaidia kukadiria uwezekano wa kushika mimba kulingana na tarehe ya kuanza kwa hedhi ya mwanamke, tarehe ya tendo la ndoa bila kinga, na urefu wa mzunguko wa hedhi. ​ C. Vikokotoo vya Vipimo & Uchunguzi Vikokotoo hivi vinasaidia kuelewa muda sahihi wa kufanya vipimo na tafsiri za awali za matokeo. ​​ Kipimo cha Mimba Hukokotoa muda sahihi wa kupima ujauzito (mkojo au damu) kulingana na mzunguko wa hedhi. ​ Kipimo cha Hatari ya kisukari Kikokotoo hiki hukusaidia kutathmini uwezekano wako wa kuwa na kisukari au kuwa kwenye hatari ya kupata ugonjwa huu. Hatari ya kisukari huongezeka kutokana na umri mkubwa, uzito kupita kiasi, shinikizo la damu, historia ya familia na kiwango cha mazoezi unayofanya. ​​​​ Kipimo cha mimba kwa mkojo baada ya Mimba kutoka/kutoa Kikokotoo hiki kimeandaliwa ili kukupa elimu na mwongozo wa jumla kuhusu muda unaohitajika kwa homoni ya ujauzito (hCG) kupungua baada ya kutoa mimba—iwe kwa dawa, kusafishwa, au mimba imetoka yenyewe. Kikokotoo hiki hakitoi jibu la moja kwa moja kama una mimba au huna mimba, bali kinaeleza kama muda uliopita unaweza kuathiri matokeo ya kipimo chako. ​ D. Vikokotoo vya Lishe & Mwili Vikokotoo hivi vitahusiana na afya ya mwili, uzito na lishe. ​ Kiasi cha chakula cha kula na mpango wa chakula wa siku-Kikokotoo Kikokotoo cha Lishe na Uchambuzi wa Mlo ni mfumo wa kisayansi unaokusaidia kufahamu mahitaji halisi ya mwili wako kila siku. Kikokotoo hiki kinatumia kanuni sahihi za kibayolojia kukokotoa kiwango cha kalori unachotakiwa kula kulingana na umri, jinsia, uzito, na malengo yako ya afya iwe ni kupunguza uzito, kuongeza misuli, au kudumisha afya yako. ​ Uwiano wa uzito kwa urefu(BMI) ​ Uzito Unaofaa ​ Kikokotoo cha Mahitaji ya Kalori kwa siku ​Kikokotoo cha kalori (nishati) ni zana rahisi na yenye manufaa inayokusaidia kujua takriban kiasi cha kalori unazohitaji kula kila siku kulingana na taarifa zako binafsi. Kipimo hiki kinazingatia umri, jinsia, uzito, urefu, kiwango cha shughuli za mwili, na lengo lako la afya kama kupunguza, kudumisha, au kuongeza uzito. ​ Uwiano wa uzito na urefu (BMI) na mlo wa wiki ​Huhesabu BMI (Uwiano wa uzito kwa urefu) ya mtu na kutoa mapendekezo ya mpango wa mlo wa wiki kulingana na matokeo. ​ E. Vikokotoo vya Afya ya Mwili Vikokotoo hivi vinahusiana na kazi za mwili kwa ujumla, maji, mkojo, na mapigo ya moyo. Kiwango cha Mapigo ya Moyo Hukokotoa mapigo ya moyo salama kulingana na umri na shughuli. Kiasi cha Maji ya Kunywa kwa Siku Hukokotoa kiasi kinachopendekezwa cha maji kwa siku (uzito, jinsia, hali ya hewa, shughuli). Idadi ya Kwenda Haja Ndogo kwa Siku Hutathmini idadi inayotarajiwa ya haja ndogo kulingana na unywaji wa maji na afya ya kibofu. Shinikizo la damu na ushauri wa chakula na mazoezi Kutathmini hali ya shinikizo la damu kulingana na vipimo vya systolic na diastolic, na kutoa miongozo ya lishe na mazoezi kusaidia kudhibiti BP. ​ F. Vikokotoo vya dawa kwa watoto Vinafanya kazi ya kukokotoa viwango sahihi vinavyohusiana na watoto. Dozi ya dawa kwa watoto Hukadiria dozi sahihi za dawa kulingana na uzito wa mtoto.​​​ ​ G: Vikokotoo vya dalili Vikokotoo hivi vinakupa ufahamu wa kufahamu visababishi au magonjwa yanayoweza kupelekea dalili mbalimbali katika mfumo husika. Majibu ni kwa ajili ya kielimu tu na hayachukui nafasi ya daktari. ​ Muwasho na kuungua kwenye mrija wa mkojo- Mwanamke ​ Muwasho na kuungua kwenye mrija wa mkojo- Mwanaume ​ Maumivu ya tumbo kwa mwanake ​ Maumivu ya tumbo kwa mwanaume
bottom of page
