Saratani ya Kaposi (Kaposi's sarcoma, KS) ilielezewa kwa mara ya kwanza mwaka 1872 na mtaalamu wa ngozi wa Hungarian anayeitwa, Moritz Kaposi. Saratani hii huathiri katika chembe hai za ukuta wa ndani wa mishipa ya damu. Saratani ya kaposis huwa na hatua tofauti kuanzia kwenye ngozi mpaka kuhusisha viungo vya ndani ya mwili. Dalili za awali za saratani ya Kaposis sarcoma ni muonekano wa mabaka mekundu au zambarau juu ya ngozi. kisha mabaka haya hukua na kutengeneza vimbe kama vinundu. Inaweza kuleta uharibifu kuanzia kwenye ngozi laini ya midomo na viungo vya ndani ya mwili. Saratani hii imegawanywa katika makundi 4 ambayo ni
Inayohusiana na ugonjwa wa UKIMWI
Inayohusiana na kushuka kwa kinga ya mwili
Classic au sproadic
Inayohusiana na Waafrika
Saratani ya kaosisi inayohusiana na ugonjwa wa UKIMWI, ukilinganisha na aina zingine huwa na madhara ya haraka na mabaya. Saratani aina hii inayohusiana na ugonjwa wa UKIMWI hutokea mara nyingi ukilinganisha na zingine kusoma zaidi ingia kwenye linki hii
Comentarios