top of page

Kujikinga na meno kutoboka | ULY CLINIC

Updated: Jun 29, 2020

Imeandikwa na madaktari wa uly clinic


Utangulizi

Mashino kwenye jino husababishwa na kutoboka kwa sehemu ngumu ya jino, mashimo hayo yanaweza kusababishwa na mkusanyiko wa mambo mablimbali. Meno kuoza na kutoboka hutegemeana, yaani meno yakioza hupelekea kuwa rahisi kutoboka. Tatizo la meno kuwa na mashimo au kuoza husababishwa na kushambuliwa na bakteria waliopo ndani ya kinywa, kula vyakula vyenye sukari kwa wingi, na kutosafisha meno yako vema

Tatizo la meno kutoboka linajulikana duniani kote na hutokea sana kwa watoto, vijana wadogo na wazee. Hata hivyo ifahamike kwamba kila mtu anaweza kuoza meno na kutoboka ikiwa ni kichanga au mtu mzima.

Endapo tatizo la meno kuoza na kutoboka halijatibiwa mapema, matobo hayo huweza kwenda chini mpaka kufika kwenye mzizi wa jino na kuanza kuleta Matatizo ya meno kuuma na jino kulegea na kutoka.

Dalili za meno kuoza

 • Kupata maumivu ya jino bila kuwa na sababu ya msingi

 • Jino kuwa na hisia sana, mfano kuuma dhidi ya kula vitu aina kadhaa

 • Kupata maumivu makali unapokula kitu cha baridi, moto au chenye sukari

 • Meno kubadilika rangi, rangi ya ugoro, kuwa na michirizi mweupe

 • Kupata maumivu wakati wa kung’ata meno

Visababishi

Meno kuoza husababisha matobo kwenye meno, tukio hili si la ghafla bali hutumia muda kutokea, baadhi ya maelezo ya namna ya Matatizo ya meno kuoza yanavyotokea yameelezewa hapa chini;

Kula vyakula vyenye sukari na wanga kwa wingi

Vyakula hivi husababisha kufanyika kwa kuta nje ya jino ambayo huliwa na bakteria, jinsi bakteria wanavyovamia kuta hii na kuila hupelekea kutengenezwa kwa kuta ingine ngumu ambayo haiwezekani kutolewa na bakteria


Kuta iliyotengenezwa kuvamiwa

Kuta ngumu iliyotengenezwa hapo juu huwa na asili ya u tindikali(asid) hivyo huvamia mfupa wa jino nan a kuuozesha na kusababisha vitobo. Vitobo vinapofanyika, asidi hupita na kuingia kwenye vitobo hivyo na kusababisha vitobo viendelee chini zaidi kwenye mzizi wa jino ambako kuna mishipa ya fahamu na damu. Mtu kwa hatua hii huwa anapat amaumivumakali ya jino.


Uvamizi kuendelea

Endapo mtu asipopata matibabu mapambano dhidi ya bakteria na kuta zilizofanyika huendelea, asidi huendelea kuharibu mzizi wa jino na kuleta maumivu zaidi, matokeo yake huweza kusambaa hadi kwenye mfupa unaoshikilia jino na kufanya uharibifu huko


Madhara

 • Madhara mengi yanayoweza kujitokeza ni kama vile

 • Maumivu ya meno

 • Usaha kwenye meno

 • Kuvimba kwa fizi

 • Kuvunjika na kuharibika kwa meno

 • Matatizo ya kushindwa kutafuna

 • Kucheza kwa meno na kung’oka


Kama mashimo yakiendelea kwa muda mrefu Matatizo yanayoweza kutokea ni pamoja na

 • Maumivu makali yanayoharibu ubora wa maisha ya mtu

 • Kupoteza uzito kutokana na kushindwa kula

 • Kung’oka kwa meno

 • Kufanyika kwa usaha kwenye mzizi wa meno

Kujikinga


 • Osha meno yako na dawa ya meno yenye madini ya fluoride, angalau mara mbili kwa siku, au kila baad aya kula chakula

 • Suuza mdomo wako kwa maji yenye fluoride(yanawezaekana yakawa maji maalumu)

 • Mwone daktari mara kwa mara kwa uchunguzi endapo una Matatizo ya meno

 • Ziba meno yaliyo mazima kujikinga na meno kutoboka haswa kwa watoto walio kwenye umri wa kwenda shule

 • Kunywa maji ya bomba- maji haya huwa na fluoride ambayo hulinda meno

 • Usile mara kwa mara vyakula vyenye sukari kwa wingi na vinywaji vyenye sukari

 • Pata matibabu ya mara kwa mara ya madini ya fluoride kutoka kwa daktari wako ili kujikinga na kmeno kutoboka

 • Tumia dawa za kuua bakteria endapo una maambukizi kwenye meno

 • Tumia dawa asilia ambazo zinasemekana kuponya meno na kuzuia yasitoboke. Kumbuka unabidi utumia dawa zilizothibitishwa na kuwa hazina madhara.


Endapo una shida ya meno kutoboka wasiliana nasi kwa namba za simu zilizo chini ya mtandao huu kwa ushauri na tiba. Kusoma zaidi kuhusu vihatarishi bonyeza hapa

Toleo la 3

Imeboreshwa14/2/2019

658 views0 comments

Recent Posts

See All

Comments


bottom of page