
01
Kifungua kinywa
Asubuhi
Rojorojo nzito
Viambato:
Zapote mamey na mbadala wake ni tikiti maji au embe
Maziwa ya nazi
Sharubati ya nanasi
Maji
Unga wa mdalasini
Faida
Kila mililita 250 za mchanganyiko huu huupa mwili nishati yenye kalori 314
Huupa mwili vitamin na mafuta muhimu kwa urembo wa ngozi
Kati ya asubuhi na mchana
Sharubati yangozi safi
Viambato:
Asufi
Karoti
Matango
Tufaa
Faida
Kila mililita 250 ya mchanganyiko huwa na nishati yenye kalori 92
Huondoa sumu zinazoumua na kuchakaza Ngozi
02
Mlo wa katikati ya mchana na jioni
Sharubati ya kulainisha Ngozi
Viambato:
Tango
Figili
Sharubati ya nanasi
Faida
Kila mililita 250 za sharubati ya mchanganyiko huu huupa mwili nishati yenye kalori 65
Huondoa uchafu katika ngozi na kuzuia uvimbe wa Ngozi
03
Mlo wa alasiri
Sharubati ya karoti
Viambato:
Karoti
Sharubati ya limau
Faida
Kila milimita 250 za sarubati huupa mwili nishati yenye kalori 98
Nichazo kizuri cha vitamin A muhimu katika kutunza ngozi na
04
Mlo wa jioni
Sharubati ya nanasi
Viambato:
Nanasi
Faida
Kila milimita 250 huupa mwili nguvu yenye kalori 133
Hupunguza uvimbe uchungu kwenye Ngozi
Husaidia kuondoa sumu mwilini na kwenye ngozi
Vinywaji vya kiafya husafisha ngozi kuanzia ndani mpaka nje ya Ngozi. Ngozi ya binadamu inayokisiwa kuwa na ukubwa wa wastani wa mita mbili za mraba, haifanyi kazi ya kukinga mwili na mazingira tu bali pia kuondoa uchafu mwilini. Kama ndani ni kuchafu ngozi hitakuwa na mwenekano mzuri kwa hiyo uzuri wa ngozi huanzia ndani kuja nje. Haisadii kutumia vipodozi vya gharama kama sehemu ya ngozi ya ndani imejaa sumu. Hivyo uboreshaji wa uzuri wa ngozi unapaswa kuanzia kwa tiba ya kuzimua sumu ndani ya mwili ili kupata uzuri wa Ngozi ya nje. Tumbaku ni moja ya vitu vinavyofanya ngozi ikunjamane mapema.
Kina nani wanafaa kutumia mlo huo juu
Mlo kwa ajili ya Ngozi inafaa kwa;
Watu wenye Ngozi chakavu
Watu wenye Ngozi kavu
Njia zingine za kuongeza urembo wa Ngozi
Fanya Ngozi yako iwe bora kwa;
Kuftumia tiba isafishayo mwili
Kulala muda wa kutosha
Kunywa maji ya kutosha
Kuepuka kupata choo kigumu
Kuepukana na sigara
Kuepuka kupigwa na miale mikali ya jua (jua la mchana)
Imeboreshwa;
27 Desemba 2021, 08:06:58
Rejea za mada hii:
Abbas, Sukaina et al. “Applications of bromelain from pineapple waste towards acne.” Saudi journal of biological sciences vol. 28,1 (2021): 1001-1009. doi:10.1016/j.sjbs.2020.11.032
Massimiliano R, et al. Role of bromelain in the treatment of patients with pityriasis lichenoides chronica. J Dermatolog Treat. 2007;18(4):219-22. doi: 10.1080/09546630701299147. PMID: 17671882.
Fam, V. et al. (2020). Prospective Evaluation of Mango Fruit Intake on Facial Wrinkles and Erythema in Postmenopausal Women: A Randomized Clinical Pilot Study. Nutrients, 12(11), 3381. https://doi.org/10.3390/nu12113381.
Sankararaman S, et al. Are We Going Nuts on Coconut Oil? Curr Nutr Rep. 2018 Sep;7(3):107-115. doi: 10.1007/s13668-018-0230-5. PMID: 29974400.
