top of page

Utapiamlo hupunguza uwezo wa kiakili


Utapiamlo ni hali inayotokana na utumiaji wa lishe yenye virutubisho ambavyo havitoshi au lishe iliyozidi, inayopelekea athari kwa afya ya mtoto. Tatizo hili husababisha athari katika ukuaji wa mwili na akili ya mtoto. Watoto walio chini ya umri wa miaka 5 huathirika zaidi. Aina Upungufu wa lishe yenye virutubisho umegaganyika katika makundi mawili nayo ni Nyongea na Unyafuzi(kwashako). Hali hizi zinaweza kutokea kwa pamoja lugha nyingine huitwa Marasmickwashiokor. Nyongea ni hali inayowapata watoto kutokana na kupata lishe yenye upungufu wa chakula aina ya wanga/nishati(kabohaidreti). Unyafuzi ni hali inayotokea ikiwa kuna upungufu wa protini katika lishe kwa ajili ya mahitaji ya ujenzi wa mwili. Kwa nchi zinazoendelea watoto wengi hupata hali zote yaani unyafuzi na nyongea kutokana na umaskini, elimu duni ya lishe,magonjwa n.k. Lishe kuzidi ni hali ya kupata lishe kupita kiasi kinachohitajika mwilini, hupelekea mwili kunenepa zaidi, na kuleta Kiribatumbo, hali hii katika nchi zinazoendelea huzania ni afya kwa mtoto kwa sababu ya kukosa ufahamu. Chanzo/visababishi.

 • Ukosefu wa vyakula vya wanga/nishati, protini, madini na vitamin kwa muda fulani

 • Hali ya njaa ya kudumu inayotokana na umaskini .

 • Kukosa sehemu muhimu ya lishe kama protini, nishati ,madini, vitamin kutokana na gharama za chakula cha aina fulani.

 • Kukosa sehemu muhimu ya lishe kutokana na kukosa ufahamu mzuri kuhusu lishe bora.

 • Magonjwa yaweza kuleta utapiamlo kwa muda mfupi kwa watoto, mfano homa ya matumbo, nimonia, malaria mtoto anakosa hamu ya chakula, ikiwa mtoto anahitaji lishe nzuri kwa ajlili ya ukuaji.

 • Tamaduni katika makabila huwa wanatabia ya kukataza wanawake wajawazito na watoto kula aina Fulani za chakula, tamaduni hizi zinasababisha kuzaliwa kwa watoto wenye tatizo hili.

Dalili. Mtoto anaweza kuwa anaonekana ana afya nzuri kumbe ana tatizo hili, Dalili za utapiamlo(nyongea) kwa watoto ni

 • Uchovu

 • Tumbo kufura

 • Ngozi kukauka

 • Mtoto kulia bila sababu

 • Mtoto kupata magonjwa ya mara kwa mara

 • Mwezo wa kudhibiti joto la mwili hupungua

 • Dalili za unyafuzi(kwashikor) ni mwili ni

 • Kuvimba mwili(miguu, uso n.k)

 • Kuchubuka kwa ngozi

 • Rangi ya ngozi kubadilika(kuongezeka au kuzidi ukilinganisha na kabla ya tatizo),

 • kupata vidonda kwenye miguu,mapaja,viuno na nyuma ya masikio.

 • Pia watoto wengi wenye matatizo ya unyafuzi na nyongea huwa na matatizo mengine kama

 • tatizo la macho kutokana na upungufu wa vitamin A

 • pia huwa na upungufu wa damu

Ukiona mtoto ana dalili hizo wahi hospitali kwa ajili ya vipimo na matibabu Chakula chenye mchanganyiko wenye ubora mfano nafaka,maziwa nyama,samaki na maharagwe inaweza kupunguza tatizo. Elimu itolewe kwa wamama wanaolea watoto na jamii kwa ujumla kuhusu lishe bora. FAhamu zaidi kuhusu utapiamlo hapa, au namna ya kuandaa lishe ya mtoto hapa

33 views0 comments

Recent Posts

See All

Comments


bottom of page