Mwandishi:
ULY CLINIC
Mhariri:
Dkt. Mangwella S, MD
3 Novemba 2021 09:51:21
Cefixime inatibu nini?
Cefixime ni antibayotiki kizazi cha tatu cha cephalosporin. Hutumika kutibu maradhi mbalimbali kutokana na bakteria jamii ya gramu chanya na hasi.
Vimelea wanaodhuriwa na cefixime
Staphylococcus aureus
Streptococcus pneumonia
Streptococcus pyogenes
Hemophilus influenza
Moraxella catarrhalis
Eschelician coli
Klebsiella
Proteus mirabilis
Salmonella
Shigella
Neisseria gonorrhoeae
Kumbuka, kutokana na matumizi ya dawa yasiyo sahihi pamoja na kubadilika kwa utu wa vimelea vya maradhi, cefixime inaweza isifanye kazi yake ya kuua baadhi ya vimelea viivyoorodheshwa hapo juu.
Cefixime inatibu nini?
Cefixime inatibu magonjwa yanayosababiswha na bakteria wanaodhuriwa na dawa hii. Baadhi ya magonjwa yanayotibiwa na Cefixime ambapo inapaswa kutumika yenyewe au ikiwa imechanganyika na dawa zingine ni;
Bronkaitiz
Gono
Otitis
Pharyngitis
Tonses
U.T.I
Wapi unapata maelezo zaidi kuhusu cefixime?
Pata maelezo zaidi kuhusu cefixime katika makala za dawa sehemu nyingine katika tovuti hii.
ULY CLINIC inakushauri uwasiliane na daktari wako kwa ushauri na tiba kabla ya kuchukua hatua yoyote ile baada ya kusoma majibu haya.
Kupata ushauri zaidi au tiba kutoka kwa daktari wa ULY CLINIC bofya hapa au tumia linki ya Pata tiba
Imeboreshwa,
3 Novemba 2021 10:27:52
Rejea za mada hii
Cefixime (Suprax) . https://www.medicinenet.com/cefixime/article.htm. Imechukuliwa 03/11/2021
Takahata S, et al: Amino acid substitutions in mosaic penicillin-binding protein 2 associated with reduced susceptibility to cefixime in clinical isolates of Neisseria gonorrhoeae. Antimicrob Agents Chemother. 2006 Nov;50(11):3638-45. Epub 2006 Aug 28.
Zhao S, et al. Genetics of chromosomally mediated intermediate resistance to ceftriaxone and cefixime in Neisseria gonorrhoeae. Antimicrob Agents Chemother. 2009 Sep;53(9):3744-51. doi: 10.1128/AAC.00304-09. Epub 2009 Jun 15.