Mwandishi:
Mhariri:
Dkt. Sospeter M, MD
Dkt. Charles W, MD
9 Juni 2020 10:16:31
Kutunza miguu ya mgonjwa wa kisukari
Namna kisukari kinavyoathiri miguu
Watu wenye kisukari si rahisi kuhisi majeraha endapo yatatokea kwenye miguu kwa sababu ya kupungua kwa hisia, hivyo huwa hatarini kupata majeraha makubwa.
Kisukari huweza kusaabisha uharibufu katika mishipa ya fahamu kwa lugha nyingine uhalibifu huu hufahamika kama diabetic peripheral neuropathy, pia husababisha kupungua kwa mzunguko wa damu kwenye miguu na vikanyagio na hufahamika kwa pamoja magonjwa ya mishipa ya fahamu na mishipa ya damu kwenye miguu. Matokeo ya uharibifu huu ni kukosa hisia kwenye maeneo ya miguu dhidi ya majeraha kama malenge au kukatwa au kuchomwa na kitu. Kisukari pia hufanya majeraha haya kutopona haraka. Endapo maambukizi yatatokea kwenye majeraha haya na yasipotibiwa huweza kuleta madhara makubwa sana.
Namna ya kutunza miguu
Tiba kinga ni muhimu siku zote katika matibabu. Matunzo mazuri ya kila siku ya miguu huweza kukusaidia kuwa na miguu yenye afya njema;
Unda kikapu chako chenye vifaa kwa ajii ya utunzaji wa miguu yako, kinatakiwa kiwe na vitu vifuatavyo. Kikatio cha kucha, mafuta ya losheni na kioo kidogo cha kushika mkononi(Ukiwa na vitu vyako hivi basi fuata mambo yafuatayo kila siku
Osha miguu yako kwenye maji ya uvuguvugu (yasiwe ya moto), kwa kutumia sabuni isiyo kali, usiloweke miguu yako kwani huweza kusababisha miguu kukauka.
Kausha miguu yako kwa uangalifu, usisahau kukausha katikati ya vidole.
Tizama na chunguza miguu yako sehemu zote, kati ya kidole kimoja na kingine,ili kuhakikisha hakuna michaniko au jeraha au kucha ndefu, malenge n.k tumia kioo cha mkononi ili kuona kwenye kikanyagio au mwombe mtu mwingine akuangalie sehemu hizo kama unatatizo.
Osha vidonda au mikwaruzo kwa kutumia sababuni na maji, kisha funika kwa kitambaa kikavu na maalumu kwa ajiri ya ngozi.
Kata kucha zako vema, kwa kutumia kikata kucha, ni vema usitumie wembe kwani huweza kukata kucha vibaya pamoja na ngozi na kukusababishia kidonda. Usikate kucha kuwa fupi sana.
Paka mafuta ya losheni nzuri kwenye miguu na kikanyagio. Futa losheni ya ziada ambayo haijafyonzwa, usipake losheni kati ya kidole na kidole kwa sababu majimaji ya losheni yakizidi huweza kusababisha kutokea kwa maambukizi.
Vaa soksi safi na zinazokutosha vema kila siku, ikiwezekana vaa soksi nyeupe ili hata kama ukitobolewa au kukatwa na kitu soksi hiyo itavia damu, hivyo utajua mapema kuna shida imetokea.
Ushauri wa msingi
Mambo ya kufanya
Vaa viatu vinavyokupasa kuvaa, vinatakiwa vikutoshe vema, vyenye kisigino kifupi au visivyo na kisigino (ili kuzuia kuanguka) na visiwe vya kubana au kukufinya. Nunua viatu hivi kwenye maduka yenye wataalamu wa viatu au wasiliana na daktari wako wa kisukari ili akupe ushauri na mahali pa kupata viatu maalumu.
Nunua viatu wakati wa mchana- kwa sababu miguu yako huvimba kiasi wakati huo na utapata namba nzuri ya kiatu ambacho hakitakubana wakati miguu ikivimba kiasi.
Vaa soksi wakati wa usiku kama unahisi baridi miguuni
Nyanyua juu miguu yako unapokuwa umekaa kwenye kiti kwa mda mrefu
Chezesha vidole vyako na chezesha magoti na miguu huku na huko kwa dakika kadhaa mara nyingi mchana ili kusaidia mzunguko wa damu kwenye miguu na vikanyagio.
Fanya mazoezi kwa kuzingatia ratiba ili kuimarisha mzunguko wa damu.
Kagua miguu yako kila siku haswa angalia joto la ngozi kwa kushika mguu, na utofauti kati ya mguu mmoja na mwingine.
Marufuku
Kutumia madawa ya kujinunulia mwenyewe kwenye famasi ili kutibu maoteo ya vinyama kwenye miguu(wasiliana na daktari wako)
Kuvaa vitu vya kubana kwenye miguu, kama soksi za kubana sana au viatu vyenye kisigino kirefu
Kutembea miguu wazi(bila kuvaa viatu) hata kama ni ndani ya nyumba. Nunua viatu vya kutumia ndani tu na viwe na sifa ile kama ilivyotajwa kwenye mambo ya kufanya.
