top of page

ASPIRINI INAWEZA KUPUNGUZA KUPATA KIFAFA CHA MIMBA

Updated: Feb 11, 2019




Tafiti zimeonyesha kwamba kupata dozi ndogo ya aspirini mapema zaidi wakati wa ujauzito na madini ya kalisium  miezi mitatu ya kwanza kunaweza kusaidia kupunguza kupata kifafa cha mimba kwa wamama walio katika hatari ya kupata kifafa hicho.

Wanawake waliohatarini kupata kifafa cha mimba wanaweza kupunguza kupata kifafa cha mimba endapo watatumia dozi ndogo ya aspirini kabla ya wiki 16 za ujauzito na madini ya kalisium baada ya wiki 20 ya ujauzito, ripoti hii ilichapishwa na The Obstetrician & Gynaecologist Found.


Kifafa cha mimba kinatokea kwa asilimia 3 hadi 5 ya ujauzito zote na huchangia vifo vya wakinamama zaidi ya 50,000 Duniani kila mwaka.

Mama mwenye kifafa cha mimba huwa na muunganiko wa vitu vifuatavyo;

  • Shinikizo la damu la juu

  • Na kuwa na protini kwenye mkojo kama akifanya kipimo

Kifafa chamimba kinaweza kuleta madhara makubwa katika maisha ya mama kama

  • Kiharusi

  • degedege-huweza kusababisha kifo kwa mama na mtoto

  • organi mbalimbali mwilini kama Figo, Ini, kushiindwa kufanya kazi

  • Mtoto kushindwa kukua vyema akiwa tumboni

  • Mtoto kufia tumboni na

  • Kujifungua kabla ya wakati au mtoto njiti

Utafiti uliwachunguza wamama walio katika hatari ya kupata kifafa cha mimba (pre eclampsia) wakiwa katika miezi mitatu ya kwanza na mitatu ya pili wakati wa ujauzito na kuwapa dozi ndogo ya aspirini na madini ya kalisium. Kupata Dozi ndogo ya aspirin kabla ya kufikisha wiki 16 kulionekana kupunguza hatari ya kupata kifafa cha mimba na pia kupata madini ya kalisium yalionekana kupunguza  kutokea kwa kifafa cha mimba kwa wamama ambao walikuwa na upungufu wa madini hayo mwilini.

Uchunguzi huo wa wanawake katika wiki 11 ya ujauzito ulifanyika kwa vipimo vya kupima shinikizo la damu kwa kutumia kipimo cha biochemical marker na uterine Doppler assessment. Mtafiti aliona vipimo vingi vinahitajika ili kuchunguza  vihatarishi vya kupata kifafa cha mimba, Mama alichukuliwa historia na kufanyiwa vipimo vya biochemical na biophysical marker kwa kujiridhisha kwamba vipimo vikionyesha mama yupo hatarini ndipo  akawekwa katika dozi ndogo ya aspirin.


Wakati matibabu kwa sasa ya dozi ndogo ya aspirini yamewekwa  kwa wamama walio katika hatari ya kupata kifafa cha mimba tu, mbeleni inaweza kufanywa kuwa matibabu ya kuzuia kifafa cha mimba kutokana na matokeo mazuri ndani ya miezi mitatu ya kwanza ya ujauzito. Lakini utafiti zaidi unatakiwa kufanyika  ili kuona kama wamama ambao hawapo katika vihatarishi(low risk population) wanaweza kufaidika pia.

Si kila hospitali zinaweza kufanya vipimo hivi kama vya Doppler, sonograph na biochemical marker kwa sababu vipimo hivi vinaweza kuwa havipo au wataalamu wa kupima hawajui kuelezea matokeo ya vipimo hivyo, hili linaweza kurudishanyuma uchunguzi wa kinamama kwa baadhi ya hospitali na kushindwa kujua yupi anaweza kunufaika na utafiti huu katika nchi zinazoendelea

Ingia kwenye makala zetu

48 views0 comments

Recent Posts

See All

Comments


bottom of page