top of page

Mwandishi:

ULY CLINIC

Mhariri:

28 Oktoba 2021 15:57:14

Je, vipele vidogodogo mgongoni huashiria UKIMWI?

Je, vipele vidogodogo mgongoni huashiria UKIMWI?


Hapana!


Ni mara chache sana kwa vipele vidododogo kwenye ngozi ikiwa pamoja na ngozi ya maeneo ya mgongo kutumika kama ishara ya maambukizi ya VVU. Vipele vidogo mgognoni huweza tokea kwa mtu mwenye au asiye na maambukizi.


Hata hivyo aina fulani ya vipele huwapata sana watu waishio na VVU au wenye kinga ya mwili dhaifu tu. Aina hizo zimezungumziwa kwenye makala ya Vipele vya UKIMWI.



Utambuzi wa VVU


Ili kuweza fahamu hali yako ya maambukizi ya VVU, ni vema ukafanya hivyo kwa kupima tu. Usiwe na hofu mara zote kuwa una VVU unapokuwa na vipele vidogo mwilini.


Soma zaidi kuhusu vipele mgongoni katika makala zingine za ULY CLINIC

ULY CLINIC inakushauri uwasiliane na daktari wako kwa ushauri na tiba kabla ya kuchukua hatua yoyote ile baada ya kusoma majibu haya.

Kupata ushauri zaidi au tiba kutoka kwa daktari wa ULY CLINIC bofya hapa au tumia linki ya Pata tiba

Imeboreshwa,

28 Oktoba 2021 16:57:24

Rejea za mada hii

  1. ULY CLINIC. Vipele mgongoni. https://www.ulyclinic.com/dalili-za-ugonjwa/Vipele-mgongoni. Imechukuliwa 28.10.2021

bottom of page