Shingo ya kizazi ni njia inayounganisha uke na mfuko wa kizazi. Ni kiungo chenye aina mbili za seli inayotokana na makutano ya seli za mfuko wa kizazi na uke. Seli hizo ni seli columnar kutokea kwenye uke na selli za squamous kutokea kwenye uke. Sehemu ya ambako muunganiko hutokea huitwa makutano ya squamocolumnar hii ni sehemu yenye hatarishi ya kupata saratani.Saratani ya shingo ya kizazi ni saratani inayojitikeza katika shingo ya kizazi na kusambaa ndani na nje ya kizazi. Ni moja ya saratani inayoathiri wanawake kwa kiwango kukubwa. Ni ya tatu kati ya saratani inayotokea kwa wanawake hapa duniani. Saratani Hii ni hutokana na ukuaji usio wa kawaida wa chembe hai katika sehemu hiyo ya makutano ya seli aina mbili, selli hizi zilizokuwa saratani husambaa na kushambulia maeneo mengine ya karibu na shingo ya kizazi.
Aina za saratani ya shingo ya kizazi
Aina za saratani ya shingo ya kizazi ni saratani ya seli za Squamous ambayo inatokea kwa asilimia kubwa, aina nyingine ni saratani ya Adenocarcinama. Visababishi:
Kuna virusi aina ya HPV(Human pappiloma virus), kwa asilimia 99.7 ukiwa una maambukizi ya virusi hawa unakuwa katika ki hatarishi cha kupata saratani ya shingo ya kizazi. Kirusi huyu wa HPV huambukizwa kwa kufanya ngono isiyo salama. Kila mwanamke ana hatarishi ya kupata maambukizi ya virusi vya pappiloma kwa asilimia 30 hadi 80, vifwatavyo ni vihatarishi vya kupata kirusi huyu
Kuanza ngono katika umri mdogo .
Kuwa na wapenzi wengi.
Magonjwa ya zinaa.
Uvitaji wa sigara.
Maambukizi ya ukimwi na magonjwa yanayoshusha kinga ya mwili.
Kurithi(kuwa na historia ya mama au dada kuwa na saratani ya shingo ya kizazi).
Dalili za saratani ya shingo ya kizazi: Katika hatua ya mwanzo wa tatizo hili huwa hakuna dalili zozote, baada ya muda mrefu baadae (miaka kumi au zaidi) mwanamke anakuwa na dalili zifuatazo; Kutoka damu ukeni bila mpangilio wa kawaida baada ya hedhi kukoma hedhi),Kutoka damu ukeni baada ya kutoka hedhi,Kuwa na maumivu wakati wa tendo la ndoa,kutoka majimaji ukeni yenye harufu mbaya bila muwasho wowote.Ikichelewa kugundulika tatizo husambaa sehemu mbalimbali za mwili(tumboni,mifupa, mapafu) Vipimo :
Kuna vipimo vinaweza fanyika kugundua tatizo navyo ni Ultrasound ya tumbo, Pap smear na VIA(Chembe za uke huwekwa kwenye kemikali asud ya acetic kasha huchunguliwa kwenye hadubini) VIA ni aina ya kipimo kinachofanyika zaidi ya Pap smear kwa nchi nyingi masikini kwa sababu ni rahisi na gharama yake ni ndogo. Matibabu kwa hatua za mwanzo (CIN1-CIN2) wa saratani ya kizazi Inatibiwa kwa njia ya Kugandisha selli zilizoathirika na saratani, Kugandisha seli zilizoathirika na saratani ni moja ya njia pekee ya matibabu ya saratani ya shingo ya kizazi katika hatua za mwanzo kabisa. Inatumika mara baada ya kufanya kipimo cha VIA tatizo likigundulika mwanamke anaweza tibiwa.Kwa asilimia 91-100% inasaidia kutibu tatizo.Matibabu haya hutumia hewa mchanganyiko wa CO2, NO na Nitrogen . Baada ya kipimo cha VIAi) Mwanamke atawekewa kifaa kinachogandisha seli katika shingo ya kizazi na Kugandisha kwa muda wa dakika 3, ii)baada ya hapo chembe hizo huyeyushwa kwa dakika 5 iii) Unagandisha tena kwa dakika 3. Iv) baada ya kufanya hivyo utapata ushauri wa kurudi lini na nini cha kufanya baada ya matibabu. Kusoma zaidi bonyeza hapa
Commentaires