Utaratibu wa kupata huduma zetu za Matibabu mtandaoni
Tafadhari soma hatua zote nne mpaka mwisho ili kupata uelewa wa kina wa namna huduma zetu zinavyotolewa kabla ya kujaza fomu yoyote.
1. Hatua ya kwanza: Kujaza Fomu ya Historia ya Tatizo
Mgonjwa anapaswa kwanza kujaza dodoso la tatizo lake la kiafya (historia ya ugonjwa). Kupitia fomu hii daktari hupata taarifa muhimu za historia ya tatizo lako inayohusiana na hali yako ya kiafya.
Fomu za matibabu mtandaoni zinapatikana kwa kubofya hapa
2. Hatua ya pili: Kukubaliana na SERA YA MATIBABU MTANDAONI
Kabla ya kuanza tiba, unatakiwa Kukubaliana na Sera yetu ya matibabu mtandaoni. Sera hii inasema kwamba:
-
Hutapewa majibu ya tatizo lako, kipimo cha kufanya, dawa au dozi kabla daktari hajafahamu hali yako ya kiafya.
-
Daktari lazima apate taarifa zako kupitia dodoso au majibu ya vipimo atakavyokuandikia.
-
Usalama na ubora wa tiba hutegemea taarifa sahihi utakazojaza.
Ikiwa unakubaliana na sera hii, unatakiwa kujibu maswali kweney dodoso na mengine utayoulizwa na daktari kwa usahihi na ufasaha.
3. Hatua ya tatu: Kuchangia huduma
Baada ya kujaza dodoso, utaelekezwa kwenda kwenye ukurasa wa kuchangia huduma. Kwenye kuraha hiyo utachagua aina ya huduma kulingana na mahitaji yako. Kurasa ya uchangiaji wa huduma inapatikana kwa kubofya hapa:
4. Hatua ya nne: Kutuma uthibitisho wa malipo
Baada ya kuchangia aina ya huduma, unatakiwa kutuma uthibitisho wa malipo kupitia kurasa ya kuchangia huduma.
Hii inamwezesha daktari kuendelea na hatua inayofuata ya uchunguzi na ushauri wa kitabibu.
5. Hatua ya tano: Kupokea huduma ya matibabu
Baada ya daktari kupokea:
-
Dodoso la historia ya tatizo
-
Uthibitisho wa malipo
Daktari atakuuliza maswali ya ziada kama itahitajika. Baada ya hapo, utapokea huduma unayostahili kulingana na shida yako. Huduma zetu zinatolewa kwa weledi na kwa kuzingatia viwango vya juu vya kitaalamu na taaluma.
Kwa nini tunafuata utaratibu huu wa matibabu?
Tunafuata utaratibu huu ili;
-
Kulinda afya yako kwa kutoa huduma sahihi na salama
-
Kuzuia makosa ya kitabibu
-
Kuhakikisha tunatoa huduma bora kwa taarifa kamili
-
Kufanya matibabu ya mtandaoni kuwa salama kama matibabu ya ana kwa ana.
Bofya hapa kwenda kwenye kurasa ya dodoso la matibabu mtandaoni kuanza kupata huduma.
Wapi utapata maelezo zaidi kuhusu matibabu mtandaoni?
Kuelewa zaidi kuhusu huduma za mtandaoni na mipaka yake, bofya hapa
Huduma maalumu: Siku ya matibabu bila malipo
Tunanaamini katika kusaidia jamii, hasa wale wasio na uwezo. Kwa hiyo tumeanzisha huduma maalumu:
Matibabu bila malipo kwa wateja wasio na uwezo
Kwa wagonjwa wanaopata huduma kwa mara ya kwanza na wenye baadhi ya matatizo ya afya, tunatoa matibabu bila gharama siku ya Jumamosi au siku nyingine kama itakayotangazwa kupitia kundi maalumu la whatsapp la ULYCLINIC:
Muda: Kuanzia saa 12 jioni (6:00 PM) – saa 4 usiku (10:00 PM).
Huduma hii ni;
-
Kwa wagonjwa wasio na uwezo wa kifedha
-
Kwa baadhi ya magonjwa tu (kulingana na mwongozo wa daktari)
-
Kwa wateja wapya wanaotibiwa kwa mara ya kwanza kupitia mfumo huu
