Mwandishi:
WAMJW
Mhariri:
Dkt. Benjamin L, MD
9 Oktoba 2021 08:37:37
Je, kuvaa miwani ni sehemu ya njia ya kujikinga na Corona?
Miwani inaweza kukinga macho kukutwa na matonetone ya maji kutoka kwenye njia ya hewa ya mtu mwenye maambukizi ya virusi vya COVID-19 wakati wa kukohoa, hata hivyo njia za kujikinga na maambukizi ya covid-19 zinazoshauriwa sana ni;
Kuvaa barakoa
Kunawa mikono kwa majitiririka na sabuni
Kusafisha mikono kwa kutumia vitakasa mikono
Kuepuka misongamano
Kutumia chanjo
ULY CLINIC inakushauri uwasiliane na daktari wako kwa ushauri na tiba kabla ya kuchukua hatua yoyote ile baada ya kusoma majibu haya.
Kupata ushauri zaidi au tiba kutoka kwa daktari wa ULY CLINIC bofya hapa au tumia linki ya Pata tiba
Imeboreshwa,
9 Oktoba 2021 09:16:18
Rejea za mada hii
https://www.who.int/emergencies/diseases/novel-coronavirus-2019/question-and-answers-hub. Imechukuliwa 09.10/2021