top of page
Writer's pictureDr.Sospeter Mangwella, MD

Matumizi ya pombe kama kinga | ULY CLINIC

Updated: Jun 29, 2020

Ukweli kuhusu waini nyekundi na kukukinga dhidi ya magonjwa ya moyo.



Kunywa waini nyekundu kwa kiasi imekuwa ikifikiriwa kuwa na umuhimu kwenye afya ya moyo.


Pombe na aina fulani ya kemikali zilizo kwenye waini nyekundu zinazoitwa antioxidanti husaidia kukukinga dhidi ya magonjwa ya mishipa ya moyo ya koronari. Magonjwa ya mishipa hii huweza kupelekea mtu kupata mshituko wa moyo na kifo cha ghafla.



Uhusiano kati ya waini nyekundu na kupunguza mshituko wa moyo bado haujajulikana vema kutokana na tafiti chache kufanyika.


Hata hivyo faida mojawapo inajulikana kuwa antioksidant zilizo kwenye wine nyekundu huweza kuongeza kiwango cha kolestro aina ya HDL, ambayo hufanya kazi ya kuosha damu kwa kuondoa kiwango cha kolestro aina ya LDL. Kolestro ya LDL ikiwa kwa kwiango kikubwa mwilini hupelekea kupungua kwa kipenyo cha mishipa ya damu ya koronari(mishipa inayolisha moyo) kutokana na kuganda kwa Mafuta kwenye mishipa hiyo, na hata kuziba kwa mishipa hiyo.

Mishipa ya damu inapoziba au endapo Mafuta yaliyoganda yakajichomoa kutoka kwenye kuta za mishipa ya damu, husafiri kwenye mzunguko wa damu hivyo kusababisha kuziba kwa mishipa ya damu midogo ya koronari (hivyo kupelekea mshituko wa moyo) au kuziba kwa mishipa midogo ya ubongo (na kupelekea kiharusi-stroku)


Hata hivyo, waini nyekundu huwa na kemikali inayoitwa polyphenol aina ya resveratrol ambayo hulinda kuta za ndani za mishipa ya damu kwa kupunguza kiwango cha LDL


Kemikali ya resveratrol hupatikana kwenye vyakula gani?


Resveratrol hupatikana kwenye kwenye badhi ya mimea na matunda. Kemikali hii huzalisha na mimea wakati wa hatari, kama vile wakati mmea umevamiwa na vimelea vya bakteria au fangasi ili kupambana na adui hao.


Matunda yenye kemikali hii ni kama vile zabibu na matunda yanayofanana na zabibu, forosadi na matunda yanayofanana na forosadi na karanga.


Ni kiwango gani cha pombe unatakiwa kunywa?


Kiwango cha pombe unachotakiwa kunywa kitaalamu inategemea jinsia yako. Soma Zaidi mada hii kwenye mada ya pombe na afya ya mwili wako kwenye tovuti hii.


Kumbuka


Tafiti kubwa zaidi zinahitaji kufanyika ili kujua mahusiano kati ya pombe na dhidi ya kuzuia magonjwa ya moyo, hii ni kutokana na baadhi ya majibu ya tafiti zilizofanyika kupingana.


Wasiliana na daktari wako endapo unahitaji ushauri zaidi kuhusu pombe na afya ya mwili wako.


Wasiliana na daktari wa uly clinic kwa maswali na majibu zaidi kupitia forum au namba za simu chini ya tovuti hii.

88 views0 comments

Recent Posts

See All

Comments


bottom of page