top of page

Mwandishi:

ULY CLINIC

Mhariri:

Dkt. Peter A, MD

21 Novemba 2021 15:47:32

Majira na hamu ya ngono

Je, vidonge vya majira yenye vichocheo viwili hubadili maono na hamu ya kufanya ngono kwa wanawake?

Kwa ujumla, hapana.


Baadhi ya wanawake wanaotumia majira yenye vichocheo viwili wameripoti malalamiko haya. Watumiaji wengi wa majira yenye vichocheo viwili hawajaripoti mabadiliko hayo, hata hivyo, baadhi yao wameripoti kuwa na ongezeko la hamu ya ngono kufuatia matumizi ya vidonge hivi.


je mabadiliko haya yanasababishwa na majira?


Ni vigumu kusema kama mabadiliko hayo yanatokana na vidonge vya majira yenye vichocheo viwili au sababu nyingine. tafiti moja imetoa mapendekezo ya kufanyika kwa tafiti zingine zaidi kuangalia kama kuna mahusiano ya moja kwa moja. (Anne R Davis, et al)


Kama una mabadiliko ufanyaje?


Kama una mabadiliko ya hamu ya ngono na hisia, ongea na mtoa huduma kupata msaada.

ULY CLINIC inakushauri uwasiliane na daktari wako kwa ushauri na tiba kabla ya kuchukua hatua yoyote ile baada ya kusoma majibu haya.

Kupata ushauri zaidi au tiba kutoka kwa daktari wa ULY CLINIC bofya hapa au tumia linki ya Pata tiba

Imeboreshwa,

21 Novemba 2021 15:47:32

Rejea za mada hii

  1. Davis AR, et al. Oral contraceptives and libido in women. Annu Rev Sex Res. 2004;15:297-320. PMID: 16913282.

bottom of page