top of page

Kunywa Pombe kwa kiasi chochote kile huleta madhara kwenye mwili wako

Updated: Nov 24, 2018


Kutokana na tafiti zilizofanyika nyuma kuhusu kiwango salama cha matumizi ya pombe kwa ajili ya afya ya binadamu kilionyesha kuwa mtu akitumia pombe kwa kiwango cha uniti 7 kwa wiki(mwanamke) na unit 14(kwa wiki) huwa ni kiwango salama na hakiwezi dhuru mwili wa binadamu. Tafiti hii imepingwa na tafiti mpya iliyofanywa na wanasayansi madaktari kuanzia mwaka 1990 mpaka 2016 na kutolewa katika mtandao wa sciecnedaily kuwa "matumizi ya pombe kwenye Kiasi chochote kile huambatana na madhara makubwa katika maisha na mwili wa ya binadamu." Tafiti hii imeonyesha kuwa takribani watu milion 3 duniani wamekufa mwaka 2016 kutokana na matumizi ya pombe. Tafiti hii pia imeonyesha ukubwa wa matumizi ya pombe katika nchi mbalimbali ukiangalia jinsia na nchi, ambapo tafiti hii imefanyika katika nchi 195 duniani. Denmark imekuwa inaongoza kwa matumizi ya pombe kwa asilimia 97.1 huku pakistani ikiwa na kiwango cha chini kabisa cha asilimia 0.9. Pia wanaume wameonekana kutumia pombe kwa wingi zaidi kwa asilimia 63 Unywaji wa pombe umeonekana kuhusiana/ kusababisha matatizo zaidi ya 23 ikiwa ni magonjwa ya kuambukizwa, magonjwa yasiyo ya kuambukizwa na majeruhi. Hali hizo ni

  • Magonjwa ya moyo- moyo kutopiga vema, kiharusi, shinikizo la juu la damu, ugonjwa wa misuli ya moyo, na ugonjwa wa moyo wa ishemia

  • Saratani: saratani ya ziwa/chuchu, ini, kimeleo, koo, midomo, pua, koo

  • Magonjwa yasiyo ya kuambukiza; kusinyaa kwa ini, kisukari, kifafa, Kuchomeka kwa pancreata, kasoro pombe,

  • Magonjwa ya kuambukizwa: Maambukizi ya mfumo wa chini wa upumuaji na kifua kikuu

  • Kujidhuru mwili kwa kukusudia au kuwadhuru wengine waliokuzunguka

  • Kudhurika kwa mwili bila kukusudia: Kupewa sumu, moto, joto na kushika vitu vya moto, kufiamaji, na madhara mengine yasiyo na kukusudia

  • Ajari za barabarani

Kutokana na madhara hayo, ni vema kuchukua tahadhari, au wasiliana na daktari wako endapo utahitaji ushauri zaidi. Kwa maswali au ushauri tuandikie kupitia email zetu zilizochini ya mtandao huu, au nenda sehemu ya mawasiliano hapo kulia kwako.

KARIBU ULYCLINIC kwa tiba na ushauri

24 views0 comments

Recent Posts

See All

Comments


bottom of page