Virusi vya corona vipo duniani kote, kuna aina saba (7) ya virusi ambavyo wanasayansi wanavifahamu kuwa vina athiri binadamu na kuwafanya waugue.
Baadhi ya virusi hawa waligunduliwa zamani sana na wengine wamegunduliwa hivi karibuni. Virussi vya corona kwa wanaweza sababisha homa kiasi au homa kali sana.
Wapo Virusi wawili waliojulikana hivi karibuni kusababisha binadamu kuugua mara kwa mara ambaao ni kirusi aina ya SARS-CoV na kirusi cha MERS-CoV.
Mambo ya kufanya kuzuia maambukizi ni pamoja na
Kunawa mikono mara kwa mara
Kufunika midomo na pua unapopiga chafya au kukohoa
Kupika vema mayai na nyama
Kutokaa karibu na mtu ambaye ana dalili za kuumwa kifua kama vile kukohoa na kupiga chafya
Kutosafiri kwenda sehemu zenye maambukizi hayo mpaka kuhakikisha usalama kwanza
Usisahau kuwashirikisha watu uwapendao kupakua app ya ULY CLINIC
Karibu ULY CLINIC kwa tiba na ushauri.
Comments