Haipahaidrosis ni neno tiba linalomaanisha kutoa jasho kwa wingi kusiko kwa kawaida, kusikohusiana na mazoezi au joto kali. Jasho hili linaweza kutoka sehemu Fulani tu katika mwili au mwili mzima. Neno tiba hili limetokana na neno ‘hidrosis’ ambalo ni neno la kigiriki na kilatini lenye maana ya ‘kutoa jasho’
Mtu anaweza kutokwa na jasho jingi kiasi kwamba likaharibu ubora wa maisha yake, jasho linaweza kuchuruzika au kulowanisha sehemu ya nguo au nguo yote.
Dalili
Dalili huwa pamoja na;
Kutokwa na jasho kupita kiasi wakati wa mazoezi na kutembea
Kutokwa na jasho zaidi ya watu wengine wakati upo kwenye hali ya hewa ya joto
Jasho kutoka sehemu mbili zinazofanana mwilini mfano makwapa yote, viganja vya mikono, miguuni
Kutokwa na jasho maeneo ya usoni, kanyagio la miguu, viganja vya mikono, miguuni au mikononi
Visababishi
Kutokwa na jasho ni njia mojawapo inayotumiwa na mwili kupunguza joto mwilini. Mfumo wa neva huamsha tezi za jasho katika ngozi ili ziweze kuzalisha jasho kuitikia joto lililozidi ndani ya mwili. Kwa kawaida jasho hutoka kwenye maeneo ya viganja vya mikono endapo una wasiwasi uliopitiliza.
Visababishi vya haipahidrosis vipo katika makundi mawili
Kundi la awali
Husababishwa na mwitikio wa tezi jasho dhidi ya taarifa za kuzalisha jasho kutoka mfumo wa neva. Mfumo wa neva kama ilivyozungumzwa hapo awali huwa na kazi za kuamsha tezi kuzalisha jasho. Endapo mtu ana wasiwasi au msongo wa mawazo, jasho huzalishwa zaidi kuliko kawaida. Jasho mara nyingi hutoka sana kwenye maeneo ya viganja vya mikono/miguu au usoni, na siku zote haisababishwi na ugonjwa mwilini na huweza kuwa la kurithi kati ya familia na familia.
Haipahidrosis ya sekondari
Haipahidrosis ya sekondari husababishwa na hali au magonjwa mbalimbali ndani ya mwili kama vile;
Ugonjwa wa Kisukari
Ugonjwa wa Kifua kikuu
Magonjwa ya tezi ya thairoidi
Haipoglaisemia (Kushuka kwa kiwango cha sukari mwilini)
Komahedhi
Baadhi ya saratani
Mshituko wa moyo
Magonjwa ya mfumo wa neva
Maambukizi
Matumizi ya baadhi ya dawa kama madawa ya kulevya
Madhara
Kuwa na kihatarishi cha kupata Maambukizi ya ngozi
Kupata Msongo wa mawazo na kujitenga vitu Fulani katika jamii
Endelea kusoma kuhusu makala hii kwa kubonyeza hapa
Wasiliana na daktari wa uly clinic endapo una maswali au unahitaji ushauri. Piga namba za simu chini ya tovuti hii au bonyeza link iliyoandikwa pata tiba
Wasiliana na daktari wa ULY CLINIC endapo una maswali au unahitaji ushauri. Piga namba za simu chini ya tovuti hii au bonyeza link iliyoandikwa Pata tiba
Comments