top of page

Dermatosis papulosa nigra |ULY CLINIC

Updated: Dec 31, 2020

Imeandikwa na madaktari wa ULY-Clinic


Utangulizi



Dermatosis Papulosa Nigra(DPN) ni hali ya ngozi kuwa na vipele vinavyoanza kama vipele vidogo vya rangi nyeusi vilivyoinuka kidogo sana kwenye usawa wa ngozi maeneo ya usoni na shingoni haswa maeneo ya kuzunguka jicho na hutokea kwa watu wenye rangi nyeusi(waafrika na waafrika waishio bara la Amerika). Vipele hivi vinaweza kutokea pia kwenye kifua na nyuma ya mgongo. Watu wengi wamekuwa wakiviita kwa jina la sunzua, hata hivyo huwa havifanani na sunzua(warts) kwa tabia na kisababishi.


Asilimia 50 ya watu watu weusi huwa natatizo hili na wanawake huathirika mara mbili zaidi kuliko wanauume.



Kisababishi


Kisababishi cha vipele hivi hakifahamiki. Kuna ushahidi wa kitaalamu kwamba hili tatizo huwapata watu weusi na huonekana kwa wanafamilia wa koo moja. Vidoti hivi vikichuguzwa huonekana kuwa si saratani na pia haviwezi kubadilika kuwa saratani


Vipele huwa sugu, jinsi mtu anavyokuwa na kuongezeka umri na vyenyewe huongezeka idadi na ukubwa


Vihatarishi vya kupata tatizo hili


Kuwa na ndugu wa damu kama mama au baba au mdogo wako mwenye tatizo hili


Hatima ya vidoti hivi

Vipele hivi huanza kwenye umri wa ujana, jinsi mtu anavyoongezeka umri vipele hivi huongezeka ukubwa na idadi. Vipele pia huongezeka sana kwa kina mama haswa wakati wa ujauzito.



Matibabu

Mpaka sasa bado hakuna matibabu halisi ya kuondoa vipele hivi kabisa

Kabla ya kugunduliwa kwa kifaa cha umeme kinachoweza kukausha vipele hivi vyeusi tatizo hili lilikuwa ni gumu kutibiwa, kwa sasa mtu anaweza kutibiwa na kurudisha mwonekano wake wa awali. Baadhi ya matibabu huweza kusababisha kuota kwa vipele vipya kwa kasi kubwa. Hata hivyo mtu baada ya kupata matibabu anaweza kuotwa na vipele sehemu zingine za mwili(uso au shingoni au mgongoni)


ULY CLINIC inakushauri siku zote uwasiliane na daktari wako kwa ushauri na tiba kabla ya kuchukua hatua yoyote ile baada ya kusoma makala hii.


Wasiliana na daktari wa ULY CLINIC kwa ushauri zaidi na tiba kwa kubofya 'Pata tiba' au kupiga namba za simu chini ya tovuti hii.



147 views0 comments

Recent Posts

See All
bottom of page