top of page

Wakati gani useme una presha? | ULY CLINIC

Updated: Jun 29, 2020


Ili uweze kusema kuwa una shinikizo la juu la damu, muhudumu wa afya anatakiwa apime kwa umakini na kisahihi shinikizo hilo.

Shinikizo la damu lazime ligawanywe kwenye makundi tofauti ambayo ni shinikizo la kawaida,shinikizo lililo juu, shinikizo hatua ya 1, au shinikizo hatua ya 2;

  • Shinikizo la damu la kawaida ni lile ambalo SBD ni chini ya 120 na DBP ni chini ya tisini au shinikizo chini ya 120/90mmHg

  • Shinikizo la damu la juu ni lile ambalo SBD ni kati ya 120-129 na DBP ni chini ya 80

  • Shinikizo la damu la juu hatua ya 1 ni lile ambalo SBD ni kati ya 130-139 na DBP ni kati ya 80-89 au shinikizo la damu kati ya 130-139/80-89mmHg

  • Shinikizo la damu la juu hatua ya 2 ni lile ambalo SBD ni sawa au zaidi ya140 na DBP ni sawa au zaidi ya 90, au shinikizo la damu lililozidi 140/90mmHG

Kabla ya kumbatiza mtu kuwa ana shinikizo la juu la damu, ni vema vipimo viwili vilivyofanyika katika nyakati mbili tofauti vifanyike. Vipimo vinavyofanyika nje ya ofisi ni vizuri kwa sababu huzuia kupanda kwa shinikizo la damu kutokana na kuona au kutembelea maeneo ya hospitali. Kujipima shinikizo la damu ukiwa nyumbani ni vizuri sana katika kugundua, kujiridhisha na kudhibiti shinikizo la damu, pia kwa mtaalamu wa afya itamsaidia kutumia vipimo hivi ili kurekebisha dozi ya dawa unazotumia kwa wakati na ufanisi zaidi.

Ukiwa nyumbani pima shinikizo la damu nyakati tatu, wakati wa asubuhi, wakati wa mchana na wakati wa jioni. Rekodi kila muda unapopima shinikizo lako la damu na unaweza kumshirikisha daktari wako kuhusu shinikizo hili la damu.

Hakikisha kifaa unachotumia kinafanya kazi vizuri, hakikisha betri ni mpya na endapo umezitumia, hakikisha unazitoa katika kipimo na kuzihifadhi ili zisiishe. Kila unapopima rudisha betri kwenye kipimo.

  • Endapo unatumia kipimo kinachotumia umeme ni vema zaidi kwa sababu husoma vizuri kutokana na umeme kubaki uleule ukilinganisha na matumizi ya betri.

  • Vipimo vya digitali ni vizuri kwa mtu ambaye si mtaalamu wa afya lakini maelekezo ya hapo juu lazima kuzingatiwa

  • Kipimo cha manual kwa mtaalamu wa afya mwenye uzoefu kinashauriwa kutumia zaidi kuliko kipimo cha digitali.

57 views0 comments

Recent Posts

See All

Comentarios


bottom of page