Mwandishi:
ULY CLINIC
Mhariri:
Dkt. Mangwella S, MD
13 Novemba 2021, 16:47:12
Vimelea gani husababisha uume na uke kutoa usaha?
Kutokwa majimaji yasiyo ya kawaida kwenye uume au uke ni kutokwa na maji mithiri ya usaha au ya kuteleza kama mlenda kwenye mrija wa urethra kwa wanaume na kwenye shingo ya kizazi kwa wanawake licha ya kutokea mara chache. Maambukizi ya vimelea kwenye mrija wa mkojo au shingo ya kizazi huamsha mfumo wa kinga ya mwili unaodhibiti vimelea na hivyo kusababisha kutokea kwa michomo kinga kwenye njia hizo.
Vimelea wanaosababisha kutokwa na usaha sehemu za siri huambukizwa kwa njia kuu ya kujamiana au kugusa maji maji yenye vimelea hivyo.
Vimelea wanaosababisha kutokwa na usaha sehemu za siri wamegawanyika katika makundi mbalimbali ambayo ni vimelea wakuu, vimelea wengine na vimelea ambavyo bado havijathibitishwa.
Jinsia inayoonesha dalili zaidi
Usaha sehemu za siri huonekana sana kwa wanaume zaidi ya wanawake licha ya maambukizi kutokea kwenye jinsia zote kwa vijana na watu wazima wanaoshiriki ngono mara nyingi na isiyo salama.
Vimelea vikuu
Asilimia 40 ya usaha sehemu za siri husababishwa na vimelea wafuatao;
Chlamydia trachomatis
Neisseria gonorrhoeae
Kiasi kilichobaki husababishwa na
Mycoplasma genitalium
Trichomonas vaginalis
Herpes simplex virus
Adenovirus
Vimelea vingine
Vimela vingine ambavyo bado havijathibitishwa bado kusababisha tatizo la usaha kwenye uume na uke ni;
Mycoplasma hominis
Ureaplasma urealyticum
ULY CLINIC inakushauri uwasiliane na daktari wako kwa ushauri na tiba kabla ya kuchukua hatua yoyote ile baada ya kusoma majibu haya.
Kupata ushauri zaidi au tiba kutoka kwa daktari wa ULY CLINIC bofya hapa au tumia linki ya Pata tiba
Imeboreshwa,
13 Novemba 2021, 17:29:04
Rejea za mada hii
Chapter 3. Urethral Discharge. https://accessmedicine.mhmedical.com/content.aspx?bookid=369§ionid=39914779. Imechukuliwa 13.11.2021