top of page

"Fahamu jinsi ya kujikinga na chunusi"

Updated: Jan 24, 2021


Badili mtindo wa maisha


Unaweza kuzuia au kudhibiti chunusi bila kutumia madawa pia kwa kifanya mambo haya yafuatayo;


Osha eneo lililoathirika, usitumie nguvu- mara mbili kwa siku kwa kutumia mikono yako na sabuni ya kawaida isiyo na malashi pamoja na maji ya uvuguvugu. Kama ukitokewa na chunusu kwenye maeneo ya nywele basi jaribu kutumia shampoo ya nywele kila siku.


Usitumie dawa kama za scrub, ku mask uso kwa sababu husababisha ngozi kuwasha na michomo. Kuosha mara kwa mara na ku srub huweza kuleta michomo ya ngozi na chunusi. Nyoa nywele taratibu bila kujikata kwenye eneo lililoathirika kwa chunusi ili kuzuia michomo na miwasho.


Usitumie dawa zinazokausha sana ngozi na kuleta magamba-tafuta dawa zenye kemikali ya benzoyl peroxide. Pia dawa zenye sulphur, resorcinol na salycyclic asidi huwa nzuri.


Dawa hizi zinaweza kuleta wekundu, ukavu wa ngozi na makovu ambayo huisha ndani ya miezi kdha ya kutumia dawa.


Zuia vikereketa ngozi-Zuia vitu au mafuta ya kunata, losheni na dawa za nywele-Tumia dawa zilizoandikwa water based au noncomedogenic yaani hazisababishi chunusi.


Chunga nini kinagusa ngozi yako- zuia nywele zisiguse ngozi yako, weka nywele zako ziwe safi na zisiguse uso, usiweke mikono au vitu kewnye uso wako kama kipokelea simu. Usitumie nguo za kubana, kofia na zuia haswa kama una tokwa na jasho. Jasho na mafuta huweza kuleta chunusi.


Usikamue au kupasua chunusi- kufanya hivui unaweza sababisha makovu na maambukizi kwenye chunusi na ngozi.



Kujikinga na chunusi


Osha eneo linalotokwa na chunusi mara mbili kwa siku- kufanya hivyo unaondoa mafuta na seli zilizokufa. Usioshe sana uso kwani huweza kuchangia kuleta chunusi. Tumia sabuni zisizo kali na nguvu unapoosha uso wako. Tumia dawa zisizo na mafuta kuosha uso wako.


Tumia krimu za kununua duka la dawa au mafuta ya kukausha ngozi na kuondoa mafuta yaliyozidi- dawa zenye kemikali ya benzoyl peroxide au sulphur na salycyclic asid hutumika na huleta matokeo mazuri.


Usitumie makeup yenye mafuta- kutumia makeup zenye mafuta husababisha kuziba kwa vitundu vya ngozi na kuleta chunusi.


Toa makeup kabla ya kulala-Unapoenda kulala hakikisha umeosha uso wako kwa maji safi ya sabuni. Unapoenda kulala na makeup, makeup hizi husababisha kuziba kwa vitundu vya ngozi na kusababisha chunusi.


Vaa nguo zisizobana mwili-Nguo za kubana husababisha jasho na huleta chunusi kwa kuleta miwasho ya ngozi. Zuia kutumia helmet za kubana, kofia za kubana, na vifaa vya michezo vya kubana mwili


Oga baada ya mazoezi- mafuta na jasho huondoka kwenye ngozj unapooga na husaidia kujikinga na chunusi


Zuia kugusa au kupasua chunusi- kwa kufanya hivi unasababisha kuamsha chunusi nyingi zaidi.


Ingia kwenye tovuti kujua kuhusu chunusi na matibabu kwa kubofya hapa

93 views0 comments

Recent Posts

See All

Comments


bottom of page