top of page

Maoteo sehemu za siri

Updated: Jun 7, 2021


Maoteo sehemu za siri(genital warts) hufahamika kwa majina mengine kama chunjua au dutu ni aina mojawapo ya ugonjwa unaoambukizwa kwa zinaa na unaotokea kwa watu wengi. Nusu ya watu wanaojihusisha na ngono mara kwa mara haswa isiyo salama hupata maambukizi haya muda fulani katika maisha yao na wanawake huathiriwa zaidi.


Kama jina lilivyo chunjua hudhuru sehemu za siri. Maoteo haya huonekana kwenye maumbo tofauti, mfano chunjua ndogo huonekana kama mwinuko mdogo na mrefu au kuwa na umbo kama la ua lililosambaa. Kwa watu wengi huwa na umbo dogo sana kiasi cha kuonekana kwa shida.


Chunjua huweza kutokea sehemu yoyote ile ya mwili na kisabaishi cha tatizo hili ni maambukizi ya kirusi cha Human papilloma (HPV).


123 views0 comments

Recent Posts

See All

Comments


bottom of page