top of page

Mguu kifundo-Talipes equine


Mguu kifundo ni tatizo ambalo mtoto anazaliwa nalo, mpaka sasa hakuna sababu za moja kwa moja zinazoweza kuelezeka kwamba ni nini kinacho sababisha tatizo hili moja kwa moja. Baadhi ya mambo yanayoonyesha kuambatana/kuwa kihatarishi cha tatizo hili ni kama vile matumizi ya dawa zenye madhara wakati wa ujauzito mfano sodium aminopterin na kuwa na maji kidogo kwenye chupa ya uzazi wakati wa ujauzito


Mguu kifundo hutokea kwa mtoto 1 kati ya watoto 1,000 wanaozaliwa na kutokea huku hutofautiana kati ya taifa moja na lingine. Watoto wa kiume wanahatari zaidi kupata mguu kifundo kuliko wakike, wanawake walio wahi kupata mtoto mwenye mguu kifundo wana asilimia 10% kupata mtoto mwingine mwenye tatizo hili.


Nini hutokea kuleta tatizo hili?

Kuna maelezo mengi yanayotolewa kuhusu tatizo hili yakiwa pamoja na, kushindwa kukua vema kwa mifupa mwororo( cartilage) ambayo hutengeneza maungio ya miguu na hitilafu katika utengenezaji wa mfumo wa fahamu wa mtoto.


Mtoto anaonekanaje akiwa na mguu kifundo?

Mtoto mwenye mguu kifundo anaweza kutambuliwa kabla hajazaliwa kwa kipimo cha ultrasound au anapozaliwa kwa kuwa miguu yao huonekana isiyo ya kawaida kama uonavyo katika picha hapo chini

Je tatizo hili linatibika?

Matibabu ya mguu kifundo yapo yanafanyika katika hospitali zenye vitengo vya mifupa, mtoto anatakiwa kuwahishwa hospitali mapema zaidi kabla ya mifupa mwororo kukomaa. Wiki 1 au 2 baada ya kujifungua mtoto akipelekwa hospitali anaweza kupewa viatu maalumu ambavyo vitamsaidia kulekebisha miguu yake na kuleta matokea mazuri

Watoto wanaocheleweshwa nyumbani , matibabu yao yanakua magumu naya muda mrefu pia


Kumbuka:Ukimwahisha mtoto hospitali atapata matibabu na kuwa na miguu mizuri, muwahishe mwanao sasa endapo amepata tatizo hili la mguu kifundo.

27 views0 comments

Recent Posts

See All

Comments


bottom of page