Komamanga
Imeandikwa na madaktari lishe wa ulyclinic
Komamanga huwa na virutubisho vingi sana kama vile
Nyuzinyuzi, Protini, Vitamin C, Vitamin K,Madini ya Folate, Potassium
Pia kuna kemikali aina mbalimbali kama punicalagins ambayo husaidia kuzuia magonjwa ya michomo ya chembechembe hai za mwili(antinflammatory) na magonjwa ya mwili kujishambulia wenyewe(autoimmune) ambayo huongoza kwa vifo kama vile Magonjwa ya moyo, kisukari aina ya 2, ugonjwa wa alzheimer. Hata hivyo unene pia unaweza kuzuia kwa kutumia tunda hili
Kuzuia saratani ya tezi dume
Tafiti zinaonyesha juishi ya komamanga huweza kuzuia kiwango cha kemikali ya PSA ambayo hutolewa na tezi dume kwa. Kemikali hii ikiwa inapozalishwa kwa wingi huweza kuishia chembe za tezi kuwa saratani. Kiwango cha PSA kikijiongeza mara mbili zaidi kwa mtu mwenye saratani hatari yake ya kufa huongezeka mara dufu zaidi
Katika tafiti zinaonyesha kwamba juisi ya komamanga kiasi cha Mililita 250 kwa siku ina uwezo wa kurudisha nyuma kujizalisha kwa kemikali hii mara mbili badala ya miezi 15 na kuwa miezi 54
Pia tunda hili linauwezo wa kuuza chembe zenye sifa ya saratani(apoptosis)
Kupunguza shinikizo la damu
Matumizi ya mililita 150 ya juisi ya komamanga kwa siku kwa mda wa wiki mbili imeonyesha kupunguza shinikizo la damu.
Kushusha Shinikizo la damu la juu
Comments