Kunawa na maji ya moto kwenye miguu au kuweka kitu cha moto kwenye miguu
Kuvuta sigara, kuvuta sigara hupunguza mzunguko wa damu na uwezo wa mwili kuponesha vidonda na huongeza kwa kiasi kikubwa hatari ya kukatwa viungo vya mwili(kama miguu)
Imeboreshwa
11 Desemba 2021 14:03:31
Uly clinic inakushauri siku zote uwasiliane na daktari wako kabla ya kuchukua hatua yoyote dhidi ya afya yako.
Wasiliana na daktari wa ULY clinic kwa kubonyeza 'Pata Tiba' au kwa kupiga namba za simu chini ya tovuti hii.
Rejea za mada hii;
-
Tessier D, Meneilly GS. Diabetes management in the elderly. In: Gerstein HC, ed. Evidence-based diabetes care. Hamilton: BC Decker Inc., 2001, pg. 370–9.
-
Lipska KJ, De Rekeneire N, Van Ness PH, et al. Identifying dysglycemic states in older adults: Implications of the emerging use of hemoglobin A1c. J Clin Endocrinol Metab 2010;95:5289–95.
-
Crandall J, Schade D, Ma Y, et al. The influence of age on the effects of lifestyle modification and metformin in prevention of diabetes. J Gerontol A Biol Sci Med Sci 2006;61:1075–81.
-
Chiasson JL, Josse RG, Gomis R, et al. Acarbose for prevention of type 2 diabetes mellitus: The STOP-NIDDM randomised trial. Lancet 2002;359:2072–7.
-
DREAM (Diabetes REduction Assessment with ramipril and rosiglitazone Medication) Trial Investigators, Gerstein HC, Yusuf S, et al. Effect of rosiglitazone on the frequency of diabetes in patients with impaired glucose tolerance or impaired fasting glucose: A randomised controlled trial. Lancet 2006;368:1096– 105.
-
Inzucchi SE, Viscoli CM, Young LH, et al. Pioglitazone prevents diabetes in patients with insulin resistance and cerebrovascular disease. Diabetes Care 2016;39:1684–92.
-
Kronsbein P, Jorgens V, Muhlhauser I, et al. Evaluation of a structured treatment and teaching programme on non-insulin-dependent diabetes. Lancet 1988;2:1407–11.
-
Wilson W, Pratt C. The impact of diabetes education and peer support upon weight and glycemic control of elderly persons with NonInsulin Dependent Diabetes Mellitus (NIDDM). Am J Public Health 1987;77:634–5.
-
Braun AK, Kubiak T, Kuntsche J, et al. SGS: A structured treatment and teaching programme for older patients with diabetes mellitus–a prospective randomised controlled multi-centre trial. Age Ageing 2009;38:390–6.
-
Fagan PJ, Schuster AB, Boyd C, et al. Chronic care improvement in primary care: Evaluation of an integrated pay-for-performance and practice-based care coordination program among elderly patients with diabetes. Health Serv Res 2010;45:1763–82.
-
McGovern MP, Williams DJ, Hannaford PC, et al. Introduction of a new incentive and target-based contract for family physicians in the UK: Good for older patients with diabetes but less good for women? Diabet Med 2008;25:1083–9.
-
Maar MA, Manitowabi D, Gzik D, et al. Serious complications for patients, care providers and policy makers: Tackling the structural violence of First Nations people living with diabetes in Canada. Int Indigenous Policy J 2011;21:http://ir.lib.uwo.ca/iipj/vol2/iss1/6. Article 6.Imechukuliwa 05.06.2020
-
Jacklin KM, Henderson RI, Green ME, et al. Health care experiences of Indigenous people living with type 2 diabetes in Canada. CMAJ 2017;189:E106– 12.
-
Chandler MJ, Lalonde C. Cultural continuity as a protective factor against suicide in First Nations Youth. Horizons 2008;10:68–72.
-
Oster RT, Grier A, Lightning R, Mayan MJ, Toth EL. Cultural continuity, traditional Indigenous language, and diabetes in Alberta First Nations: A mixed methods study. Int J Equity Health 2014;13:92. doi:10.1186/s12939-014- 0092-4.
-
Truth and Reconciliation Commission of Canada. Truth and reconcilliation commission of Canada: calls to action. Winnipeg, MB: Truth and Reconciliation Commission of Canada 2012. 2015. http://www.trc.ca/websites/ trcinstitution/File/2015/Findings/Calls_to_Action_English2.pdf.Imechukuliwa 05.06.2020
-
Yu CH, Zinman B. Type 2 diabetes and impaired glucose tolerance in aboriginal populations: A global perspective. Diabetes Res Clin Pract 2007;78:159– 70.
-
Gracey M, King M. Indigenous health part 1: Determinants and disease patterns. Lancet 2009;374:65–75.
-
Chronic Disease Surveillance and Monitoring Division, Centre for Chronic Disease Prevention and Control. Diabetes in Canada: Facts and figures from a public health perspective. Ottawa, ON: Public Health Agency of Canada, 2011 http://www.phac-aspc.gc.ca/cd-mc/publications/diabetes-diabete/facts -figures-faits-chiffres-2011/index-eng.php. Imechukuliwa 05.06.2020
-
Turin TC, Saad N, Jun M, et al. Lifetime risk of diabetes among first nations and non-first nations people. CMAJ 2016;188:1147–53.
-
Singer J, Putulik Kidlapik C, Martin B, et al. Food consumption, obesity and abnormal glycaemic control in a Canadian Inuit community. Clin Obes 2014;4:316– 23.