
01
Kifungua kinywa
Asubuhi
Sharubati ya zabibu
Viambato:
Zabibu (hususani nyeusi au za rangi ya zambalau au nyekundu.)
Faida
Kila mililita 250 inayonywewa hutoa nishati ya kalori 174
Maganda yake huzuia saratani kutokana na kuwa na viinilishe muhimu
Katikati ya asubuhi na mchana
Sharubati ya mboga za majani izuiayo uvimbe uchungu
Viambato:
Brokoli
Rojo ya ufuta
Sharubati ya nanasi
Tufaa
Faida
Kila mililita 250 inayonywewa hutoa nishati ya karoli 139
Tafiti nyingi zimethibitisha uwezo wa brokoli na tufaa ya kuzuia saratani
Mpangilio wa mlo mbadala
Sharubati ya tufaa
Viambato:
Tufaa
Sharubati ya limau
Faida
Kila mililita 250 inayonywewa hutoa nishati ya kalori 123
Viinilishe vyake ni kinga dhidi ya saratani ya utumbo mpana
Katikati ya asubuhi na mchana
Sharubati ya zambarau
Viambato:
Kabichi nyekundu
Beri za bluu
Maziwa ya nazi
Sharubati ya limau
02
Mlo wa katikati ya mchana na jioni
Sharubati iongezayo nyongo
Viambato:
Spinachi
Kabichi au sukumawiki
Shamari
Sharubati ya nanasi
Mnanaa
Faida
Kila mililita 250 inayonywewa hutoa nishati ya kalori 97.
Huondoa sumu nyingi mwilini hivyo kudhibiti ongezeko la chembe za saratani.
03
Mlo wa alasiri
Sharubati isafishayo mwili
Viambato:
Karoti
Tufaa
Figili
Limau
Faida
Kila mililita 250 inayonywewa hutoa nishati ya kalori 130.
Huchochea usafishaji wa sumu mwilini,ambazo nyingi zaweza kuwa chanzo cha saratani.
04
Mlo wa jioni
Sharubati mchanganyiko
Viambato:
Sharubati ya nanasi
Maji ya glanadini
Sharubati ya chungwa
Faida
Kila mililita 250 inayonywewa hutoa nishati ya kalori 78.
Viinilishe vilivyomo katika matunda haya vinauwezo wa kuzuia saratani
Namna ya kuzuia saratani ya utumbo mkubwa
Maelezo muhimu ya kufahamu
Vinywaji hivi havitibu, bali hupunguza uwezekano wa kuugua saratani, sambamba na kuboresha tiba zingine.
Uwezo wa kuzuia saratani hupatikanao katika vyakula vya asili ya mimea umesha thibitishwa katika tafiti za watu katika maabara na epidemiolojia. Vyakula hivi vya kuzuia saratani hufanya kazi yake vinapoliwa katika mfumo wa vinywaji pia.
Waweza kukinga saratani ya utumbo mpana kwa;
Kupunguza au kuacha vyakula vya nyama hususani nyama za kopo na zilizo
Kaushwa kwa chumvi (kama soseji,na minofu ya nyama).nyama za aina hii
Huwa na sumu isababishayo saratani.
Achana na unywaji wa pombe maana pombe inaonekana kuwa chanzo cha
Saratani aina nyingi zishambuliazo mfumo wa mmeng᾽enyo wa chakula.
Ongeza ulaji wa nyuzi lishe kwa kula mkate wa ngano isiyokobolewaa nafaka isiyo kobolewa.
Epuka hali ya kupata choo ngum
Uwe a ratiba ya mazoezi na uizingatie
FAIDA ZA SHARUBATI KATIKA KUZUI SARATANI
Sharubati na vinywaji vingine vijengavyo afya vinafaida kubwa ukilinganisha na vyakula vigumu:
Ulaji wake ni rahisi
Huwezesha mwili kupata sehemu kubwa ya viinilishe vizuiavyo saratani kwa mfano sio kila mtu anaweza kula karoti tano za ukubwa wa kati kwa kuzitafuna vizuri ilikupata viinilishe vingi vilivyo ndani yake.hata ivyo karibu kila mtu anaweza kunywa bilauri ya sharubati ya karoti.
Huwezesha ulaji wa vyakula vibichi na vilivyo chakatwa katika uasili wake hivyo huifadhi uwezo wake wakuponya mangojwa.kwa mfano ni rahisi kunywa sharubati ya brokoli mbichi pekee yake au kabichi nyekundu kuliko kula mbichi.
Vinywaji dhidi ya saratani
Kwa ujumla sharubati na rojorojo ni vya muhimu katika kuzuia saratani kwa sababu ya kuwa na viinilishe vinavyo zuia saratani.
Imeboreshwa;
27 Desemba 2021, 08:07:21
Rejea za mada hii:
Chang, et al. “Bromelain inhibits the ability of colorectal cancer cells to proliferate via activation of ROS production and autophagy.” PloS one vol. 14,1 e0210274. 18 Jan. 2019, doi:10.1371/journal.pone.0210274
Gerhauser C. Cancer chemopreventive potential of apples, apple juice, and apple components. Planta Med. 2008 Oct;74(13):1608-24. doi: 10.1055/s-0028-1088300. Epub 2008 Oct 14. PMID: 18855307.
Maeda N, et al. Anti-cancer effect of spinach glycoglycerolipids as angiogenesis inhibitors based on the selective inhibition of DNA polymerase activity. Mini Rev Med Chem. 2011 Jan;11(1):32-8. doi: 10.2174/138955711793564042. PMID: 21034405.
Zhou, et al. “Potential anticancer properties of grape antioxidants.” Journal of oncology vol. 2012 (2012): 803294. doi:10.1155/2012/803294.
Katiyar, et al. “Grape seeds: ripe for cancer chemoprevention.” Cancer prevention research (Philadelphia, Pa.) vol. 6,7 (2013): 617-21. doi:10.1158/1940-6207.CAPR-13-0193
